Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Wamarekani ni wabaguzi sana hasa Hawa weusi,si ajabu ndo mana wamarekani weusi wanabaguliwa mpaka Dunia ya Leo ya mwangaza.

Wamempiga chini Kamala kwa sababu ya uanamke wake na ngozi yake yenye uweusi ndani yake.Naamini wale manguli weupe kama Trump,Elon musk bado wanaamini wao ndo Wana haki na Taifa Hilo,na hata kwa Obama nafikiri walimchagua ili kujarbu kubalance ubaguzi ila hata Leo nafikiri ni doa kubwa kwao.

I hope wanafuraha Sasa mzungu pure ndo kashinda.Suala la Vita na mambo mengine hayatobadilika hata chembe,walichojarbu kuzuia TU ni taifa lao Kua na Mtu mweusi Tena Mwanamke.Tuendelee kuamini hiki kizazi cha hawa weupe ambao waliwahi kututawala,kutubagua,kurunyanyasa na kutupora kua ni Mitume ktk zama hizi
Mkuu, usimtee sana Kamala na Democrats. Awamu yao imekuwa mbovu mno katika historia ya Marekani. Isitoshe, sera zao nyingi ni fedheha kupindukia.
 
Kile kitendo chake cha kuanza kampeni ndicho kimewagharimu sana Democrats. Inaonesha hawakuwa na uhakika na wanachokifanya - wabahatishaji hata kwenye mambo ya msingi kama urais wa nchi!

Hebu fikiria kama Joe Biden angeshinda tena!

Hilo ndilo limewafanya wafuasi wao wengi wapoteze imani na chama. Halafu, Kamala hakuwa na muda mrefu wa kujiandaa. Miezi mitatu tu ya kampeni halisi, wakati Trump tayari alikuwa mkongwe majukwaani?

Ndiyo maana siku JB anaachia ngazi na Kamala akatangazwa kuwa mgombea rasmi, Trump alidai angeshinda asubuhi na mapema. Akawashukuru JB na Democrats kwa kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho.
Yes, ni kweli kabisa.

Joe Biden alipaswa atangaze angalau mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi kwamba hataweza kugombea tena kiti cha uRais ili kuwapa nafasi Wanachama wa Chama chake cha Democrats muda wa kutosha wa kumuandaa Mgombea mwingine badala yake.
 
Bila popular votes huwezi kupata electoral votes. Hizo zinategemeana kabisa. Unadhani kwa nini Trump amepata electoral votes 16 za jimbo la Florida?

Kwa sababu ameshinda jimbo hilo. Bila kushinda jimbo husika, unakosa electoral votes zake.
Sasa ina maana gani hii? Mbona ni kupoteza muda kusiko na maana yoyote.

Kama kushinda popular votes ndiyo kushinda electoral votes kwanini isiachwe tu hiyo popular votes?

Hillary Clinton alipogombea na Donald Trump, Hillary Clinton alimshinda Trump kwenye popular votes lakini Trump akamshinda Hillary Clinton kwenye electoral votes na kupelekea Trump kuwa Rais wa Marekani.

Sasa hoja yako ya kwamba popular votes na electoral votes zinaendana mbona kama haina uhalisi?
 
Chama cha Democrats kilikosea kupiga mahesabu vizuri kuhusiana na suala la Uchaguzi huu. Kampeni za Uchaguzi huu walipaswa kuanza mapema mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi wenyewe kwa kumuweka Wazi mapema Mgombea wao mtarajiwa ili kumnadi kwa Wapiga Kura.
Kamala Harris aliibuka tu kama surprise au kama ambush kwa Wapigakura.
Ama walidhani Joe Biden angeweza kupiga muhula mwingine wa miaka 4, au walikuwa wanapoteza muda ili Kamala Harris asipitie ile michakato, ushindani na michujo chamani kwake.

Nadhani hii ya pili ndiyo sahihi zaidi, maana kila mtu alijua Joe Biden hangeweza tena kuwa rais.

Hatua yao ya kujaribu kumrahisishia njia Kamala ndiyo imewagharimu kukubwa.
 
Trump ameshinda katika ngome zote zenye upinzani mkali:
1. Georgia
2. North Carolina
3. Pennsylvania
4. Wisconsin

Bado 3
5. Arizona
6. Michigan
7. Nevada

Nimeamini huwezi kushinda uraisi wa Marekani bila kushinda jimbo la Pennsylvania!
Na hapo Pennsylvania si ndipo walipomchapa risasi? Kura za huruma probably ukizingatia electoral votes zipo za kutosha pale.
 
Ni rahisi na ungeelewa mifumo Yao ni mizuri sana
Kwani wananchi wakipiga kura moja kwa moja (popular votes) kuna shida gani?

Au nao ni wezi wa kura tu kama Afrika ndiyo maana hawawaamini wananchi wao kuwa na maamuzi ya mwisho?
 
Back
Top Bottom