Dola ya Kimarekani inakimbilia 2,600 Tshs muda huu!

Dola ya Kimarekani inakimbilia 2,600 Tshs muda huu!

Vitu vya kawaida kwa sababu hii ni pair tzs/usd kwahiyo ni comparative, that's means uchumi wa marekani unakuwa ukilingalisha na wa tanzania, au uchumi wa tanzania unashuka ukilinganisha na wa marekani.
 
Naombeni mtaalamu kidogo anieleweshe madhara ya hii kwenye bei ya vitu vya nje? Je dollar ikipanda ndo husababisha mfumko wa bei?
Vitu vingi tuna import, ikiwa ina maana ukitaka kwenda kunua vitu china, ili kupata kiwango kile kile cha dollar ambazo ulikuwa unatumia mfano kununua gari mwaka ambao dollar ilikuwa chini, itabidi utumie kiasi kikubwa cha pesa ya kitanzania hivyo ukishaleta hizo bidhaa itabidi uziuze kwa kiasi cha juu cha tshs hence mfumoko. mfano, mwaka juzi assume dollar ilikuwa 2300, leo dollar 2500, so mwaka juzi ulikuwa watumia 2300 kupata dollar moja ila mwaka huu unatumia 2500 kupata dollar 1, kuna ongezeko la 200. Hivyo ukitaka dollar 10000, mwaka juzi ungetumia milioni 23, ila mwaka huu utatumia milion 25, so vitu ambavyo mwaka juzi ulikuwa wavinunua kwa milioni 23, sasa unavinunua kwa miliioni 25, hivyo vikifika lazima uongeze bei kufidia ongezeko la dharama lililotokana na FX.
 
Back
Top Bottom