Domant phone numbers wanazogawiwa wateja wapya

Ina maana umeuziwa na magonjwa ya huyo aliekua na simu...kapime kabisa
 
Ifunge Ili Uepuke Kadhia
Ukiitupa Tu Kule Kwenye Usajili Inasoma Wewe
Ni kweli kuitupa kutaongeza ukubwa wa tatizo, irudishe makao makuu ya mtandao husika na pia toa ripoti kituo Cha polisi ili kuweka ushahidi mapema.
 
Kuna mtu alinitafuta sana nikamwambia Mimi sikujui ila alining'ang'ania sana kesho yake asubuhi akanitumia meseji akasema toka nje nipo hapa kwako nikamuuliza kwangu wapi? Daah mwishowe akaniambia malipo ni hapahapa.
Marcus ungetoka nje mkalipana[emoji23][emoji1787]
 
Warudishie line yao.Wakupe nyingine.
 
Nimemalizia tu kusajili laini ya 062 nashangaa lundo la meseji za namba tofauti tofauti sijakaa vizuri simu za wanawake wakilalamika hovyo kwamba nimewatupa siku nyingi mpaka ikawa kero.
 
Juzikati nipo pale G7 Kinyerezi akapita dogo anasajili laini. Nikakumbuka kurenew laini yangu ya Airtel, salaleee wameshaigawa.
Nikamwambia anisajilie nyingine. Anapigaga maza mmoja ye kila siku anaulizia hamjambo huko? Namwambia hatujambo.....baadae anauliza lakini mbona wewe sio mwenye simu. Mwenyewe yuko wapi. Namwambia umekosea namba. Ameshapiga kama mara 5 na haachi.

Juzi hapa nimetumiwa message, NIAMBIE WE MWANAMKE.....sikuijibu.
Leo tena imekuja nyingine MAMB....nikajua hawa madogo wanatongozana.
Ngoja niendelee nione itakavyokuwa.
 
[emoji3]mkuu hawajatuma hela
 
Sasa solution nini hapo..😥 tufanyaje.namba ndio ivo zinagawiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…