DOKEZO Dotto Magari atasababisha watoto wengi kukataa shule

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ingekuwa nchi za kimafia akifika hospital unachukua ugonjwa kama cancer au hepatitis unamuambukiza alafu unamuacha na maneno yake baada ya siku 180 kwisha habari yake ndio atajua elimu ina heshima kuliko upuuzi wake. Pesa Haiwezi dhidi Elimu hata siku moja
 
Tatizo siyo la Dotto Magari, bali tatizo ni la kitaifa. Rais wetu ana elimu gani? Baadhi ya wabunge wetu wana elimu gani? Kwanini tunachagua makamu/rais na wabunge wa aina hii?

Tunaendekeza ujinga kama taifa, hivyo tumeanza kuvuna matunda ya ujinga wetu.

Mleta mada kwann unamlwumu Dotto Magari na hulaumu wabunge ambao wemekuwa walitumia platform ya bunge kuibagaza elimu?

Ni mara ngapi Msukuma, Kishimba na Lusinde (kibajaji) wamejigamba kwa kuwa wao ni darasa la 7 na kuibagaza elimu na maprofesa wa nchi hii?
 
mtu alikuwa ana nunua simu za wizi ndio mnunuaji mkubwa wa simu za wizi na spear za magari za wizi.tunaye mjua watu wakinondoni tukae kimya leo kelele kibao katusua
 
Elimu kiujumla ni nihitaji muhimu kwa kila mwanadamu.

Ila wasomi wetu hapa nchini ndio wanasababisha elimu ionekane ni kitu cha hovyo, wasomi wetu ndio wanahusika kwa kiwango kikubwa kutukwamisha kwenye nyanja tofauti.

Mfano,
Wasomi wetu ndio wapokea na watoa rushwa ili kupindisha mambo fulani kwa manufaa binafsi.

Wasomi wetu ndio wezi wa pesa kwenye miradi na mali za umma na kupelekea miradi kufa au kujiendesha chini ya kiwango

Wasomi wetu sio wazuri kwenye kutumia taaluma zao kuvumbua, kuleta unafuu au kutatua changamoto zinazoikabiri nchi.

Unakutana na muhitimu wa chuo anakwambia ana mtaji wa M1 ila hajui afanye nini, unabaki kumshangaa kama elimu yake haiwezi kumsaidia yeye mwenyewe kutafuta taarifa kuzichakata na kufanya maamuzi kwahuo mtaji alonao atawezaje kutumia elimu yake kuwahudumia wengine.
 
Yule teja nae ni wa kuwanyima raha kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…