Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani hizi ni assumption zako mkuu,
Ila kumbuka Bandari inayojengwa si ya wachina. Mfano mdogo tu mkuu: Kwani ukitafuta fundi ujenzi akakujengea nyumba unategemea huyo fundi kulala hiyo nyumba au kupanga kwenye hiyo nyumba??
Wanachina wameshinda tender ya kujenga bandari, na siyo lazima meli zao zifunge kwenye hiyo gati. Mbona transhipments zinafanyika tu hata bandari ya Dar??
Hili swala kwa mtazamo wangu limepelekwa kisiasa zaidi, siyo kama lina tija kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Kwanza kina cha maji Bagamoyo hakisupport meli zenye draft kubwa ku-berth, sasa hizo meli kubwa za kichina unazosema zitatumia hiyo bandari ya Bagamoyo zitawezaje kufunga gati?? Cha msingi walipaswa ku-improve Bandari ya dar na kuifanya ya kisasa zaidi. Kuweka miundo mbinu ya barabara na reli mizuri kutoka bandarini. Kuongeza kina cha kwa berths na kuinstall vifaa vya kisasa. Kama umewahi kufika Antwerp port, walichofanya ni kuongeza kina cha maji kuanzia anchorage mpaka kwenye berths zao, meli za draft mpaka 30m zinafunga.
Kwanza kwa takwimu zilizopo meli za kutoka china zinazokuja hapa kwetu hazizidi kumi kwa mwaka.
Political motivated project goes politically not economically!! Like the dar-bagamoyo felly!!. We beg the next president to stop this and upgrade Mtwara and Tanga port!!
Na ndio maana nimezungumzia suala la possibility ya kuwa transshipment port, that's one, but second, usisahau kwamba huu mradi unakuwa financed na China Merchants Holdings (International) Co Ltd, so unless kama unataka kusema Wachina ni wapumbavu kiasi cha kuweza ku-finance multi-billion project just to favor political lust of African Leaders! Hebu tujikumbushe kidogo habari ambayo iliwahi kutolewa na CNN.
Quote nyingine ni hii hapa chini:Sasa hivi Mkuu wangu unataka kuniambia Wachina siku hizi wamekuwa stupid kiasi hicho? Kama wanaowekeza ni Wachina, sasa kama mradi ni wa kisiasa, je unatarajia kum-favor nani? Can Chinese President Xi Jinping's political career shine in his coountry kwa kuwekeza kwenye white elephant project in a foreign country? Nani anayelengwa kunufaika ikiwa ni just for political reason?
Lakini vile vile haya mambo ya kusema kina cha maji pale ni kidogo ni kujaribu ku-abuse utaalamu wa watu! Hivi kweli inawezekana Wachina wakurupuke from nowhere na kutaka ku-invest billions of dollars wakati wanafahamu kwamba kina cha maji hakiwezi ku-support the entire project? Kwa Watanzania inawezekana lakini sio kwa Wachina!
Wewe bwana acha ubishi wa kipuuzi. Gati ya Bandari ya Dar ni nyembaba, kiasi kuwa hat ameli mbili za size ya kati kupishana tu ni mgogoro. kama hujui kitu nyamaza au kubali unapoelekezwa. kujifanya mjuaji wakati unachoandika kinaonesha kinyume na huo ujuaji ni vitu vya ajabu kwa kweli.
Bandari ya Dar umeshaambiwa inakuwa improved and $600M zinatumika, mkopo kutoka benki ya dunia. Nenda kurasini, eneo lote kuanzia kidongo chekundu,mivinjeni hadi baraza la maaskofu limenunuliwa na serikali kwa ajili ya kuongeza capacity.
Bandari yenye ukubwa wa Bagamoyo haitoshi kuijenga sehemu ilipo bandari ya Dar,acha ubishi. Hakuna mtu anayeweza ku-invest $10B dunia ya leo akawa politically motivated kipuuzi puuzi. Greece mwezi wa sita sasa hivi wanabishana na EU kuhusu malipo ya mkopo wa $8B, sasa wewe unaichukulia dollar bilioni 10 kiurahisi rahisi tu. That is some serious investment decision, that only nations as powerful as china can take on at the current global economy. ONLY a huge fool will turn away such an investment for reasons as stupid as it's location.
kwa kweli lawama nyengine ni za kipuuzi na zisizo na economical wala technical backing behind them. yani mtu anakurupuka tu na kuanza kubwawaja. Kuna chizi mwengine alikuwa analaumu morogoro road eneo la kimara kuwa na mitaro mirefu eti magari yatatumbukia,hajui kuwa hiyo mitaro ndio inaepusha mafuriko maeneo hayo, mara ya mwisho kusikia mafuriko kimara ni lini?
asilimia 80 ya bidhaa kariakoo zinatoka china halafu unategemea tuchukulie hizi porojo zako za meli kutoka china hazidi kumi kwa mwaka?are effn serious?
Unaweza kudhani unajua kumbe hujui. Pia kwa mtu mstaarabu huwezi kuchangia hoja kwa kutoa matusi.
