Dotto Biteko anashauriwa na kina nani?

Kama wanafanya hivi kweli basi washughulikiwe haraka
 
Sidhani kama ni ishu kubwa kama unavyosema, hii anaweza hata akafanya mwenyewe kwenye simu au kompyuta yake! Au hata akinitumia debit number yake naweza kumtengenezea na kumtumia. Na mimi sifanyi kazi TRA.
 
Ila kanda ya ziwa hiyo tabia wanayo sana,ukienda pale chuo ubaharia kila idara wamejazana wenyewe,yan pale ni vululu vululu,kulikua na wakenya na waganda wanakuja kwa wingi kusoma pale ila now wameanza kupakimbia sababu ya utaratibu wa kishamba
Kama ni kweli, hiyo hali inabidi idhibitiwe haraka
 
Hapana, nani wa kuomba control no. kabla ya kuweka data zake vizuri?. Just last week walinitumia ujumbe wa kuja kuchukuwa control no kulipia amount ikatajwa pia na deadline ikatajwa.
 
KNK......Huyu mwamba ana chapa kazi na matokeo ya kazi yake yanaonekana,umeme ulikua zaidi ya kero,atleast tumeanza kuinjoi,shughuli za kiuchumi zinaenda,umeme umetulia.
Ishu ya kuzuia likizo,nadhani ni ilikua ishu ya mpito sababu ya kukabiliana na kadhia iliyokuwepo,hawezi kuzuia likizo milele,sheria za kazi na mahusiano kazini zipo wazi.
Chapa kazi Mzee wa "Kusema na Kutenda"
KNK...
 
Umeme umeanza kuonekana kwa sababu ya kuchapa kazi au mvua kujaza mabwawa?
 
Angekuwa ameyafanya yote haya na umeme bado unasumbua ningekuunga mkono ila kwakuwa sasa hivi umeme ni uhakika binafsi naona alikuwa sahihi.
 
Unaweza kumtengenezea control number?
Hii ni huduma self service, si lazima uende TRA. Hata yeye akiwa na ile karatasi yake ya assessment anaweza kujitengenezea. Infact mtu yeyote anaweza kujitengenezea. Unaingia tu kwenye taxpayer portal self service na kufanya. Kinachohitajika ni debit number. Ukiwa nayo unaweza kujitengenezea. Hata wewe nenda taxpayer portal kuwa na tin kama username na password. Ukisha log in. Unaweza kujifanyia. And yes mtu akikupa debit number yake, ukiingia kwenye portal ya TRA( i mean uki log in ) unaweza kumtengenezea conntrol number.

Na infact kama ni ya kwako mwenyewe hata debit number huitaji kuikumbuka ukishalogin in utaziona hizo robo tatu zilizobaki. Robo ya mwezi wa sita. robo ya mwezi wa tisa na robo ya mwezi wa kumi na mbili. Unachagua ulipe robo moja, mbili au zote tatu. Then una generate control number.

Hope this will help.
 
Hatutaki story za jaba, umeme ndio tunataka.hata ingekua mimi ningefanya the same,likizo ya nini na umeme hakuna!

Watz tukipata wachapakazi hatutaki tunataka viongozi wanaotuletea stress tu.

Biteko piga kazi,siku hizi umeme umetulia.
 
Mkuu suala la likizo tu ndiyo imekushawishi kusema kuwa Dotto amekosea sana na hawezi kuvaa viatu vya Magufuli au kuna kingine zaidi ya hapo.
Kwa Taarifa yako tu, hapa Tanzania bado hatujapata kiongozi mwenye afadhali including wewe kama ni kiongozi wa kisiasa hapa Tanzania. Vp DP WORLD uwekezaji wao hapo Bandarini unaona dalili ya kuleta manufaa?
 
Likizo tu ndo uongee yote haya?
 
Mmeanza majungu baada ya kuona umeme umeanza kutulia ili turudi kulekule sasa hao kama wa kanda ya ziwa wanachapa kazi na umeme unapatikana shida ipo wapi?
Au unataka wa kanda yako alafu umeme usiwepo
Hiko ndiyo kiwango chako cha kujua Jambo fulani ni majungu, mwambie afute katazo lake na awake sawa uendeshaji wa shirika kwani maamuzi mengi yameelemea kwenye Ukanda wa Ziwa ni hatari kwa ukuajia wa shirika. Kupatikana Kwa umeme si kigezo cha kuwepo kundi moja kubwa kwenye hatma ya shirika mbona hakuleta huo umeme wa uhakika miezi 6 nyuma huko. Hata akiwa wa kanda yangu lakini asiwe wa kuwagawa watu na huduma iwepo na vile siyo muumini wa Ukanda zaidi ya utanzania na maslahi ya Chama zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…