Dondoo za hatifungani za leo - 20yrs Bond 15.49%

Mkuu hizi hesabu haziko sahihi depending na t-bonds ambazo umezungumzia,sababu hujaconsider vitu kama face value,bidding price,yearly coupon,etc ambazo mwisho wa siku zitatupa total gain.
 
Kama ni kweli interest rate ni above 15% annually basi ni uwekezaji mzuri at least unapunguza hatari ya kupoteza mtaji wako.
 
Kama ni kweli interest rate ni above 15% annually basi ni uwekezaji mzuri at least unapunguza hatari ya kupoteza mtaji wako.
Inategemea tu malengo yako. Mimi nimeweka mzigo wa 20m kwa ajili ya dogo wa 10yrs kama ada nikiwa sipo kazini. Sasa hapo kipi bora, ifanye biashara ipotee yote au ipoe BOT baada ya 10 years achukue plus 15% interest?
 
Mkuu nadhani na wao siyo wajinga. Wanajua kwamba currency yetu siyo stable. Ndo maana wanatoa % kubwa ya returns. Bond za US na nchi nyingine zilizoendelea, sidhani kama interest inazidi 2%. au 3%. Wakati kwetu ni 15%+.

Kwa mtu asiye na uchumi mkubwa, au mwenye matamanio ya biashara, hati fungani ni investment nzuri sana. After all, kibongo kibongo, kipato cha mwajiriwa hakijawahi kuendana na inflation.

Ukiwa na bonds, hata ukitangulia mbele ya haki, una matumaini kwamba madogo hawatakosa karo na matumizi mengine ya kila siku.
 
Inategemea tu malengo yako. Mimi nimeweka mzigo wa 20m kwa ajili ya dogo wa 10yrs kama ada nikiwa sipo kazini. Sasa hapo kipi bora, ifanye biashara ipotee yote au ipoe BOT baada ya 10 years achukue plus 15% interest?
Umefanya powa sana.
 
Mkuu Covax , tupe tips na elimu zaidi kuhusu Bonds za US na UK for foreigners.

Financial literacy ni muhimu sana kwa maisha ya sasa.

Cc: Masanja

-Kaveli-
 
Milioni 15 kwa mwaka zidisha kwa 20 jibu ni milioni 300 duuh mbona faida nene
Hapa nipo wanapofactor in infation.Ina maana kwamba baada ya miaka 20 milioni mia 300 inaweza kuwa sawa na milioni 100 ya sasa.Yaani kituna unachonunu kwa 1000 sasa hivi kitauzwa 3000.Unachonunua kwa 10,000 kitauzwa 30,000...
 
Mkuu Covax , tupe tips na elimu zaidi kuhusu Bonds za US na UK for foreigners.

Financial literacy ni muhimu sana kwa maisha ya sasa.

Cc: Masanja

-Kaveli-
Kama una pesa wewe nunua bonds tuu. Hati fungani ni kama insurance. Ni rahisi kushauriwa kwamba uweke pesa kwenye biashara. Ila biashara pia ni kamari. Mifumo yetu ya kibongo ni wizi wizi tuu. Ukiwa na million 100, Million 50 weka Bond na 50M weka kwenye biashara. Usiweke mayai yote kwenye kikapu kimoja.

Naona siku hizi pia kuna uwezekano wa kununua bonds kwenye nchi za SADC. KIKUBWA JIONGEZE. Angalia nchi yenye uchumi imara kama Botswana au Namibia au SA. Nunua huko.

Kwa maisha yetu ya kibongo kibongo, ukiwategemea akina Mwigulu ambao na wenyewe wanapambana kujikomboa kwa jasho la walalahoi..ni ngumu kuchomoka.
 
Mim naungana na wewe mkuu, ni bora sana narudia tena ni hora sana milioni 100 kuiwekeza kwenye nyumba ya kupangisha ambayo inaweza kukupa hiyo milioni 15 kwa mwaka na bado unaweza kutumia hiyo nyumba kama collateral kuomba mkopo na ukaweza kujenga nyumba nyingine ambapo ukiwa na mahesabu mazuri ndani ya miaka 10 huwez kukusa nyumba walau 3. Nyumba inapanda thamani kila kukicha ila shilingi yetu inaporomoka sana thamani yake kila siku
 
Hapa nipo wanapofactor in infation.Ina maana kwamba baada ya miaka 20 milioni mia 300 inaweza kuwa sawa na milioni 100 ya sasa.Yaani kituna unachonunu kwa 1000 sasa hivi kitauzwa 3000.Unachonunua kwa 10,000 kitauzwa 30,000...
Ni kweli kabisa ila wengi hawaliangalie mwaka 2004 tulikua tunapanda daladala kutoka ubugo mpaka kkoo kwa sh 150, mwaka 2024 ubungo mpaka kkoo ni sh 600, manaake sh 150 ya 2004 ni sawa sawa na sh 600 ya leo ni mara 4 yake, hiyo ndo inaoitya hyper inflation.
 
Umefanya vyema mkuu baada ya miaka 10,mtaji pamoja na faida utakuwa na 50m+
Hii elimu wengi wetu hatuna ndio maana tunaangaika
Inategemea tu malengo yako. Mimi nimeweka mzigo wa 20m kwa ajili ya dogo wa 10yrs kama ada nikiwa sipo kazini. Sasa hapo kipi bora, ifanye biashara ipotee yote au ipoe BOT baada ya 10 years achukue plus 15% interest?
 
Lakini mkuu ata kwenye bond pesa inaongezeka hiyo 15% inaifanya pesa yako uliyoiweka isiwe ile ile ya mwaka 2004 itakuwa ni kubwa leo 2024
Watu mnaongea mambl mengi as if haizai
Kuweka kwenye bond ni tofauti na kusave bank
 
And people think like…..life is static. Hapana. Hali yetu 2004 na leo ni tofauti sana.
 
Tuwekeze kwa gold value Wala sio hata iyo dollar yako pia huwa inashuka ingawa sio Kama tzs Ila bucks ,fiber ,lira,Aussie,loonie and kiwi zinashuka pia
 
Tuwekeze kwa gold value Wala sio hata iyo dollar yako pia huwa inashuka ingawa sio Kama tzs Ila bucks ,fiber ,lira,Aussie,loonie and kiwi zinashuka pia
Mbona hata dhahabu inashuka pia, wewe umeshindwa kujua inflation na depreciation vyote vinamanisha kushuka ila havifanani, pesa ya bongo ina hyper infñation sio kushuka kwa kawaida depreciation.....dollar in depreciate sio ku-inflate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…