Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644

1 Tim 4:12 SUV​

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Lk 2:52 SUV​

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Efe 6:11-18 SUV​

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.

Mit 8:17 SUV​

Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
=======================
Haya wana wa Mungu twendeni kazi
👇🏻👇🏻👇🏻
 
1 Tim 4:12 SUV​

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Lk 2:52 SUV​

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Haya wana wa Mungu twendeni kazi
👇🏻👇🏻👇🏻
Ee Bwana,usikie kuomba kwangu,Kilio changu kikufikie.
 
YOSHUA MWANA WA SIRA 22​

1Mvivu hufanana na jiwe litiwalo mavi,
Kila mtu atamfyonya katika aibu yake.
2Mvivu hufanana na uchafu wa jaani,
Kila augusaye atakung'uta mkono.

3Ni aibu ya baba kuzaa mwana aliye juha,
Na binti asiye na akili ni hasara yake.
4Binti mwenye busara ni tunu kwa mumewe;
Bali aletaye aibu ni huzuni ya mzazi wake.
5Aliye mtundu huwaaibisha baba na mume,
Naye atadharauliwa na wote wawili.
 
Yona 4:3-5
[3]Basi, sasa, Ee BWANA, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.

[4]Naye BWANA akasema, Je! Unatenda vema kukasirika?

[5]Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule utakuwaje.

Huyu Mwamba alikua anamkoromea Sir God eti......kisa aliambiwa jamaa wataangamizwa na Sir God hakufanya hivyo!
 
Methali 28:1-25 BHN​

Waovu hukimbia japo hawafukuzwi na mtu, lakini waadilifu ni hodari kama simba. Taifa la fujo huzusha viongozi wengi, lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini, amefanana na mvua kubwa inayoharibu mimea. Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu, lakini wanaoishika sheria hupingana nao. Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa. Afadhali maskini aishiye kwa unyofu, kuliko tajiri aishiye kwa upotovu. Mtoto ashikaye sheria ni mwenye hekima, lakini rafiki wa walafi humwaibisha baba yake. Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini.
 
1 Tim 4:12 SUV​

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Lk 2:52 SUV​

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Efe 6:11-18​

Efe 6:11-18 SUV​

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote?

Haya wana wa Mungu twendeni kazi
👇🏻👇🏻👇🏻
Uwatakase kwa ile kweli,•neno lako ndiyo kweli(Yohana 17:17).
 
Hagai 1:5-6 (KJV) Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.
 
Yona 4:3-5
[3]Basi, sasa, Ee BWANA, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.

[4]Naye BWANA akasema, Je! Unatenda vema kukasirika?

[5]Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule utakuwaje.

Huyu Mwamba alikua anamkoromea Sir God eti......kisa aliambiwa jamaa wataangamizwa na Sir God hakufanya hivyo!
Kisa cha yona kukataa kwenda Ninawi 🤣🤣 ile neema ya Mungu ilikuwa juu ya Ninawi
 
1 Tim 4:12 SUV​

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Lk 2:52 SUV​

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Efe 6:11-18​

Efe 6:11-18 SUV​

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote?

Haya wana wa Mungu twendeni kazi
👇🏻👇🏻👇🏻

Waebrania4:9​

Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
 
Back
Top Bottom