Dongo lililojificha kwenda kwa wanaojiita Simba

Dongo lililojificha kwenda kwa wanaojiita Simba

Wanamuziki wetu wengi wana Talanta, lakini wanakosa kitu muhimu sana kinaitwa strategies.. Kwasasa industry nzima imekariri kuwa ukitaka kiki basi uwadiss WCB.. Ni kweli utaongelewa ila ni poor strategy

First time nimesikia huu wimbo nilisikia huo mstari na nikajua tu nini kinatafutwa na nikasikitishwa sana na darasa..

Nitoe mfano; hakuna shabiki ambaye anashabikia msanii mmoja pekee.. Kwa mfano mimi shabiki mkubwa wa muziki wa WCB lakini pia ni shabiki wa Darasa toka enzi zile..

Sasa; muziki ni hisia na huwezi kupenda mziki wa mtu ambaye roho yako haina amani naye! Sasa inapotokea msanii akafanya upuuzi wa kuanzisha chokochoko na msanii mwingine unayemshabikia lazima hisia zako kama mshabiki zitachagua side.. Ndio kusema kwa mfano kwa ishu hii shabiki The Bold lazima ushabiki wake kwa darasa utapungua na kubakia kuwa shabiki wa WCB! Sasa darasa ajiulize anapoteza mashabiki wangapi kwa mtindo huu..

Nitoe mfano mwingine; juzi kati fiesta ilivyokuja Moro nikapata 'shavu' fulani hivi katika maandalizi yake and kwa wiki nzima ile nikajikuta nasikiliza sana clouds fm tofauti na kawaida yangu.. Nakumbuka kuna siku Darasa alikuwa anahojiwa na Diva, akaulizwa unazungumziaje mziki wa singeli na man fongo? Akajibu simjui man fongo... Diva na mbwembwe zake zile akahamaki "ooooohh my gooorsh kwahiyo hujawahi kusikia Hainaga ushemeji?? Unasikikizaga nini sasa kwenye redio??" Akajibu sisikilizi mziki wowote zaidi ya mziki wangu..!!!!

Doooohh nikasema ndugu yetu sifa zishamzidi, nayeye anajiona 'tembo' sasa..
Ila nikapotezea mpaka sasa ndio nakumbuka yale majibu yake yanareflect vipi personality yake ya sasa..

Ninachojaribu kusema ni nini??
Kuna kitabu mashuhuri sana cha Jemedari wa kivita Bwana Sun Tzu (ART OF WAR) na kuna kanuni moja anazungumzia kuwa "dont fight unnecessary wars".. Vita yoyote ina gharama! Kwahiyo kabla ujaanzisha/ujaingia kwenye vita yoyote kwanza fanya tathimini faida na hasara ya vita hiyo.. Je gharama utakayoitumia kupigana vita hiyo inaendana na manufaa utakayoyapata???

Sasa wabongofleva wao wanajua kuanzisha vita tu bila kutathimini gharama za vita hizo na faida gani watapata! Wao wamekariri tu "nitapata kiki"

Hiki ndicho kimemgharimu Dimpoz.. Alianzisha vita bila kufanya tathimini,
Yeye alipagawishwa tu "nitapata kiki" bila kujua gharama ya vita anayoianzisha..
Hakujua mashabiki wake wengi ndio hao hao mashabiki wa WCB na ulipofika muda wa kuchagua kuwekeza hisia zao za muziki kati ya dimpoz na WCB asilimia kubwa wakachagua kuwekeza hisia WCB.!!

Hapa ndipo ninaposema wasanii wetu wengi wana talanta lakini hawana Strategies.. Hata wakiweka strategies wanaweka poor strategies.. Ndio maana sijawahi kujutia kuwaunga mkono WCB, wana mikakati mwanana, muziki mwanana, washauri vichwa na hata wakiamua kuanzisha vita, wanaanzisha vita ambayo wana uhakika hawawezi kushindwa..

The Bold.
Wangekuwa wanaanzisha vita wasiyoshindwa mbona kwenye views povu lilitoka balaaa macho kodooo kwa mic hhahaahahha. Wazee wa views
 
Hapo kwenye red ndio nimepapenda zaidi na sidhani kama Darasa na wasanii wengine wanalijua hilo...Mtu anaingia kwenye vita lakini ukimtazama unaona kabisa hana ubavu wala pumzi na hachukui dakika anashindwa..

Mimi pia ni mmoja wa mashabiki wa Darasa napenda sana muziki wake na anavyo imba na mwanzo nilimuona ni mtu asiyependa makuu lakini nilishangaa kusikia wimbo wake huo kujaa majungu kiasi kile lakini nilimkumbuka kuwa ukitaka kuona hasira za mlevi mwaga pombe yake.....Bila shaka ni kweli Darasa maneno yamemtoka baada ya kile anacho kipenda kuguswa...
Najua Darasa nae anajaribu kufanya ya Dimpoz lakini sijui kama kajiandaa kwa matokeo,....
Kwanza mimi Darasa namuonea huruma na nisingependa ajiingize kwenye migogoro na mashabiki wa wasanii fulani fulani maana naamini yeye ana share mashabiki na wasanii fulani fulani.

