Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Imetangazwa dakika chache zilizopita na vyombo vya Habari

=====

Rais wa zamani Donald Trump kutoka chama cha Republican, ameshinda Uchaguzi wa Marekani.
View attachment 3144969
Chanzo: Spectator Index

Donald Trump ameoa mara tatu, Ivana na Marla Maples, mke wa kwanza na wa pili mtawalia ambao wote ametalikiana nao. Mke wake wa sasa ni Bi Melania.

Bwana Trump ana watoto watoto watano, watatu wa kiume Donald Trump Jr, Eric, Barron na watoto wawili wa kike Ivanka na Tiffany.

Rais huyo wa Zamani wa Marekani alizaliwa Juni 14 mwaka wa 1946, mjini New York, akiwa mtoto wa tano kati ya watoto sita.

Babake Fred alikuwa tajiri aliyemilki majumba na babu zake Trump walikua wahamiaji kutoka Ujerumani.

Mamake Mary alikuwa mzaliwa wa Scotland.
View attachment 3144983
Tangu utotoni, Trump alikuwa mtundu na wazazi wake walimpeleka shule ya msingi iliyofadhiliwa na jeshi mjini New York.

Baadaye alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, kitivo cha elimu ya biashara mwaka wa 1968.

Alifanya kazi katika kampuni ya babake ambaye aliendesha biashara ya kuuza nyumba kwa raia wa kipato cha kadiri, viungani mwa New York.

Hata hivyo Donald Trump alikuwa na ndoto ya kufanya biashara nje ya makaazi ya Queens na Brooklyn.

Aliwekeza katika biashara kubwa ya ujenzi na kuweza kujenga mojawapo ya mijengo ya kifahari zaidi nchini Marekani. Alifanikiwa kutokana na sera ya kiuchumi iliyowekwa na utawala wa Reagan miaka wa 1980.

Yapo mahoteli, viwanja vya mchezo wa gofu, makazi ya kifahari, majumba ya kamari kutoka Carlifonia hadi Mumbai nembo yake ikiwa ni Trump.

Ameandika Riwaya kadhaa kuhusu biashara, huku umaarufu wake uking'aa zaidi katika makala yanayoelezea maisha halisi, "The Apprentice," katika runinga ya NBC. Hata hivyo alitupwa nje ya makala hayo baada ya kutoa kauli zilizowakera raia wa Mexico.
Ameshinda pemnyslivia yenye vote 19 sasa bado kura tatu afikishe kura 270 aukwae rasmi urais. Ila katika yale majimbo manne ya swing states ambayo bado wanahesabu anaongoza kwa mbali ndio maana inatangazwa ameshinda. Kwa trend ya majibu jinsi kura zinavyohesabiwq ni muijiza kushindwa.

Azam na wachambuzi wao wenye chuki waone aibu. Rabi na Shakur walikuwa wanaingiza ushabiki. Mchambuzi wa Azam ambaye huwa anachambua objectively mambo ni Thabit Mlangi lakini huwa hawamuiti mara kwa mara..

Mungu ametenda kwa Trump

Nb; pia wamechukua udhibiti wa bunge la Senate.
 
Mkuu ipo hivi. Majimbo ya marekani (states) zimepewa idadi fulani ya electoral college kulingana na uwingi wa watu. Mfano carlifonia ina electoral collage 54. North Carolina 16, etc.

Mhombea anayeshinda jimbo husika kwa kura za wananchi pia anashinda hizo electoral college. Mfano kamala kashinda califonia ina maana pia kapata electoral college za carlifonia.

Kwa hivyo ni wananchi ndo huamua mshindi na sio hao wajumbe 538 wa electoral college.

Umeelewa?
Angalia hapa Hillary Clinton alimshinda Trump kwenye kura za wananchi hivyo kama kweli wananchi ndio huamua nani awe Rais wao basi Hillary Clinton ndiye alipaswa kuwa Rais na sio Trump.
 

Attachments

  • Screenshot_20241106_105756_ChatGPT.jpg
    Screenshot_20241106_105756_ChatGPT.jpg
    265 KB · Views: 2
Mifumo yao ni ile ya zidumu fikra za mwenyekiti?
Isitoshe tayari uchumi wa Marekani umekuwa ukiyumba ingawa watu waaminishwa vingine, vita ya Gaza ndo imekuwa sababu ingine kubwa kwa sababu wale watu wa kutoka mashariki ya kati wamekuwa wakipiga kelele na wameeleweka.
 
