Donald Trump apatikana na hatia ya makosa yote 34 katika kesi ya kughushi nyaraka na kutaka kuficha kuhusu hela alizomlipa pornstar ili akae kimya

Donald Trump apatikana na hatia ya makosa yote 34 katika kesi ya kughushi nyaraka na kutaka kuficha kuhusu hela alizomlipa pornstar ili akae kimya

Mkuu, hii kesi leo wazee wa baraza wamemtia hatiani Donald Trump kwa makosa yote 34 ya kughushi nyaraka kuhusiana na pesa alozitoa kwa yule mwanamke zinoitwa "Hush Money".

Hivyo akiwa madarakani akawezesha nyaraka kughushiwa yaani kuchakachua na kurekebisha mahesabu kwamba fedha alozilipa ama ni ndogo au hakikuwepo kabisa,

Hivyo hii kesi yahusu Hush Money au Hush Money Trial.

NB
Hizi fedha za hash au Hush Money ni zile fedha unozilipa kwa mchepuko ili asije kutoa siri/taarifa zako nje au kumfunga mdomo pale siri au taarifa hizo zinapoleta dhahama kwako au familia yakop na mstakabali mzima wa maisha yako.
Falsification ya documents siyo crime, ni misdemeanor. Inakuwa crime tu iwapo inafanywa kwa lengo la kuficha makosa mengine. Makosa mengine waliyokuwa wanaficha ndiyo yaliyomtia hatiani
 
Kina Mobetto wana la kujifunza hapa, wauza papa/wacheza ngono wenzao wanapewa pesa ndefu kuweka mambo faraghani. Kina Mobetto wakilalwa na Diamond tu wanaitisha press conference na hawaambulii chochote.
 
..Trump ni mbinafsi, tapeli, na mhalifu, toka zamani.

..sasa hivi anatumia siasa kufichama asijibu kwa makosa aliyoyafanya.

..Marekani inapitia kipindi kigumu kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

..Donald Trump sio aina ya kiongozi ambaye Marekani inamhitaji kwa sasa hivi.

..waliomtia hatiani Donald Trump ni wananchi wenzake [ jury ] waliosikiliza tuhuma na utetezi dhidi yake na kwa pamoja wananchi 9 wamemkuta na hatia.
Trump wa sasa ni liability kwa chama cha Republican ukilinganisha na Trump wa pre-2021. Ni kwa vile tu Republicans hawana option nyingine kwenye ballot box kuelekea mwezi Novemba, hivyo wako kwenye "point of no return".

Hizi convictions zinazoendelea hivi sasa huenda zikaigharimu Republican kwenye uchaguzi ujao na kuipelekea kukosa idadi kubwa ya kura za urais kutoka kwa baadhi ya voting blocs hasa independents.
 
Donald Trump apatikana na hatia ya kughushi nyaraka.
Upo sahihi.

Synthesizer jina kuuuubwa la kiuandishi hapa JF lakini kumbe hana umakini wa anachokiandika au, kibaya zaidi, labda akisoma kinachoendelea huko duniani haelewi!

Hakuna kosa wala kesi duniani ya kumlipa mtu asitoe siri ya kulala nae.
 
..Marekani inapitia kipindi kigumu kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

..Donald Trump sio aina ya kiongozi ambaye Marekani inamhitaji kwa sasa hivi.
na kwa pamoja wananchi 9 wamemkuta na hatia.
Wako 12, sio 9, hakunaga 9.

Na hakuna wakati ambao USA ilikuwa haipiti kipindi kigumu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Maraisi wamepigwa risasi kuanzia enzi za Lincoln. Kumekuwa na mavita toka Civil War, World War, Vietnam, Cold War, Iraq, na kadhalika. Kiuchumi kumekuwa na ma Great Depression, ma Oil Crisis, ma Covid recession, ma Morgage Crisis, na kadhalika. Kijamii kumekuwa na migogoro ya kibaguzi toka Jim Crow, abolition movements, civil rights movements, na kadhalika.... na kadhalika, na kadhalika.

