Dondoo za hatifungani za leo - 20yrs Bond 15.49%

Dondoo za hatifungani za leo - 20yrs Bond 15.49%

Enkulu

Member
Joined
Sep 29, 2022
Posts
20
Reaction score
76
Leo jumatano ya tarehe 31 Julai 2024, ni siku ya mnada wa Hatifungani ya miaka 20 yenye riba ya 15.49% kwa mwaka.

Kwa watakao shinda katika mnada huu watakuwa na dhamana ya miaka 20 kama nilivyosema hapo awali. Dhamana hii itakuja na kuponi mbili kwa mwaka, yaani kila baada ya miezi sita (06)

Ninaposema kuponi namaanisha utalipwa nusu ya riba ndani ya miezi sita na nusu nyengine utalipwa baada ya miezi sita tena ili kukamilisha mwaka.

Hatifungani hii itadumu Kwa muda wa miaka 20 hivyo baada ya miaka 20 utalipwa pesa uliyowekeza (principal amount). Mfano huo hapo kwenye picha
InShot_20240731_073046449.jpg

FAIDA ZA HATIFUNGANI HII

:-Kama zilivyo hatifungani zengine itakupa faida zifuatazo zitakazodumu kwa muda wa miaka 20

📚 Hatifungani ni dhamana (collateral) hivyo una uwezo wa kukopa Benki kupitia hatifungani hii, uwezo wa kukopa utatofautiana kulingana na fedha ulizowekeza.

📚Kuwa na uhakika wa malengo ya muda mrefu. Mfano, ada ya mtoto. Kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu Mtanzania hutumia miaka 17 shuleni. Hivyo unaweza kuwekeza pesa ambayo kuponi zake zitatumika kama ada ya mwanao.

📚 Hatifungani ni uwekezaji wenye hatari ndogo. Hatifungani za serikalli zinasimamiwa na serikalli kupitia Benki kuu ya Tanzania (B.O.T) hivyo uwezekano wa wewe kupata hasara ni mdogo mno.

NOTE: Faida zipo nyingi sana hizo ni baadhi tu, kujifunza mengi kuhusu Hatifungani, karibu uwanja wa email @geminifinaces808@gmail.com

Kila la kheri🙏🇹🇿

Hi
 
Leo jumatano ya tarehe 31 Julai 2024, ni siku ya mnada wa Hatifungani ya miaka 20 yenye riba ya 15.49% kwa mwaka.

Kwa watakao shinda katika mnada huu watakuwa na dhamana ya miaka 20 kama nilivyosema hapo awali. Dhamana hii itakuja na kuponi mbili kwa mwaka, yaani kila baada ya miezi sita (06)

Ninaposema kuponi namaanisha utalipwa nusu ya riba ndani ya miezi sita na nusu nyengine utalipwa baada ya miezi sita tena ili kukamilisha mwaka.

Hatifungani hii itadumu Kwa muda wa miaka 20 hivyo baada ya miaka 20 utalipwa pesa uliyowekeza (principal amount). Mfano huo hapo kwenye picha
View attachment 3057276

FAIDA ZA HATIFUNGANI HII

:-Kama zilivyo hatifungani zengine itakupa faida zifuatazo zitakazodumu kwa muda wa miaka 20

[emoji432] Hatifungani ni dhamana (collateral) hivyo una uwezo wa kukopa Benki kupitia hatifungani hii, uwezo wa kukopa utatofautiana kulingana na fedha ulizowekeza.

[emoji432]Kuwa na uhakika wa malengo ya muda mrefu. Mfano, ada ya mtoto. Kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu Mtanzania hutumia miaka 17 shuleni. Hivyo unaweza kuwekeza pesa ambayo kuponi zake zitatumika kama ada ya mwanao.

[emoji432] Hatifungani ni uwekezaji wenye hatari ndogo. Hatifungani za serikalli zinasimamiwa na serikalli kupitia Benki kuu ya Tanzania (B.O.T) hivyo uwezekano wa wewe kupata hasara ni mdogo mno.

NOTE: Faida zipo nyingi sana hizo ni baadhi tu, kujifunza mengi kuhusu Hatifungani, karibu uwanja wa email @geminifinaces808@gmail.com

Kila la kheri[emoji120][emoji1241]

Hi
Kwahilo ukiweka pembeni masuala ya kukopa manaake ni kiweka 100m na pata 115m baada ya miaka 20, yani kama nina 40yrs kwasasa napata hiyo pesa nikiwa 60yrs......
Hapo tatiizo kubwa ni inflation rate ya Tz shilling, inaweza ikawa kubwa ndani ya miaka 20 kuliko intrest rate hiyo ya 15%
 
Kwahilo ukiweka pembeni masuala ya kukopa manaake ni kiweka 100m na pata 115m baada ya miaka 20, yani kama nina 40yrs kwasasa napata hiyo pesa nikiwa 60yrs......
Hapo tatiizo kubwa ni inflation rste ya Tz shilling inaweza ikawa kubwa nfani ya miaka 20 kuliko intrest rate hiyo ya 7.5%
Mkuu,Umechanganya Vitu Vingi SANA.Bond za Serikali na RIBA yake haikokotolewi hivyo.Angalia kwenye hilo Jedwali happo kweny Milioni 100 kila mwaka utalipwa milioni 15.Kisha Baada ya mika 20 Utarudishiwa Milioni zako 100 ingawa sasa hiyo Rate ya Asilimia 15 inanitisha sana Labda Mleta Uzi afafanue zaidi.
 