What if akishindwa kwenye kura za mabwanyenye?
Kura za mabwanyenye ndio hizo ameshinda, mkuu. Popular votes ni kura za umma.

Halafu hizo unazoita kura za mabwanyenye ni uelewa potofu, kwa sababu zinategemea kura za umma (popular votes). Bila popular votes hakuna electoral votes.

Wale wajumbe 538 wanapiga kura kwa kuzingatia ushindi wa mgombea kwenye kila jimbo.
 
Isitoshe tayari uchumi wa Marekani umekuwa ukiyumba ingawa watu waaminishwa vingine, vita ya Gaza ndo imekuwa sababu ingine kubwa kwa sababu wale watu wa kutoka mashariki ya kati wamekuwa wakipiga kelele na wameeleweka.
Ashinde tu Trump akasitishe vita Ukraine na kupigana na mashoga.
 
Putin siyo mbaya kama unavyoaminishwa na CNN,NK!
Putin ni mtu mbaya sana sawa sawa kabisa na Shetani. Je, unaujua ubaya au uovu wa Putin tangu akiwa boss wa Shirika la Ujasusi la KGB la Urusi ya zamani (USSR) ?
Putin ndiye aliyeanzisha na kuboresha pakubwa Sana Maabara (Kiwanda) kikubwa Sana cha KGB/FSB cha Kutengeneza sumu za Kuulia Watu, hususani wale watu wakosoaji wa Serikali ya Urusi na wanaharakati. Kila siku ndani ya Urusi Watu wanauawa kimya kimya kwa kuwekewa sumu na Mawakala wa Siri wa Mamlaka ya Ujasusi ya nchi hiyo KGB/FSB.

Ukiwa nchini Urusi ni hatari tupu, kifo mkononi. Ukiwa nchini Urusi, kumkosoa Putin au kukosoa utawala wake ni KUJIKATIA TIKETI YA KIFO.
 
Ashinde tu Trump akasitishe vita Ukraine na kupigana na mashoga.
Ni kweli kwani watu wamepiga sana pesa. Maseneta wamekuwa wakituhumiwa kupoteza fedha ambazo Biden amekuwa akiahidi kuzipeleka Ukraine lakini fedha hizo zaishia hewani na wale wenye maviwanda ya silaha nao wameipiga sana Marekani kiasi cha kuifanya FR kuchapisha pesa kila mara.
 
Chombo gani wewe hapo BBC,CNN na aljazeera wanasema ameshinda majimbo mawili makubwa bado mengine wewe jamaa muongo sana

USSR
Sasa hapo Lumumba akili ndogo utajuwa ya Dunia kweli ....wee seto huko uchawani
 
Putin ni mtu mbaya sana sawa sawa kabisa na Shetani. Je, unaujua ubaya au uovu wa Putin tangu akiwa boss wa Shorika la Ujasusi la KGB la Urusi ya zamani (USSR) ?
Putin ndiye aliyeanzisha na kuboresha pakubwa Sana Maabara (Kiwanda) kikubwa Sana cha KGB/FSB cha Kutengeneza sumu za Kuulia Watu, hususani wale watu wakosoaji wa Serikali ya Urusi na wanaharakati. Kila siku ndani ya Urusi Watu wanauawa kimya kimya kwa kuwekewa sumu na Mawakala wa Siri wa Mamlaka ya Ujasusi ya nchi hiyo KGB/FSB.
Ukiwa nchini Urusi ni hatari tupu, kifo mkononi.
Nani kakusimulia hayo?

Weye waaminikila unokisikia?

Kuna ushahidi wa tuhuma hizo?
 
Ni kweli kwani watu wamepiga sana pesa. Maseneta wamekuwa wakituhumiwa kuupoteza fedha ambazo Biden amekuwa akiahidi kuzipeleka Ukraine lakinifedha hizo zaishia hewani na wale wenye maviwanda ya silaha nao wameipiga sana Marekani kiasi cha kuifanya FR kuchapisha pesa kila mara.
AIsee
 
Back
Top Bottom