Kama Trump hafai hafai, hakuna wakati ambao angefaa, hakuna wakati ambapo nchi yeyote duniani huwa pametulia panafaa kiongozi mbovu....
 
Katika kesi iliyokuwa ikimkabili Raisi wa zamani wa Marekani Donald Trump iliyohusu kutumia fedha isivyo halali kumlipa mwanamke aliyelala naye, wazee wa mahakama (jury) 12 wamefikia uamuzi kwamba Donald Trump ana hatia na hivyo lililobaki na jaji kutoa hukumu dhidi ya Raisi huyu wa zamani wa Marekani.

Donald Trump alikuwa akikabili mashitaka 34 ya kughushi nyaraka kuhalalisha malipo aliyofanya kwa mchezaji wa sinema za X, Stormy Daniels, ili amfichie siri za kutembea nae. Amepatikana na hatia katika mashitaka yote 34. Malipo hayo aliyafanya kwa kutumia fedha za kampuni na kujaribu kughushi nyaraka kuhalalisha malipo hayo kama vile ni sehemu ya malipo ya huduma za kibiashara za kampuni yake, ambalo ni kosa nchini Marekani.

Bado haieleweki ikiwa jaji huyu atatoa hukumu ambayo itatia ndani Donald Trump kutumikia kifungo gerezani. Trump atahukumiwa tarehe 11 July, na hukumu katika kesi kama hii inaweza kuwa hadi kufungwa miaka minne gerezani, au faini, au kifungo kifupi au kifungo cha nje. Na anaweza kufungwa gerezani na bado akawa raisi wa Marekani, ambapo itabidi atolewe gerezani kwenda kukabili majukumu ya uraisi White House. Kwa sasa akifungwa gerezani itabidi apatiwe ulinzi kama raisi mstaafu akiwa ndani ya gereza. Hukumu hii haimuondolei haki yake ya kuendelea na kugombea uraisi, japo anakuwa mgombea uraisi mhalifu wa kwanza nchini Marekani. Inajulikana kwamba chama chake cha Republicans kinaweza kuamua Trump asiwe mgombea wao wa uraisi, japo uwezekano huu ni mdogo sana kwa jinsi anavyoungwa mkono ndani ya chama.

Kesi hii imechukua wiki sita kukamilishwa, na inatarajiwa kwamba Trump atakata rufaa dhidi ya hukumu hii.

Pia Soma:

- Marekani: Donald Trump ashtakiwa kwa pesa haramu anazodaiwa kumlipa nyota wa filamu za ngono

- Trump atakiwa kumlipa mwanamke aliyemdhalisha Kiongono Tsh. Bilioni 211

---

Donald Trump found guilty in hush money case - becoming first ex-president to be criminally convicted​

Donald Trump has become the first former US president to be criminally convicted.

In a historic decision, a New York jury has found him guilty of falsifying business records to commit election fraud.

He was found guilty of all 34 counts he faced. Unanimity was required for any verdict.

The former president is set to be sentenced on 11 July.

Speaking outside the court, Trump said the conviction was a "disgrace" and that he is "a very innocent man".

He said the trial was "rigged" and that the judge was "conflicted" and "should never have been allowed to try this case".

Trump was at the centre of a scheme to cover up "hush money" payments to buy the silence of a porn star in the days before the 2016 election.

When revelations by Stormy Daniels of a sexual liaison with Trump threatened to upend his presidential campaign, he directed his lawyer to pay her $130,000 (£102,000) to keep her quiet.

The payment buried the story, and Trump was later elected to be the 45th president of the United States.

Trump watched the jurors dispassionately as they were polled to confirm the guilty verdict.

The Speaker of the US House of Representatives Mike Johnson said: "Today is a shameful day in American history."

The trial in the Manhattan Criminal Court heard how the backdrop to the crime was a scandal in the Trump campaign a month before the 2016 election.

A video tape from the TV show Access Hollywood was made public, in which Trump was caught on a microphone talking in lewd terms about groping women ("When you're a star they let you do it, grab them by the p***y. You can do anything.")

The trial heard how it was viewed as a "crisis" within Team Trump and that the campaign was soon facing another.

