Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Sio kweli. Kama wananchi (popular votes)ndiyo wanaoamua nani awe Rais wao basi Hillary Clinton angekuwa Rais wa Marekani alipogombea na Trump maana Hillary Clinton alimshinda Trump kwa zaidi ya kura milioni tatu lakini Trump alitangzwa mshindi wa Urais baada ya kushinda kwenye electoral votes.

Sasa ubabaishaji huu una maana gani? Kwani wananchi wakifanya maamuzi moja kwa moja kuna shida gani?

Au wananchi wa Marekani hawana IQ za kujua nani anafaa kuwa Rais wao ndiyo maana hawaaminiwi badala yake wanachaguliwa Rais na watu wasiozidi 538.
 
Sasa ina maana gani hii? Mbona ni kupoteza muda kusiko na maana yoyote.

Kama kushinda popular votes ndiyo kushinda electoral votes kwanini isiachwe tu hiyo popular votes?

Hillary Clinton alipogombea na Donald Trump, Hillary Clinton alimshinda Trump kwenye popular votes lakini Trump akamshinda Hillary Clinton kwenye electoral votes na kupelekea Trump kuwa Rais wa Marekani.

Sasa hoja yako ya kwamba popular votes na electoral votes zinaendana mbona kama haina uhalisi?
Hiyo electrol vote naona ni km inabalance maamuzi ya majimbo yote. Kwa maana wanaondoa ule uwezekano wa majimbo machache yenye watu wengi kufanya maamuzi ya kuamua nani awe rais wa marekani.

Mfano kwa hapa kwetu kanda ya ziwa kwa wingi wao wanaweza wao ndio wanatuchagulia rais, wakati sisi watu wa kaskazini kwa vile tupo wachache tunakuwa hatuna namna
 
Ni aibu kwa bara la Afrika,lenye natural resources na human resources ya kutosha, kutembeza bakuri ughaibuni na mbaya zaidi viongozi wamekuwa madalali na makuwadi wa rasilimali.
Viongozi wabinafsi ni kujilimbikizia mali utazani wakifa wanaondoka nazo
 
Uchaguzi wa kupitishwa na watu 270 kati ya 538 wa Electoral College kuwa Rais wa USA hata kama raia wengi wa USA hawajakuchagua?
Halafu wanazishadadia na kuzisema nchi zingine kwamba hazina demokrasia na kubeza chaguzi zake kwamba zimegubikwa na udanganyifu?
Waendelee na mfumo wao huo wa kiimla; lakini waache kuingilia mifumo ya mataifa mengine, maana hata wao hawana demokrasia ya kweli.

Minne; USA siyo URT.
Omba kueleweshwa haraka, mkuu. Vinginevyo utaendelea na ujinga wako kichwani hadi mwisho wa dunia.

 
.Wamarekani walionekana kumkubali sana mwanamama Kamala Haris. Ila lilipofika suala la kupiga kura ya urais, wakatafakari mara ya pili. Kuwa Mwanamke aongoze nchi? Inawezekana? Hapo ndipo wakatulia na kupata majibu,wakamtosa wakamchagua kaburu Trump. Watanzania tuwe na la kujifunza hasa linapokuja
suala la kuongoza nchi.
HAKUNA KAMA MAMA WEWE ENDEELEA TU NA CHUKI ZAKO
 
Back
Top Bottom