Donald Trump apatikana na hatia ya makosa yote 34 katika kesi ya kughushi nyaraka na kutaka kuficha kuhusu hela alizomlipa pornstar ili akae kimya

Falsification ya documents siyo crime, ni misdemeanor. Inakuwa crime tu iwapo inafanywa kwa lengo la kuficha makosa mengine. Makosa mengine waliyokuwa wanaficha ndiyo yaliyomtia hatiani
 
Kina Mobetto wana la kujifunza hapa, wauza papa/wacheza ngono wenzao wanapewa pesa ndefu kuweka mambo faraghani. Kina Mobetto wakilalwa na Diamond tu wanaitisha press conference na hawaambulii chochote.
 
Trump wa sasa ni liability kwa chama cha Republican ukilinganisha na Trump wa pre-2021. Ni kwa vile tu Republicans hawana option nyingine kwenye ballot box kuelekea mwezi Novemba, hivyo wako kwenye "point of no return".

Hizi convictions zinazoendelea hivi sasa huenda zikaigharimu Republican kwenye uchaguzi ujao na kuipelekea kukosa idadi kubwa ya kura za urais kutoka kwa baadhi ya voting blocs hasa independents.
 
Donald Trump apatikana na hatia ya kughushi nyaraka.
Upo sahihi.

Synthesizer jina kuuuubwa la kiuandishi hapa JF lakini kumbe hana umakini wa anachokiandika au, kibaya zaidi, labda akisoma kinachoendelea huko duniani haelewi!

Hakuna kosa wala kesi duniani ya kumlipa mtu asitoe siri ya kulala nae.
 
..Marekani inapitia kipindi kigumu kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

..Donald Trump sio aina ya kiongozi ambaye Marekani inamhitaji kwa sasa hivi.
na kwa pamoja wananchi 9 wamemkuta na hatia.
Wako 12, sio 9, hakunaga 9.

Na hakuna wakati ambao USA ilikuwa haipiti kipindi kigumu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Maraisi wamepigwa risasi kuanzia enzi za Lincoln. Kumekuwa na mavita toka Civil War, World War, Vietnam, Cold War, Iraq, na kadhalika. Kiuchumi kumekuwa na ma Great Depression, ma Oil Crisis, ma Covid recession, ma Morgage Crisis, na kadhalika. Kijamii kumekuwa na migogoro ya kibaguzi toka Jim Crow, abolition movements, civil rights movements, na kadhalika.... na kadhalika, na kadhalika.

Kama Trump hafai hafai, hakuna wakati ambao angefaa, hakuna wakati ambapo nchi yeyote duniani huwa pametulia panafaa kiongozi mbovu....
 
kwakua imethibitika,
Donald Trump anawajibika kutumikia athabu atakayopewa kulingana na makosa yake, na hiyo ndio maana ya haki na wajibu katika utawala wa sheria 🐒
 
Atalipa faini, labda tu hakimu amkazie adhabu moja.

Ngoja wampunguzie speed ya kugombea urais. Ni msumbufu.

Wanawake wengine Mungu sijui aliwaumba so special, haya bana

Namkumbuka na yule mwanamke Monica alikuwa akilala na Clinton huko white house.
 
Jury of his peer
 
Timu yake yote ya kampeni na biashara wamepatikana na makosa ya uhalifu mahakamani!
 
Lakini Stormy si alipewa hela asisema kitu na afunge mdomo. Wanawake wana shida gani?
Pesa atazopata sasa hivi ni nyingi kuliko hizo alizopewa na Trump afunge mdomo, na umaarufu juu yake.
 
Huyo mzee kaitingisha sana establishment ya Marekani...waliojiona wao ndo familia za siasa zote kazitingisha....Ukimuona kisiasa ni kama hana wafuasi na kumbe anawafuasi.
Wanamtafuta mpaka basi....mara impeachment, mara majahaba, mara mambo ya kodi, yaani hawampumzishi.Angekua mtu mwepesi kihisia aliishakimbia mchezo zamani sana.
Huyu mzee kuna kitu anacho maana sio kwa kumsumbua hivi
 
Timu yake yote ya kampeni na biashara wamepatikana na makosa ya uhalifu mahakamani!
Mimi nafikiri haya yote yanaanzia kwenye sababu kuu za kisiasa.
Hakuna binadamu msafi, achilia mbali wafanyabiashara..mara nyingi ukiona mtu anaanza kupata kesi ujue kuna watu kawagusa au kawaharibia kutokana na kile anachofanya
 
Mimi nafikiri haya yote yanaanzia kwenye sababu kuu za kisiasa.
Hakuna binadamu msafi, achilia mbali wafanyabiashara..mara nyingi ukiona mtu anaanza kupata kesi ujue kuna watu kawagusa au kawaharibia kutokana na kile anachofanya
Kumbe sio kesi za kusingiziwa ila unachodai ni kwamba wengine wachafu nao hawajaguswa, huu sio utetezi mzuri wenye mashiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…