Ndio maana tunahitaji viongozi wenye akili zisizo za kawaida ili kuweza kutusaidia kila kwenye ugumu kwa kutumia akili zao na maarifa yao na sio watu wenye akili za kawaida ambazo wengi wetu tunazo.
Kiongozi anapaswa kuwa exception kwa kuja na solution pale ambapo akili zote zimeshindwa, na hili hufanyika kwa kutumia resources zilizokuwepo.
Haina maana yakuwa na viongozi kama na wao wanatoka mbele na kutuambia tatizo la Dola ni la dunia nzima na sio kuja na solution yakulimaliza na kulinda Taifa lako na crisis.
Raia anapolalamika kiongozi unapaswa kutoa solution na sio kulalamika.
Kwa sababu Zambia wana tatizo la Dola basi na Tanzania kuwa na tatizo hilo ni sawa, hapa ndio tunapaswa kuona umahili wa viongozi wetu ili tuwe na confidence na kujiona kweli tuko salama tutembee kifua mbele.
Akili iliyokomaa inapaswa kuja na suluhu madhubuti ya kila tatizo na sio blahblah na malalamishi kama ya watu wa kawaida, tunahitaji kuona maana ya kuwa na viongozi na tafsiri sahihi ya uongozi na sio blah blah defensive mechanism.