Nilipo usikia huo wimbo wa Darasa kwakweli akili na kichwa kiliniambia hii ni beat ya wimbo fualni sikujua wimbo gani lakini Mungu si Athumani jumamosi nasikiliza EA radio mida ya saa sita mtangazajia(queen fifi) akasema sikilizeni wimbo huu halafu msiseme kitu...kwakweli ulipigwa wimbo ule beat ni hii hii ya Darasa mpaka melody sasa bahati mbaya siki kariri jina la wimbo.
Bado nikajiuliza huyu aliyecopy beat ndio anarusha vijembe hivi mashabiki wa huyo msanii wakiamua kuanza kuusakama wimbo wake kuwa ni copy kweli ataweza kuhimili vishindo? Nikataka kuanzisha thread kuhoji kuhusu huo wimbo lakini roho ikasema utamuharibia muache tuu..
Bado najiuliza kama wewe ikiwa kweli Darasa kajiandaa kweli kuingia vitani.
Acheni porojo ninyi ni wapi ktk hio nyimbo kamsema mtu mbona hamsemi ametaja mara ngapi 'tunachambua kama karanga' Tz shida majungu sana.
 
Aisee Dimpoz kaharibu kavujisha mchongo wa viewers kila mtu sasa amejua hii siri [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wangekuwa wanaanzisha vita wasiyoshindwa mbona kwenye views povu lilitoka balaaa macho kodooo kwa mic hhahaahahha. Wazee wa views
Hebu tuangalie tofauti ya wanaonunua views na wale wasio nunua;

a) wasio nunua views

- mwengine mpaka sasa anakaa kwa mama (he is on his 30's)
- yuko kwenye mziki zaidi ya miaka 10 na bado analalamika kufanyiwa figisu kama underground
- mwingine mziki umemtupa mpaka imebidi ajenge urafiki na waarabu unaotiliwa mashaka ili tu aweze kumudu maisha ya kistaa mjini.
- wote wanashikiwa akili na wadada wa mjini (mwegelo, sepetu & co)
- wana kila dalili ya msongo wa mawazo




b) wanaonunua views

- wanajitegemea kimaisha kwa maana ya makazi.! Kuanzia ndani na nje ya nchi
- ni 'trend setters'! Wanafanya kitu baadae kila msanii anaiga.
- wana kampuni/lebo yenye valuation ya billions of shillings.
- wanaheshimiwa kila kona ya bara la africa kimuziki.
- kila wanachogusa turns into gold.



Sasa; kuna filamu inaitwa 'wolf of wall street', kuna kipande leonardo de caprio anatoa speech kwa wenzake anawaambia "..there is no nobility into being poor! i have been a poor man and i have been a rich man, and I choose rich every f*cking time.."

Na mimi niseme kwamba, ukinambia nichague kuwa niwe nanunua views au niwe sinunui views, jibu langu "..I choose kununua views every f*cking time.."

The Bold.
 
Mi nafikiri wote mnahangaishwa na hisia ambazo ni tofauti na lengo la mwenye wimbo. Nimesikiliza wimbo huo mara kadhaa, hakuna mstari wowote katika wimbo huo unaobeza kikundi fulani cha watu.

Sikiliza wimbo na kielewe kile kilichotajwa au kumaanishwa na msanii mwenyewe na si kutafuta maana nyingine zisizo kuwa na msingi.
Mkuu ww ndio umeongea point......mm naona darasa hajamlenga mtu yoyote hio ni mistari tu ya hiphop kama mistari mingine so hao wenye team zao watulize mishono
 
Wimbo m'baya,akajipange upya.

Bila kiki ya wasafi huwezi jadiliwa JF Go chibu goooooo

beat na melody ya huu wimbo ni copy ya wimbo fulani....

Nani Kaproduce huu Wimbo?

darasa kasema kweli tupu huwezi kujiita simba huku umetoboa pua

Aisee Dimpoz kaharibu kavujisha mchongo wa viewers kila mtu sasa amejua hii siri [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kwa.kujishtukia tu hamjambo hahahaha wazee wa povu

Itaje hiyo nyimbo bas
Wakuu, hata mimi uhater najua sana sema basi tu sitaki..
Hebu tufanye hivi, nenda kasikilize huu wimbo nimeweka link hapa chini..
Sikiliza beat, sikiliza melody na angalia "plot" ya nyimbo alafu uje hapa unibishie Darasa hajacopy..


Song: Sanko
Artist: Timaya
Producer: Orbeat


 
Back
Top Bottom