Donald Trump: I Will Lock Mugabe, Museveni in Prison

Status
Not open for further replies.


Usiwe mjinga, D.Trump hajawahi kusema hayo maneno na wala Trump hana mpango na Afrika, na kwanza Afrika haipo kwenye vipaumbele vya US foreign policy na ndiyo maana Afrika haijawahi kuwa kwenye campaign theme za USA hata siku moja ukiachilia Obama na uhusiano na baba yake lkn hiyo siyo foreign policy ya USA kwa maana maslahi ya USA Afrika ni madogo sana!

Hayo maneno ni ya kupakaziwa na makasimu wa D.Trump ambao wanampakazia mengi sana ili tu wamchafue lkn D.rump hajasema hayo maneno na wala kwanza hana mpango na Afrika, kusema maneno kama hayo unahitaji mtu mwenye affinity na Afrika sasa D.Trump hana affinity yoyote na Afrika...
 
Kama ni kweli..
Basi itakua ni propergander za kampenii..
Marekani haitawaliwi na Akili ya mtu mmoja Kama Tanzania
 
Hiyo taarifa nimeipata seheme mbalimbali kwenye mitandao..Kama wamempkazia hilo ni swala jingine. Hiyo point ya kwamba US haina interest na Africa naipinga. Unadhan misaada US inayowapatia africa ni burebure tu. Africa kuna mali nyingi na ndo mana US na vimisaada vyao huku wakichukua mali zetu nyingi tu. Ni hii ni kwa nchi nyingi tu zinazitoa misaada Africa.
 


Elewa nilichosema sijasema kwamba USA haina maslahi Afrika kwa 0% bali nimesema maslahi ya USA Afrika ni madogo sana kuweza kushape foreign policy yake ukilinganisha na maslahi ya USA ASIA, Marekani Kusini au hata Ulaya, Afrika ni Bara la mwisho ambalo USA hata inajali kama lipo au halipo huwo ndiyo ukweli!
 
This man is unaware of Public International law principle on National/state/country sovereignity. He has no power to do so. Such acts will amount to "aggression", something which is not condoned by an civilized nation.
 
Huyu jamaa ni mwiba kwa Waafrika! atarudisha ukoloni...
 
Weka evidence..Nionavyo mm Africa ni bara linaloangaliwa kwa jicho la tatu na nchi za ulaya na US na interest ni kubwa tu.
 
Weka evidence..Nionavyo mm Africa ni bara linaloangaliwa kwa jicho la tatu na nchi za ulaya na US na interest ni kubwa tu.


Huko ni kujidanganya tu, unajua sisi Waafria miaka yote tumekuwa tukiishi kwa kijidanganya na tumelelewa hivyo, ni sawa na tunavyoaminishwa kwamba Bara letu la Afrika ndio Bara tajiri Duniani, hiyo siyo kweli, kila Bara lina utajiri na la kwetu halina upekee wowote ule kwanza Bara letu la Afrika ndiyo moja kati ya mabara yenye matatizo makubwa ya kijiografia kam ukame, upungufu wa vyanzo vya maji, kuna Jangwa kubwa Duniani Sahara, sehemu kubwa ya Afrika ni ukame tupu, ukilinganisha na Mabara mwengine!

Hivyo kwa USA Afrika yetu siyo priority na haijawahi kuwa hivyo, sehemu zote ambazo USA ina maslahi makubwa jambo la kwanza hujenga Military base sasa ni wapi kuna Military base kubwa ya maana Afrika ya USA?
Kwanza kitengo pekee cha USA kinachoshughulikia Afrika cha USA kiko Mji wa Stuttgart, Ujerumani kiitwacho AFRICOM na hii ni mpya lkn bado hakiko Bara la Afrika makao makuu ya ko Ujerumani mpaka leo hii USA bado hawafahamu au hawajaamua waweke wapi AFRICOM hivyo wameamua kuweka Mji wa Stuttgart, Ujerumani!
 
Rubbish
 
Swala la military base kutokuwepo africa haimaanishi US haina interest kubwa africa. Kuna interest nyingi za kuziadili,kuna interest za kiusalama,kiuchumi na mambo mengine. US imewekeza kiuchumi zaidi Africa kuliko kiusalama wakijua Africa kuna mali za kutosha.
 
Mtoa mada ni kweli 666 kwa muujibu wa Ufunuo 13 na 14 inahusu mamlaka itakayoshiniza ibada ya kumtii mwanadamu #mpinga kristo' dhidi ya Mungu. Marekani itatumika kutekeleza huo mpango, huenda na utawala ujao au mwingine lakini neno la Mungu linasema wazi marekani itahusika 'kuifanya sanamu ya mnyama'.
 


Siyo kweli ndugu, USA imewekeza Afrika yetu kiduchu sana ukilinganisha na Mabara mengine, Afrika yetu siyo priority kwa USA mpaka sasa, ingawaje inakwenda inabadilika na ndiyo maana USA ikaanzisha AFRICOM, lkn bado biashara kati ya USA na Afrika ni ndogo sana kuweza kuwafanya USA waifanye Afrika priority, huwo ndiyo ukweli!
 
kama wamarekani wangetaka kumtoa museveni wangemtoa muda mrefu lakini kutokana na museveni anavyowafurahisha kama kupeleka majeshi somalia hiyokitu sahau kumbuka marekani walijaribu kuingiza majeshi wakapata kipigo cha mbwa mwizi badala yake wamekuwa wakitumia majeshi ya kenya,uganda na washirika wake ili kupambana na al shabab
 
hey ugandans be prepared to handle museveni to trump, the guy may become the president
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…