Sasa kipi ni kipi?

Maji yawe mengi tupate umeme ama maji yawe kidogo?

Excuses za Tanesco zimekuwa za hovyo kweli. Na zote kisingizio ni maji.

Kiangazi, wanalalamika maji ni kidogo. Yamepungua kina. Sawa, mvua zimenyesha kunabadilika kuwa mvua zimekuwa nyingi, tunayapunguza. WTF!.

Walijenga bwawa kubwa kama lile bila ya kuweka viashiria kama litajaa kama litajaa kabla ya wakati?
 
Shule za kusomea ujinga:

 
Kwani hayo maji ya ziada hayawezi kuhifadhiwa sehemu halafu muda ukifika wa kuyahitaji wanayatumia?
 
Nafikiri aliekufa alikufa na mradi wake.. lakini sitaki kuamini hili maana sio kwamba wanashindwa ni kujiendekeza na ni upuuzi tupu,ifike hatua muone aibu kila siku porojo yule mzee aliona mbali alijua miaka michache ijayo kutakuwa na upungufu wa umeme maana nchi inakuwa hii, na ndio maana akaleta hilo bwawa..

Ukweli ni kwamba umeme ulikuwa hautoshi na ndio maana mgao ulikuwa ni mkali wala siswala la mvua. sasa kinachotokea ni kwasababu ya walafi fulani tu ili wafanye biashara zao za mafuta na majenereta hovyo kabisa,nina chuki na watu wa hovyohovyo ujinga tupu.
 
Hawana hela ya kuleta mitambo mingine? Mbona ma v8 yanaletwa bila kujiuliza? Nashauri viongozi wapigwe mnada fedha ipatikane ya mitambo. Mvua zinawataka waharakishe wao wanajizungusha tu
 
Kwani hayo maji ya ziada hayawezi kuhifadhiwa sehemu halafu muda ukifika wa kuyahitaji wanayatumia?
Hapo ni kama unawaambia wachimbe bwawa lingine. Cha msingi kama mitambo ni michache waongeze mingind na wauze umeme kama wanaona nchini hauhitajiki. Na kama unahitajika bei ya umeme ipunguzwe wananchi wafurahie matunda ya viongozi walio jikana nafsi kuanzisha mradi
 
St
Storage facilities za umeme wa megawatt 200 mpaka 1000 ni kama zipi? Mabetry 1000,000 ya gari yatumike kutunza charge? Kuna vifaa gani special?

Kila mwenye betri la la gari asiye na kazi nalo,tunaliomba
 
JPM alikurupuka kujenga bwawa kwa kutumia ramani za miaka ya sabini, akaambiwa, akajifanya chizi, hakufanya hata environmental impact assessment, maji yakiachiwa yanaenda katika mashamba ya wananchi na nyumba zao hapo rufiji, soon tutasikia habari ya mafuriko hapo rufiji.

Hata kipande cha reli alichojenga JPM ndicho kina kelele za kimazingira, pale Morogoro lile tuta linafanya maji yasiwr na njia, kwa hiyo yanarudi kwa wananchi na kusababisha mafuriko. Natamani wale wakazi wa maeneo yanayopata mafuriko kutokana na kutofanywa kwa Environmental Impact Assessment wafungue kesi dhidi ya serikali.

Ni muhimu serikali ikawa na msimamo kwenye mambo ya kitaalamu kuliko kukimbizana na presha za kisiasa
 
Du members wa Jamii forums,NI wataalam wa kila kutu,Wana ponda na kulaumu hata vitu cya kitaalamu,shida Sana.
 
Si ajabu hiyo turbinę yenyewe waliyokuwa wanaitumia washaikongoloa huko kupunguza maji ni kisingizio tu.

Juzi wamemwaga maji mpaka maeneo ya jirani kufurika hata week mbili hazijapita maji yamejaa tena.

Shida ni ujuaji waliotengeneza mashine wameshauri testing ifanyike taratibu mpaka mwezi wa sita ndio waanze kuitumia mitambo at full capacity (its for good monitoring reasons kwa upande wa manufacturer) serikali ya Tanzania inajua zaidi kuliko waliotengeneza hizo turbinę wamelazimisha matumizi ya full capacity washakongoloa mtambo hakuna warranty cover kutengeneza lipa.

Very useless and predictable people
 
Tanzania kuna shida kubwa sana
 
Maelezo ya Kitapeli tu haya. Tuliwambia ccm imezeeka haiwezi tena kuleta mabdiliko ndani Nchi.

Wanachojua wao ni ufisadi, wizi wa mali za umma, kuteua na kupeana vyeo tu.
 
Wakiyapunguza, mvua zikikata itabidi sasa tungoje mpaka 2026 bwawa lijae tena.

kizungumkuti.

Mitanzania ni mijinga ya mwisho duniani.
Mvua ikinyesha umeme unakatwa kuwa maji yako mengi ,ikiacha kunyesha umene unakatwa tunaambiwa tatizo maji kidogo
Hii nchi kuna shida kwa kweli
 
Storage facilities za umeme wa megawatt 200 mpaka 1000 ni kama zipi? Mabetry 1000,000 ya gari yatumike kutunza charge? Kuna vifaa gani special?

Kila mwenye betri la la gari asiye na kazi nalo,tunaliomba
Pekeni huo umeme unaozidi hata Malawi au Zambia au kenya bure au wauzieni kwa bei ndogo mbona akili hamna nyie
 
Hayo yote hawakuwa wameyaona awali?

Hakukuwepo na contingency plans zozote zile kuhusu maji kuwa mengi?
Walijua kwasababu maneno haya ''Saddle dam' niliyapata wakati wa kufuatilia ujenzi
Ukiangalia clip za awali za ujenzi kuna 'saddle dam' mbili zimejengwa kwasababu ya kudhibiti maji yakizidi

Sasa tunaposikia haya kwakweli lazima tukubali kwamba Waafrika hatuwezi kujitawala
Kwamba umeme hakuna kwasababu maji yamejaa! Kama si upuuzi ni ujinga wa hali ya juu sana

Anayesema hayo bila aibu si yule fundi wa VETA ni Naibu Waziri mkuu!

JokaKuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…