Sasa Yawekana hata unachokionge hukijui vizuri. Si dhani kama hata gati unaifahamu. Gati ya DSM port siyo nyembamba, Channel ndiyo nyembamba. Kilichotakiwa kufanywa ni kupanua channel na kufanya dredging kuanzia kisiwa cha Nyakatombe mpaka kwenye wharf. kuweka cranes za kisasa (Gant cranes) na ku-improve infrastructures zingine kama reli na barabara kwa ajili ya hinterland. Tatizo la DSM port ni narrow channel na poor operations kwa kuwa na vifaa vya kizamani. (Crane bado wanatumia za kizamani sana). Ndo maana meli zenye shehena ya nafaka au mbolea zinakaa hata mwezi zikipakua mzigo. Conveyor na hoovers wanazotumia ni za samani sana.
Kubali ukatae pamoja na kufanya investment kubwa huko Bagamoyo bado RoI itachukuwa miaka mingi mno. Kwa hiyo usipende kutoa hoja zako kwa kutukana. Pia angalia uwezo wetu wa ku-export ni mdogo sana. Pia kama unasema tunategemea land-locked countries kama Rwandwa, Burundi, Malawi, Zambia n.k, kumbuka wazambia wameishaanza kutukimbia kutokana na bei zetu kuwa juu. wanatumia Beira port. Wanyarwanda ushirikiano wetu siyo mzuri wanatumia Mombasa. Waganda nao walishahamia mombasa. Amini usiamini hata ikijengwa huko Bagamoyo bado haitakuwa na tija kwa kukuza uchumi wetu.
NB: Mara nyingine uchangie kama mstaarabu siyo kwa lugha za kiuni za kutoa matusi
- Naomba unioneshe tusi moja tu nililoandika wakati nakujibu.
- Unataka wapanue njia hapo Daresalam,hujui hapo kuna mwamba?unadhani hayo magorofa hapo posta yanajengwa kwa ajali au?Hakuna investor anayetaka kupoteza muda kufanya kazi inayomcost muda na pesa, wakati bagamoyo kumekaa idol na anaweza fanya anachohitaji bila bugudha.wewe akili yako inawaza miaka 3-5 mbele, anayetoa $10B anawaza miaka 30-40 mbele, hamuwezi kufanana.
- Unaendelea kurudia habari za maboresho, umeshaambiwa bandari inafanyiwa upgrade kupitia pesa serikali imekopa,sasa ulitaka iweje?
- Anayeamua ajenge wapi sio wewe, mchangiaji wa JF, ni mtu mwenye extra $10B. WHo has money decides where to put his money. Mfano mdogo, ukitaka kujenga nyumba humuomba dalali akuamulie wapi unajenga hiyo nyumba, au unachagua wewe panapokupendeza kwa kufuatisha vigezo ulivyoweka wewe mjenzi?
- ROI haikuhusu, pesa sio za kwako.wewe vipi?yani mie nije kununua shamba kwako halafu kiherehere cha ROI kiwe kwako na sio kwangu, wapi na wapi?Pesa za wachina ROI ya kwao, wamepewa muda wa kurudisha pesa zao, kazi kwao kuzirudisha kwenye huo muda. vilivyobaki ni jukumu lao sio la kwetu.
- Bagamoyo port prcinciple function sio ku-serve vijinchi viduchu kama Burundi na Rwanda wewe acha kuchanaganya mambo.,unajua 20M TEU ni kiasi gani cha cargo?bandari ya Dar +Mombasa+ Tanga+ Mtwara +Lamu kwa mwaka hawavuki hata 5M TEU, inamaanisha kuwa soko la hii bandari sio hizi nchi peke yake.Mbona huelewi.Go read about kazi ya transhipment ports. NDIO maana Singapore wana bandari kubwa duniani wakati nchi yao hata Dar KUBWA.think BIG
una hoja sana kuhusu huu ujenzi, personally nataman huo ujenzi uanze huko Bagamoyo mwezi wa saba kwa kuwa nina plots zangu na ntakuwa mdada wa mjini sana.Nina viwanja Kiromo na Zinga.Mlingotini hayatakuwepo makazi ya ura
ia so kama viwanja nawashauri muwahi Zinga na Kiromo.Usinunue mapinga utakuwa mbali na bandari ingawa panaonekana kuchangamka
NB:bitte, bitte TUMIA LUGHA LAINI KUELEZA HOJA ZAKO, una lugha kavu jambo linalotafsirika matusi na mchangiaji aliyetangulia.Kein probleme
una hoja sana kuhusu huu ujenzi, personally nataman huo ujenzi uanze huko Bagamoyo mwezi wa saba kwa kuwa nina plots zangu na ntakuwa mdada wa mjini sana.Nina viwanja Kiromo na Zinga.Mlingotini hayatakuwepo makazi ya raia so kama viwanja nawashauri muwahi Zinga na Kiromo.Usinunue mapinga utakuwa mbali na bandari ingawa panaonekana kuchangamka
NB:bitte, bitte TUMIA LUGHA LAINI KUELEZA HOJA ZAKO, una lugha kavu jambo linalotafsirika matusi na mchangiaji aliyetangulia.Kein probleme
Meli nyingi zinazo call Dar port kwa mwaka hazifiki kumi kwa mwaka. (Ukitaka kusibitisha Nenda SINOTA shipping Agent) watakupa takwimu ya number za meli za Kichina zinazo funga kwenye Bandari ya DAR. (SINOTA ndiye agent wa Meli zote za Kichina zinazokuja DAR).