Domant phone numbers wanazogawiwa wateja wapya

Domant phone numbers wanazogawiwa wateja wapya

swali la kizushi. kwanini kila simu wrong call m..yani simu zilizokosewa huwa ni watu wa shinyanga au mwanza.. uani umekaa tu paa namba ngeni inaongea lafudhi ya kisukuma haha majina unakuta shija
Basi hiyo namba ilikuwa ya mtu wa kanda ya ziwa
 
Hii kitu hata mimi imenikuta. Line ya kwanza nilitupa , nikasajili ya pili nayo mambo ni vile vile.
 
Hao 062 wanashida sana

Nilisajili laini hafu jamaa akanipigia nimrudishie simu na laini yake niliyomuibia
 
Mara nyingine kampuni za simu wanawahi kuzifunga namba zetu kabla hatujafanya maamuzi ya kuzirudisha tena.
Kwa mfano mwaka 2019 nilivamiwa hapa kwangu na nikaibiwa vitu vingi vya ndani pamoja na simu zangu mbili zenye laini tatu,nilifanikiwa kurudisha laini mbili,halotel na vodacom lakini Airtel sikufanikiwa kwa vile kipindi kile Airtel shop za hapa mjini hazikua na access ya ku renew namba hivyo nikashauriwa kwenda Kahama (manispaa).
Baada ya miezi minne Airtel waligawa namba hiyo 0785......kwa mteja mwingine.Laini hiyo nilikua nimetumia kwa miaka 11 tangu 2008.Mmiliki mpya alisumbuliwa na ndugu zangu wengi waliozoea kunipata kwa namba hiyo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka wasichukue namba yako weka buku 2 then iache hata miaka kumi utaikuta
 
Hili jambo linakera sana.mpaka unaona lile zoezi lakusajili simu lilikua halina maana.lilikua upotevu tu wa muda.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli na wengi wanaopiga wanaongea lugha za asili.
 
Hii kadhia huenda inawakuta wengi, nilikwenda ofisi ya 062 kupata line ya simu siku ya Ijumaa wiki iliyopita nikapewa na kuanza kuitumia, inavyoonekana hii namba ilikuwa inamilikiwa na mtu mwingine huko nyuma akaitelekeza, kinachonikuta hadi sasa ni wanawake 11 wananitumia meseji na kupiga simu tuhuma nyingi tu
  1. Ati nimetelekeza mimba
  2. Nimetelekeza watoto
  3. Nadaiwa ada za watoto
  4. Nakwepa kulipa kodi ya chumba
  5. Na meseji za mahusiano mapya nyingi
  6. Wanaume nao wananishambulia kuwa niachane na wapenzi wao wengine wananisaka
Kwa mtindo huu wapo wanaouziwa matatizo na mitandao ya simu kwa kugawa namba hizo kwa wateja wapya, imagine mtu anaambiwa atasakwa awe dead au live.
Na hili nalo Mkalitazame
 
Back
Top Bottom