Donor Fatigue: Wazungu wametuchoka, sisi tunanunua ma VX!

Donor Fatigue: Wazungu wametuchoka, sisi tunanunua ma VX!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Matusi ya Donald Trump Rais wa Marekani kwa wananchi na viongozi wa Dunia ya Tatu, hasa Afrika, yamekaa mahali pake.

Wenye akili tunaambiwa kwa sauti kubwa: OMBA OMBA YENU TUMEICHOKA!

Hapo ndio tutamkumbuka Mwalimu Nyerere na siasa yake ya kiuchumi ya KUJITEGEMEA.

Watanzania na waafrika, tutatukanwa hadi lini?


Simlaumu TRUMP!
 
download.jpeg

Wito wa Donald Trump kwa watu wa Afrika.

Mungu amebariki nchi zenu kwa rasilimali nyingi, akili, na uwezo mkubwa. Ni wkt wa kuacha kusubiri mabadiliko kutoka nje na kuanza kuwajibisha viongozi wenu wala rushwa. Acheni kukimbilia mataifa ya kigeni na kuzurura mitaani huko mkitafuta fursa ambazo zinapaswa kuwepo nyumbani kwenu.

Kama Wamarekani wangelikubali ukandamizaji na kubaki kimya, hakungekuwepo na Marekani kama unavyoiona leo. Kama Wafaransa wangekaa kimya mwaka 1775, hakungekuwa na Ufaransa ya leo. Mapinduzi yanahitaji hatua, si unyonge.

Kwa nini mnaendelea kucheza siasa za kikabila huku viongozi wenu wakiiba utajiri wa mataifa yenu bila haya?
Kwa nini mnategemea Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa dawa za msaada wkt mna wataalamu wa madawa na tiba katika nchi zenu?
Nchi zenu zimebarikiwa kwa vipaji na maarifa ya kutengeneza suluhisho za ndani.
Dai mifumo bora ya afya. Acheni viongozi wenu wakimbilie nchi za nje kutibiwa huku hospitali zenu nyumbani zikitelekezwa bila hata huduma thabiti ilihali mshajitawala tangu miaka ya 1960's.

Kwa nini viongozi wenu wanapora rasilimali zenu ili kuishi maisha ya anasa huku barabara zenu zikiwa mbovu, shule hazina fedha za kutosha, na umeme haupo wa uhakika?
Je, mnasubiri malaika waje kutatua matatizo haya?
M/Mungu amewapa uwezo wa kuchukua hatua, basi chukueni hatua!
Mataifa yaliyoendelea yamepata mafanikio kupitia uwajibikaji, kazi ngumu, na kujitolea, siyo kwa kusubiri miujiza.

Marekani ni ya Wamarekani. Ufaransa ni ya Wafaransa. Ni wkt wa ninyi kuwajibika kwa nchi zenu. Acheni kukimbilia nchi za kigeni ili kujifungua na kutafuta uraia wa moja kwa moja kwa watoto wenu. Sera hizo zimeondolewa. Rudi nyumbani na mjenge Taifa ambalo mtaweza kujivunia kuzaliwa huko kwenu.

Mapinduzi huanza na watu, kama mmechoka na uongozi mbovu, inukeni. Dai takwimu sahihi za idadi ya watu, uchaguzi wa haki, na mwisho wa wizi na ufisadi. Acheni kuruhusu wanasiasa wala rushwa na viongozi wa kidini kuwapumbaza kwa kusema ukandamizaji ni “mapenzi ya Mungu.”

Kama Wafaransa waliweza kuungana dhidi ya majeshi na watawala wakandamizaji, nanyi mnaweza. Mabadiliko hayatakuja ikiwa mtakaa kimya na kinyonge. Kama mnataka umeme wa uhakika, barabara nzuri, na maisha bora, chukueni hatua. Acheni kukimbilia Marekani, Canada, au Ulaya kwa kile ambacho mnaweza kujijengea nyumbani.

Ujumbe ni rahisi, inukeni, ungana, na mchukue hatima ya maisha yenu mikononi mwenu. Hatima ya Afrika ipo mikononi mwenu. Iwafikie mioyoni na akilini mwenu, ni ninyi pekee mnaoweza kuunda Afrika mnayoitamani!

Copied nPasted.
 
Matusi ya Donald Trump Rais wa Marekani kwa wananchi na viongozi wa Dunia ya Tatu, hasa Afrika, yamekaa mahali pake.

Wenye akili tunaambiwa kwa sauti kubwa: OMBA OMBA YENU TUMEICHOKA!

Hapo ndio tutamkumbuka Mwalimu Nyerere na siasa yake ya kiuchumi ya KUJITEGEMEA. Watanzania na waafrika, tutatukanwa hadi lini?


Simlaumu TRUMP!
Wàafrika isipokuwa wachaaache saana, na watanzania kazi hatutaki ila uchawa,wizi,ufisadi,uvivu,unaaa,umbea,kamari,na kutumaini miujiza ndio fani zetu pendwa ,acha tunyooshwe akili zetu legelege ama mbovu zirudi kwenye mhimili wake a k.a kwenye reli.
 
Aliyechoka ni Trump peke yake
We unapenda misaada ? Utakazwa mzee jifunze kujitegemea yani kabisa unasema aliechoka ni Trump pekeyake, wengine hawajachoka kukupa misaada utawapa dubri au ? Kaaa kitaalam mzee watakupelekea moto man...
 
We unapenda misaada ? Utakazwa mzee jifunze kujitegemea yani kabisa unasema aliechoka ni Trump pekeyake, wengine hawajachoka kukupa misaada utawapa dubri au ? Kaaa kitaalam mzee watakupelekea moto man...
Kwani Wewe unavyokazwa ni misaada wanakupa 🐼
 
Back
Top Bottom