Dondoo za hatifungani za leo - 20yrs Bond 15.49%

Kuna kitu watu wengi hamuangalii na ndio mnapigwa hapo.
Hiyo fedha unayowekeza baada ya miaka miwili itakua imeshuka thamani kiasi gani kutokana na mfumuko wa bei?
Ingekuwa tanaruhusiwa kuweka kwa stable currency kama USD matajiri wasingefanya tena biashara zaidi ya kununua hati fungani.

Mwaka jana nilikuwa na mradi wa nyumba za kupanga ulinigharimu kama 140m pamoja na kiwanja.
Mshikaji mmoja katika story akaniambia nimefeli bora ningewekeza katika hati fungani ningepiga hela ndefu bila usumbufu.
Nikamuuliza baada ya miaka kumi ile M140 kwenye hati fungani itakuwa na thamani ya kununua hata kiwanja chenye thamani ya M20 leo?
Na hizi nyumba baada ya miaka hiyo 10 zitakuwa na thamani ile ile ya 140m?
 
💯
 
Watanzania wengi hawana financial literacy, hususani kwenye finance market, inflation rate yetu haikuruhusu kufaidi hiyo pesa, kabisa ni kupoteza mda nikupe mfano 2004, 1US $ = 900 up to 970 Tanzanian shilling miaka 20 kwa sasa 2024 1US$ =2400 up to 2600,.....kama uliwekeza 100m miaka 20 iliopita sasa hivi wakukurudishia hiyo pesa haina value tena, kama ni dollor unapata $45,000 kwa sasa lakini miaka 20 ilio pita hiyo pesa ungepata $110 000. Hapo kuna faida kweli hapana..........

Kama unataka kufaidi finance market neenda UK au US kanunue hizo bonds wana wapa hata foreiners fursa hiyo ya kununua, wekeza dollor $50,000, rudi Tanzania kalale hutakuja kufa masikini maishani yako, utakua unakula tu exchange rate tu ya unstable currency yetu inao panda kila ukicha, kwa mwezi huwezi kukosa 10 to 15m, na pesa inawekwa tu kwenye your local account hamna haja ya kupigia customer care.
 
Kuna kuponi ya kwanza na kuponi ya pili manaake hiyo 15% imegawanywa mala mbili, manaake huenda unalipwa kila baada ya 10yrs ila sioni kila mwaka hapo kwenye jadweli.
Kuna vitu nikisoma huku una nakataa kabisa jf sio home of great thinkers

Mkuu kabla ya hii post, hukuwahi kujua chochote kuhusu government bonds? Tufanye hukujua, lakini mbona post imeeleza vizuri tena kwa urahisi sana
Sasa umeshindwa vipi kuelewa na hapo wameweka mchanganuo vizuri kabisa hadi mfano wa pesa utayoweka na utavyolipwa kila baada ya miezi 6
 
Mkuu sio dollor ni dollar
 
Hii rate ya 15.47% imepanda lini? Mwaka 2022 mwanzoni ilishushwa sana na kuwa 12%. Je imepandishwa Tena? Na imepanda lini?

Huwa kuna vitu naulizaga lakinj kwenye majinu watu huingia mitini, vinawekwa Ila majibu yanakua hakuna. Ni either mtu anakua hajui hiko kitu au anajua lakini hawezi kutoa maelezo yaliyonyooka, au na yeye kasikia tu sehemu
 
Capital gain na Interest zinakatwa kodi ya zuio (Withholding Tax)
Du. Kwa hiyo hayo malipo mwanzisha thread aliyoweka ya mara mbili kwa mwaka bado yanapigwa tena panga la kodi. Unaweza kutupa mfano wa kiwango cha kodi kama unafahamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…