Double Standard: Kwa mwaka huohuo mmoja wa kalenda, Sherehe za Mapinduzi Zanzibar sawa, ila Sherehe za Uhuru wa Tanganyika hapana

Double Standard: Kwa mwaka huohuo mmoja wa kalenda, Sherehe za Mapinduzi Zanzibar sawa, ila Sherehe za Uhuru wa Tanganyika hapana

Hivi una matatizo gani wewe?! Nani anazungumzia suala la Sherehe ya Muungano hapo?!
Juzi tulipumzika bila ya kulazimika kuangalia gwaride na makomandoo wenye kuvunja matofali vifuani mwao na pesa zinakwenda kutumika kwenye masuala mengine.

Hizo nongwa nyingine ni upuuzi tu wa humu mitandaoni.
 
Mnashikia bango mada ya kitoto sana, kuna mtu kamzuia mtanzania wa kawaida kusherehekea sikukuu ya uhuru?.

Rais akiwa mkuu wa nchi kaamua pasiwe na shamra shamra za uwanjani siku hiyo na pesa ikafanye shughuli nyingine za maana zaidi, hilo nalo ni kosa kwa akili zetu!.
Ila sherehe za ccm na mapinduzi ya Zanzibar hazisitishwi.
 
Uhuru wa Tanganyika wa tarehe 9 Desemba.
Kwanini mpumzike kwa ajili ya Uhuru wa Tanganyika wakati umeshasema:-
Uhuru wa Tanganyika baadae ukaitwa uhuru wa Tanzania baada ya muungano wa mwaka 1964, kitu ni kile kile tatizo nchi yetu kila kitu kinaongelewa kisiasa zaidi.
Kwahiyo mlipumzika kwa ajili ya Uhuru wa Tanganyika au wa Tanzania ambao ndo kwanza nausikia kutoka kwako?!
 
Kwanini mpumzike kwa ajili ya Uhuru wa Tanganyika wakati umeshasema:-

Kwahiyo mlipumzika kwa ajili ya Uhuru wa Tanganyika au wa Tanzania ambao ndo kwanza nausikia kutoka kwako?!
Kuna ubaya gani kupumzika kwa ajili ya nchi yetu?.

Ni nchi yetu haijalishi ilikuwa Tanganyika kabla ya 64 na hivi sasa ni Tanzania.
 
Kwa maoni yangu, hili halijakaa sawa.

Sherehe hizi ni za Wananchi au ni za Viongozi tuliowaweka madarakani? Je, bila kufanya kinachosemekana ni Kitaifa pale uwanja wa Uhuru, nchi imekosa njia ya namna huku vijijini Matombo wananchi tukasherehekea?

Wadau naombeni maoni yenu,tuishauri Serikali yetu.
Wewe Mtanganyika(Chogo) ni koloni la Zanzibar, pigania uhuru kwanza ujikomboe kutoka katika makucha ya utawala wa Kizanzibari ndipo uje kujipanga jinsi ya kusherehekea uhuru kwa namna uonavyo inakufaa.
 
Kuna ubaya gani kupumzika kwa ajili ya nchi yetu?.

Ni nchi yetu haijalishi ilikuwa Tanganyika kabla ya 64 na hivi sasa ni Tanzania.
Unaona sasa!! Hivi unadhani hoja hapo ni kupumzika au jinsi unavyochanganya kati ya Uhuru wa Tanganyika na Muungano?!
 
Usipindishe Mada. Unataka kusema Uhuru wa Tanganyika ilikuwa 1961/ 1962 au 1961? Nyinyi ndo mnaovamia mada bila kuwa na hoja.
Screenshot_20241209-124302.jpg
 
Huyu mama anasikitisha Sana kwani sherehe za Uhuru lazima zitumie pesa sherehe za Uhuru wa nchi ni muhimu Sana Sana kuliko sherehe zozote katika nchi

Futeni mwenge kwanza unateketeza mabilioni ya pesa!! Sio kuchezea sherehe za mashujaa wetu!!
Mwenge ndiyo ndiyo upuuzi unaotia kichefuchefu kilichopitiliza, kwa mliwahi kuuona hepu wekeneni faida mlizopata labda kuna kitu wengine tumepungukiwa kwa kutowahi kuuona.
 
Tanzania ilipumzika juzi, hilo ni muhimu. Hizi siasa zenu pelekeeni watoto wa sekondari zinawahusu zaidi.
Wewe ndo unastahili kupelekwa huko kwa watoto wa sekondari ili wakakupe shule kuhusu tofauti ya Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya ZNZ na Muungano wa Tanganyika na ZNZ!
 
Wewe ndo unastahili kupelekwa huko kwa watoto wa sekondari ili wakakupe shule kuhusu tofauti ya Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya ZNZ na Muungano wa Tanganyika na ZNZ!
Mbwembwe tu hizo mkuu, Sherehe za uhuru mwaka huu hazikufanyika, hayo maswali ya kwanini sherehe za mapinduzi zilifanyika halafu za uhuru hazikufanyika ni mada ya kipuuzi tu imo humu JF, haina msaada wowote ule kwa jamii ya watanzania.
 
Back
Top Bottom