Munambefu
JF-Expert Member
- Jun 24, 2012
- 2,811
- 7,200
Kuna kitu watu wengi hamuangalii na ndio mnapigwa hapo.Nilivo elewa ni kwamba mfano nimewekeza 20M hatifungani kwa mwaka napata faida 3098000 hii ina maana kwamba ni sawa na 258166.66 kwa mwezi
Ninaweza kwenda bank mfano crdb bank nikachukua mkopo wa 15M,labda marejesho ni 250000 monthly,naweza ongea na bank niwe nalipa kwa mwaka yaani kuponi kama alivoeleza mtoa mada,ile kuponi ninayopokea inakatwa kulipa mkopo wangu hivyo baada ya miaka 7 ntakuwa nimemaliza mkopo na mtaji wangu bado upo pale pale hii ndo faida ya kuwekeza kwenye hatifungani,unatumia faida unayopokea kulipa deni la mkopo
Faida nyingine kama sitoi hiyo koponi basi baada ya miaka 20 ntakuwa na faida ya jumla (3098000 ×20= 61,960,000) hii ni faida tu
Mtaji 20M + faida 61960000= jumla 81,960,000/= ni sawa na mafao ya mtumishi
Kama ndivyo ni uwekezaji mzuri sana
Nadhani mtoa mada atatuelewesha zaidi
Hiyo fedha unayowekeza baada ya miaka miwili itakua imeshuka thamani kiasi gani kutokana na mfumuko wa bei?
Ingekuwa tanaruhusiwa kuweka kwa stable currency kama USD matajiri wasingefanya tena biashara zaidi ya kununua hati fungani.
Mwaka jana nilikuwa na mradi wa nyumba za kupanga ulinigharimu kama 140m pamoja na kiwanja.
Mshikaji mmoja katika story akaniambia nimefeli bora ningewekeza katika hati fungani ningepiga hela ndefu bila usumbufu.
Nikamuuliza baada ya miaka kumi ile M140 kwenye hati fungani itakuwa na thamani ya kununua hata kiwanja chenye thamani ya M20 leo?
Na hizi nyumba baada ya miaka hiyo 10 zitakuwa na thamani ile ile ya 140m?