Donor Fatigue: Wazungu wametuchoka, sisi tunanunua ma VX!

Haya ndio maneno yanayotakiwa yaonekane kwenye mabango yaliyosambaa nchi nzima badala ya haya yanayosifia ujinga. Pengine vijana walamba viatu aka machawa wakiyasoma mara kwa mara akili inaweza kuwarudia wakajua wajibu wao kwa nchi yao
Kabisaaaaaa
 
 

Attachments

  • VID-20250128-WA0033.mp4
    3.9 MB
Mwanzo wa utungu kuelekea dhiki kuu. Kila kitu kutakuwa kigumu mbele ya safari kuelekea ule mwisho.
 
Hizi Nchi wao ndiyo waliziharibu walipandikiza vibaraka mpaka basi. Wakaiba na kuvuruga uchumi hadi basi. Viongozi wanamageuzi wakawaua na kuwatenga. Watulipe fidia kwanza.
 
Hizi Nchi wao ndiyo waliziharibu walipandikiza vibaraka mpaka basi. Wakaiba na kuvuruga uchumi hadi basi. Viongozi wanamageuzi wakawaua na kuwatenga. Watulipe fidia kwanza.
Suluhisho ninkupiga kazi na kuwazidi. Kukulipa hawatakulipa, tuwe kana China na tuwazidi akili.
 
Waafrika tumekuwa tunayasema haya kila siku. Kabla hata ya 1884ad

"Hatutaki misaada tunataka kufanya biashara na nyinyi" kama tulivyokuwa tukifanya biashara nyakati za 1400ad.

Our cries fell on deaf ears.

Ila wapo wanaofaidika na status quo, ya Waafrika kuwa wategemezi na hawa ndio hao hao wanaosema 'mjikomboe'.

Wafitni na manduminakuwili

=========
Watakuja wajinga, wapumbavu, mamluki, Internet trolls, Digital blackface trolls, doctrinated bafoons, bigots, racist propagandist, pundits, spinners and what have you, watasema

"Huezi"

Hao hao wanaosema 'oh ...mjitegemee', 'wacheni utegemezi'na mlolongo wa matusi mengi tu.

Ukiwauliza tufanye nini, watakujibu

"Tutawaliwe"
🤔😪🤒
Hakuna neno hopeless kama hilo na mtu analisema kwa kujitutumua unabaki kujiuliza, were you a wanted child? Did your parents refuse to listen to your troubles and triumphs?
Yani nataka niwaulize hawa watu,


What is your Problem Bro?
 
Hatukumuelewa Mwalimu tangu enzo hizo tutamuelewa Trump leo? Mungu ibariki Africa.
 

Ni kweli,sisi waafrica tumejaa zaidi ubinafsi.yaani kiongozi akipata madaraka anajiangalia yeye binafsi namna atakavyojiondoa kwenye umasikini ila siyo nchi.Matumizi ya ofisi ni ya kianasa zaidi. magari mazuri sana ya gharama kubwa sana.misafara exoensive.halafu unaomba msaada.

Hata kama ni wewe kila siku kuna mshikaji anakulilia shida unamsaidia ila kila siku unamuona kwenye ma club makubwa makubwa na wanawake na anakula starehe.ila kesho mkionana anaendelea kukulilia shida.si utampuuza
 
Trump ana akili sn, huwezi kusaidia majitu majinga yamekalia utajiri(madini ya kila aina, mito, bahari, gas, makaa ya mawe, misitu, ardhi nzuri, watu wengi, mifugo, tanzanite, mbunga za wanyama, milima, maziwa, mabwawa kibao n.k) wewe wananchi wako wanalipa kodi kubwa yenyewe wanatumia kodi kwa anasa tupu, ufisadi, utapeli na kuficha fedha za wananchi nje kwenye mabenk badala ya kuleta maendeleo. Safi Trump japo kuwa na mimi nitakipata cha moto lakini acha liwe funzo.
 
Wasio na akili wengine wanataka China na Urusi ndo waanze kutoa hizo pesa as if niwa lipa kodi wa mataifa hayo.

Mwafrika akili yake ni tegemezi ndo maana mataifa yetu yamekuwa ombaomba uko ughaibuni.
Tunaongozwa na majitu majinga haswa ndiyo maana, fedha zipo tatizo ni matumizi makubwa ya anasa na ufisadi
 
Mimi sioni kama ametukana, ila ametuambia ukweli- Ukweli mchungu. Watu wengi huwa hatupendi kuambiwa ukweli unaoumiza nafsi. Lipi jema? Kuambiwa ukweli mchungu utakaokusaidia kujisahihisha/kujirekebisha au uendelee kuishi kwenye maisha ya uongo na unafiki?
 
Wao wamechukua rasilimali zote za Africa wanadhani Wagogo wataishije?
Kuendelea kuishi na fikra kama hizi ni changamoto nyingine ya kukabiliana nayo kwa nguvu zote. Hivi hizo raslimali walichukuwa sisi tukiwa wapi? Ukiangalia kiuhalisia ukiacha kipindi cha ukoloni, raslimali nyingine nyingi wamechukuwa/tumewapa tukiwa mataifa huru. Viongozi wengi wa Kiafrika wanaendelea kugawa raslimali za mataifa yao kwa Wageni hasa Wazungu. Sasa nani wa kulaumiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…