Doto Magari ana hoja kuhusu Wasomi, asikilizwe!

Doto Magari ana hoja kuhusu Wasomi, asikilizwe!

Usiwalaumu sana hao maana hali yao ya uchumi ni duni ndio maana wako radhi kununuliwa .
Msomi anatakiwa:-

Ama.

1. Kujali mambo ya uchumi na kubadilisha hali yake ya uchumi kwa njia zilizo ndani ya maadili ya kisomi. Atachapisha vitabu, atafundisha, atafanya gunduzi na kupata patents, atajua jinsi ya kujikimu kiuchumi bila kuharibu maadiki ya kisomi.

Ama.

2. Kukubali kuwa hawezi kufanya makubwa anavyotaka kiuchumi, lakini atakuwa hana tatizo kuishi ndani ya maadili ya kisomi, hata pale ambapo mambo ya uchumi hayatakuwa mazuri sana.

Hao niliowataja wameshindwa yote mawili.
 
Umasikini ni LAANA.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Umaskini sio wa pesa tu pia wa elimu
Kutokuwa na elimu pia ni laana
Binadamu anatakiwa kubalance elimu awe nayo pia

Mtu haheshimiwi tu sababu ana pesa tu
Ndio maana traffic polisi pesa hana lakini ukipita na gari yako ya mabilioni akinyoodha tu kamkono kuwa usimame huna ujanja na pesa zako lazima ushike adabu yako na uheshimu traffic na kusimama utake usitake
Jeuri ya pesa inakuwa haina nafasi
 
Sawa,hatukatai kwamba yeye katoboa bila kwenda shule,lakini pia aangalie ni asilimia ngapi ya watu ambao hawakuenda shule na hawajatoboa maisha pia!?
Bila watu kwenda shule hata hizo gari anazozifanyia udalali zisingeundwa!!Kwa kifupi hatutakiwi kudharauliana na hapa duniani tunategemeana!
 
Kama umesoma inabidi unyang'anywe vyeti kwasababu unayumbishwa na watu wajinga na hujiamini. Mengi alikuwa kilaza? Halafu milioni 50 unaichukuliaje ndugu? Ingekuwa Mwijaku analipwa 50m kwa wiki 2 ingeonekana tu kupitia matendo yake. Hela ni kama ushuzi.. haifichiki kirahisi.

Nimesema ukiona msomi tajiri basi ujue kakwiba mpunga kwa kutumia peni....Mengi alikuwa Tajiri lakini behind the scene inajulikana source ya utajiri wake.

Mwijaku amesoma lakini vyeti amevipiga kibiriti ,Pesa ameipata kwa kujichetua.
 
Hizo fikra potofu achana nazo mkuu. Sasa hivi vijana wadogo toka chuo kikuu chini ya miaka 25 wanakimbiza na kupiga hela hatari. Nimeona vijana wadogo sana pale Tunduma wana hela kama zote.
 
Hizo fikra potofu achana nazo mkuu. Sasa hivi vijana wadogo toka chuo kikuu chini ya miaka 25 wanakimbiza na kupiga hela hatari. Nimeona vijana wadogo sana pale Tunduma wana hela kama zote.

Kwa nje utaona wanapiga pesa lakini wenyewe wanajua hali halisi...Usione ukadhani.
 
A). Mfanyabiasha Maarufu wa Magari nchini Ndugu Dotto Magari ameonekana kwenye mitandao akizungumzia namna Wasomi nchini wasivyojitambua Wala kutumia usomi wao kuongeza kipato. Na kutishia kwenye dimbwi la umaskini akifanikiwa Sana ananunua Hari ya IST Tena Kwa mikopo wa benki.

B). Namnukuu "wasomi mmesomea Njaa" jaman lolote.

C). Mheshimiwa Dotto ana hoja ya msingi kuhusu kubweteka Kwa Wasomi wetu. Asikilizwe, ana hoja.

NB: Wasomi msikilizeni Kwa makini, msitumie mihemko kumjibu. Bali jibuni hoja kwa hoja. Msimtukane Wala kumbughudhi hapo ndo kipimo cha usiku wenu kitaonekana.

Tz kila kitu kinawezekana...mhuni kuitwa mheshimiwa n.k
 
Kwa hiyo unataka kusema vinatofauti??
Elimu unafundishwa direct na Mtu fulani mfano mzuri ni hii Tunayofundishwa darasani..

Akili unaikuza mwenyewe kulingana na Lifestyle unayoishi kama vile Malezi, Changamoto za maisha, Watu waliokuzunguka..

Kuna watu hawana Elimu ila wana Akili yaani kwa lugha nyingine ukitoa yale yote uliyowahi kufundishwa iwe darasani au lah.. Utachobakiwa nacho ndio kinaitwa AKILI ...
 
hapo alipo anaongozwa na wasomi kama ana aamini akiri yake pekee ajaribu kuajiri watu wenye elimu kama yake mwinzo mwisho alafu baada ya mwezi 1 tutapata majibu
 
Kwanini wengine wasionekane?

Kwani Matajiri wote Tanzania wasiosoma unawajua? Matajiri wote wa migodini unawajua? Ukimuacha Supa Feo aliyetitangaza juzi ,Kishimba ,Musukuma ambao ni darasa la 7 ,wengine matajiri wasiosoma unawajua? Kutokuwaona wewe ndiyo hawapo?
 
Usipeleke watoto wako shule ili wawe matajiri kama Kishimba.
 
Back
Top Bottom