Ms Daniels, an adult film actor, claimed she had a sexual encounter with Trump in Lake Tahoe, Nevada, in 2006.

Fast-forward 10 years and, as he ran for office, she was hawking her story.

The details, as heard in this trial, were that she had met Trump at a golf tournament, and he had invited her to dinner.

She arrived at his hotel suite to find him dressed in satin pyjamas, until she asked him to change.

At one point, he produced a magazine, and she told the court she spanked him "right on the butt".

Later, she emerged from the bathroom to find him lying on the bed in a T-shirt and boxer shorts, and they ended up having sex.

Trump denies the liaison took place.

Her plan to sell her story was communicated to Trump by David Pecker, former publisher of the National Enquirer magazine.

He was a friend of Trump and operated a "catch and kill" scheme on his behalf, to catch negative stories and kill them before they could be published.

He'd already paid $150,000 (£117,000) to silence Karen McDougal, a Playboy model with a story of a 10-month affair with Trump.

Sky News
kwakua imethibitika,
Donald Trump anawajibika kutumikia athabu atakayopewa kulingana na makosa yake, na hiyo ndio maana ya haki na wajibu katika utawala wa sheria 🐒
 
Atalipa faini, labda tu hakimu amkazie adhabu moja.

Ngoja wampunguzie speed ya kugombea urais. Ni msumbufu.

Wanawake wengine Mungu sijui aliwaumba so special, haya bana

Namkumbuka na yule mwanamke Monica alikuwa akilala na Clinton huko white house.
 
Convince me the jury was biased against Trump, then I will consider whether you may have a valid point in what you say. Remember, the Trump defense team accepted this jury.

Overturning a guilty verdict on 34 felony counts is one hell of an uphill task buddy, don't be so optimistic about the appeal.
Jury of his peer
 
Acha sheria ichukue mkondo wake. Ameshitakiwa mbele ya mahakama kama raia mwingine yeyote wa kawaida. Ukishasema kesi ilikuwa kwenye eneo la democrats una sahau kuwa alizaliwa na kupatia umaarufu wake kwenye eneo hilo hilo. Mashahidi wote waliotumika kumtia hatiani ni marafiki zake wa zamanı aliofahamiana nao kwa muda mrefu sana.
Timu yake yote ya kampeni na biashara wamepatikana na makosa ya uhalifu mahakamani!
 
Lakini Stormy si alipewa hela asisema kitu na afunge mdomo. Wanawake wana shida gani?
Pesa atazopata sasa hivi ni nyingi kuliko hizo alizopewa na Trump afunge mdomo, na umaarufu juu yake.
 
Huyo mzee kaitingisha sana establishment ya Marekani...waliojiona wao ndo familia za siasa zote kazitingisha....Ukimuona kisiasa ni kama hana wafuasi na kumbe anawafuasi.
Wanamtafuta mpaka basi....mara impeachment, mara majahaba, mara mambo ya kodi, yaani hawampumzishi.Angekua mtu mwepesi kihisia aliishakimbia mchezo zamani sana.
Huyu mzee kuna kitu anacho maana sio kwa kumsumbua hivi
 
Timu yake yote ya kampeni na biashara wamepatikana na makosa ya uhalifu mahakamani!
Mimi nafikiri haya yote yanaanzia kwenye sababu kuu za kisiasa.
Hakuna binadamu msafi, achilia mbali wafanyabiashara..mara nyingi ukiona mtu anaanza kupata kesi ujue kuna watu kawagusa au kawaharibia kutokana na kile anachofanya
 
Mimi nafikiri haya yote yanaanzia kwenye sababu kuu za kisiasa.
Hakuna binadamu msafi, achilia mbali wafanyabiashara..mara nyingi ukiona mtu anaanza kupata kesi ujue kuna watu kawagusa au kawaharibia kutokana na kile anachofanya
Kumbe sio kesi za kusingiziwa ila unachodai ni kwamba wengine wachafu nao hawajaguswa, huu sio utetezi mzuri wenye mashiko.
 
Back
Top Bottom