Dotto Biteko: Tumezima mtambo wa bwawa la Mwl Nyerere
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amesema kuwa mashine moja iliyokuwa imewashwa kwenye bwawa la Mwl Nyerere imezimwa baada ya maji kujaa sana kwenye bwawa kinyume na matarajio ya awali kwamba bwawa hilo litatumia miaka 2 kujaa lakini sasa limetumia mwezi mmoja tu kujaa na sasa maji yanalazimika kupunguzwa.

Hapo mwanzo Chadema walitoa tahadhari kwamba bwawa halitajaa kutokana na miti millioni 3 kukatwa na Magufuli hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira na ukame nchini.
Suala hapa ni kwamba Mvua zimeendelea kunyesha kwa kiwango kilichopitiliza kote nchini.
Na watanzania wote ni mashuhuda wa hilo.
Chadema wao ni wa kusamehe bure maana kwa ujumla ni kwamba hawajui wanataka nini na wanakataa nini?
Pale wamejaa walora wa kisiasa tupu
 
Nchi ipi ulishasikia imezima mitambo ya umeme kwasababu ya ongezeko la maji? Tunayo mabwawa ya Kidatu na Mtera, kujaa kwa maji ndiyo burudani yenyewe. Kuna tatizo la kiufundi kwenye ujenzi wa hili bwawa la mwal. Nyerere ndiyo sababu mashine zimezimwa baada ya maji kuongezeka. Unataka mwanasiasa asemeje, atatafuta soft reason kuwapumbaza watu kama nyinyi. Kila kitu kwenu ni ushabiki wa CCM & Chadema. Tuna kizazi kisichotumia akili
 
Nijuavyo Mimi bwawa lolote la kimkakati linapojengwa Kuna kitu kinaitwa "SPILL WAY" Yaani mlango wa kupunguzia maji hasa yanapozidi sasa yaweza kuwa bwawa hili pamoja na dhamira njema lakini lilijengwa Kwa mihemko ya kuipinga CHADEMA utaalam ukawa hauzingatiwi kisa kuwakomoa CHADEMA ndo maana lolote litakalotokea bwawani liwe jema au changamoto ktk kuielezea jambo hilo CHADEMA lazima itajwe mfano ni huyu mleta mada,
 
Spill zipo lakini zimepuuzwa
 
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amesema kuwa mashine moja iliyokuwa imewashwa kwenye bwawa la Mwl Nyerere imezimwa baada ya maji kujaa sana kwenye bwawa kinyume na matarajio ya awali kwamba bwawa hilo litatumia miaka 2 kujaa lakini sasa limetumia mwezi mmoja tu kujaa na sasa maji yanalazimika kupunguzwa.

Hapo mwanzo Chadema walitoa tahadhari kwamba bwawa halitajaa kutokana na miti millioni 3 kukatwa na Magufuli hivyo kupelekea uharibifu wa mazingira na ukame nchini.
Hata jangwani mvua huwa inanyesha mara moja moja. Hivi karibuni Libya ilikumbwa na mafuriko.

Amandla...
 
Sasa kipi ni kipi?

Maji yawe mengi tupate umeme ama maji yawe kidogo?

Excuses za Tanesco zimekuwa za hovyo kweli. Na zote kisingizio ni maji.

Kiangazi, wanalalamika maji ni kidogo. Yamepungua kina. Sawa, mvua zimenyesha kunabadilika kuwa mvua zimekuwa nyingi, tunayapunguza. WTF!.

Walijenga bwawa kubwa kama lile bila ya kuweka viashiria kama litajaa kama litajaa kabla ya wakati?
 
Nadhani concept ni moja.

Kuna mashine 9, inayofanya kazi ni moja. Bwawa linatakiwa kuhifadhi maji ya mashine 9.

Sasa kama mashine moja kati ya 9 ndio inafanya kazi, maji mengine hayana sababu ya kuwepo pale, lazima yafunguliwe yaondoke.

Iwapo mashine zote 9 zingekua zinafanya kazi basi hayo maji bado yasingetosha.

Ni serikali kuhakikisha mashine zote zinawashwa kwa wakati mmoja tu ama vinginevyo yale maji yote yatapotea bure.
Tupeleke kwenye umwagiliaji!
 
Back
Top Bottom