Mungekua flexible tuweke hizo hatifungani kwa US dollor na tulipwe kwa dollor baada ya miaka 20, apo ningeuza my assets ili ni wekeze ila kwa Tz shilling hixi karatasi zinazo shuka kwa kasi, mtu moja anamiliki 7nb shilling nyumbani kwake, ziko pesa zote ziko nje ya mfumo rasimi hyper inflation haikwepeki.......boresheni au mueweke kwenye Gold standarnd.
 
Mkuu,Umechanganya Vitu Vingi SANA.Bond za Serikali na RIBA yake haikokotolewi hivyo.Angalia kwenye hilo Jedwali happo kweny Milioni 100 kila mwaka utalipwa milioni 15.Kisha Baada ya mika 20 Utarudishiwa Milioni zako 100 ingawa sasa hiyo Rate ya Asilimia 15 inanitisha sana Labda Mleta Uzi afafanue zaidi.
Kuna kuponi ya kwanza na kuponi ya pili manaake hiyo 15% imegawanywa mala mbili, manaake huenda unalipwa kila baada ya 10yrs ila sioni kila mwaka hapo kwenye jadweli.
 
Tenure5 Years7 Years10 Years15 Years20 Years25 Years
Coupon Rate(%)9.189.4811.4413.515.4915.95
Weighted Average Price(WAP)93.136898.8503101.387793.1934104.2543106.0636
Amount at Maturity(Face Value)107,368,945.47101,163,071.8498,631,293.54107,303,736.19,591,930.594,283,052.81
Investment Amount(Cost Value)100,000,000100,000,000100,000,000100,000,00010,000,000100,000,000
Capital Gain (Face Value - Cost Value)7,368,945.471,163,071.84-1,368,706.467,303,736.1-408,069.5-5,716,947.19
Yearly Coupon9,856,469.199,590,259.2111,283,419.9814,486,004.371,485,790.0315,038,146.92
Total Coupon Amount49,282,345.9767,131,814.47112,834,199.81217,290,065.6129,715,800.69375,953,673.08
Total Coupon Amount After Withholding Tax49,282,345.9767,131,814.47112,834,199.81217,290,065.6129,715,800.69375,953,673.08
Total Gain (Tal Coupon + Capital Gain)56,651,291.4368,294,886.31111,465,493.35224,593,801.7129,307,731.19370,236,725.89
 
Naomba kuuliza,let's say nimewekeza hiyo 100m,je endapo nitaitumia bond hiii kama collateral kwenye benki,watanikopesha asilimia ngapi kwenye huo uwekezaji wangu,na je,hesabu inapigwa kwenye hiyo face value ya bond au ni kwenye kiasi nilichowekeza pamoja na faida jumla nitakazozipata kutokana na coupons zote ndani ya hiyo miaka 20?
 
Mkuu,Umechanganya Vitu Vingi SANA.Bond za Serikali na RIBA yake haikokotolewi hivyo.Angalia kwenye hilo Jedwali happo kweny Milioni 100 kila mwaka utalipwa milioni 15.Kisha Baada ya mika 20 Utarudishiwa Milioni zako 100 ingawa sasa hiyo Rate ya Asilimia 15 inanitisha sana Labda Mleta Uzi afafanue zaidi.
Milioni 15 kwa mwaka zidisha kwa 20 jibu ni milioni 300 duuh mbona faida nene
 
Naomba kuuliza,let's say nimewekeza hiyo 100m,je endapo nitaitumia bond hiii kama collateral kwenye benki,watanikopesha asilimia ngapi kwenye huo uwekezaji wangu,na je,hesabu inapigwa kwenye hiyo face value ya bond au ni kwenye kiasi nilichowekeza pamoja na faida jumla nitakazozipata kutokana na coupons zote ndani ya hiyo miaka 20?
Nilivo elewa ni kwamba mfano nimewekeza 20M hatifungani kwa mwaka napata faida 3098000 hii ina maana kwamba ni sawa na 258166.66 kwa mwezi
Ninaweza kwenda bank mfano crdb bank nikachukua mkopo wa 15M,labda marejesho ni 250000 monthly,naweza ongea na bank niwe nalipa kwa mwaka yaani kuponi kama alivoeleza mtoa mada,ile kuponi ninayopokea inakatwa kulipa mkopo wangu hivyo baada ya miaka 7 ntakuwa nimemaliza mkopo na mtaji wangu bado upo pale pale hii ndo faida ya kuwekeza kwenye hatifungani,unatumia faida unayopokea kulipa deni la mkopo

Faida nyingine kama sitoi hiyo koponi basi baada ya miaka 20 ntakuwa na faida ya jumla (3098000 ×20= 61,960,000) hii ni faida tu
Mtaji 20M + faida 61960000= jumla 81,960,000/= ni sawa na mafao ya mtumishi
Kama ndivyo ni uwekezaji mzuri sana

Nadhani mtoa mada atatuelewesha zaidi
 
Asante Kwa ufafanuzi...Mimi nilidhani kuwa labda tuseme Kwa mfano huu wa 20m ulioyotoa...nikienda benk kuchukua mkopo kupitia hii Bond kama collateral...pale %ya kiasi ninachoweza kukopa watapigia Kwa hiyo 20m+faida(total coupons),ambapo huo mkopo utakuwa unaji -offset wenyewe kutokana na hayo malipo..
 
Enkulu sasa kwa mfano mtu nataka kununua hizo hati fungani, kuna private firms (brokers) zinatumika au naweza nunua mwenyewe direct BOT ??
Zipo mkuu, Moja wapo broker ni zan security unaweza ukawatafuta wapo fresh walinisaidia sana miaka mitano iliyopita kununua bond.
 
Back
Top Bottom