DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Vipi kuhusu ushuru wa magari utashuka au ndio yale yale ya kodi 110% ya bei ya kuagiza?
Ndugu yangu, huu ushuru ni hatari. BMW X6 inauzwa na kuletwa yaani CIF $10,108 TRA wanaweka katika Calculator yao $18,741. Unawaonesha kuwa hili gari invoice ni halali, wao wanakomaa tu. Kwa hili hata aje PD - Kuzimu siamini anaweza kutusaidia kulilekebisha. Ujanja ni kupitisha magari Zanzibar
 
Unaweza kumleta humu nasi tumtwange yetu? Je, ni mwarabu wa Dubai au ni mzawa??
 
Sasa ukipitishia Zanzibar halafu ukalileta bongo sindio unalipa difference uliokwepa TPA? 🤣
 
Ukiwa CCM unakuwa kama kipofu
 
"Nimefafanuliwa na mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga maswali" Kwahiyo kila alichokuwa anakwambia huyo mwanasheria wewe ulikuwa unameza tu na kusema tawile. Kwahiyo kama amekudanganya nawe unatudanganya sisi pia. Kikwete aliwahi kusema "za kuambiwa changanya na zako"
 
Nibora apige mbongo pesa iingie kwenye mzunguko kuliko hao Mapharao
 
Nadhani Uungwana ulitakiwa ulete hoja yako au useme wapi nimedanganya ndo unitukane ili kufurahisha nafsi yako. Mengine unajishushia heshima Mkongwe kama wewe kushindwa kujadiliana kwa hoja.
Hoja kwenye hamna acha uchawa
 
Nibora apige mbongo pesa iingie kwenye mzunguko kuliko hao Mapharao

Hiyo sasa ni chuki dhidi ya waarabu, hivi unajiskiaje kumchukia mwenzio!! Unapata faida gani!!! Kabla ya wao kuja, umefaidika na nini katika bandari hiyo?

Acha chuki, anae umia na kuteseka ni wewe, na sio wao, yani wao wala hawana time na wewe, matrilionea wale, wakiamua kuinunua nchi nzima hawashindwi, ni sekunde tu washamaliza, hela wanazo mzee. Wewe unalalamikia kabandari tu wakati wenzio wamewekeza nchi mbali mbali maviwanda, mabandari n.k!!!

Narudia tena na tena, acha chuki

Nimemaliza, Bhujiku ng'waka nkoi
 
Kilichojadiliwa na kupitishwa bungeni ni kitu gani? Tulijadili kuazimia kumpa bandari ngapi Tanganyika, bandari ngapi Zanzibar? Na kwa miaka mingapi?
 
sawa wewapetu
 
Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.
Kwa hiyo wewe ni mjuaji zaidi ya hao serikali katika maelezo yao?

Ingekuwa hivi kama unavyoeleza hapa, sida ingetoka wapi.
Usitake kufikiri kuwa wewe ni mjanja zaidi ya hao wengine wote.
Huo mkataba wa IGA ndivyo unavyoeleza, kama wewe unavyoeleza hapa?

Huko Bungeni haya uliyoeleza hapa ndiyo yaliyowasilishwa kwa wabunge na kulazimisha wayapitishe kwa udi na ubani?

Jambo rahisi kabisa, kama wewe ulivyoliweka hapa litawashinda vipi serikali nzima kulieleza kwa uwazi kwa wananchi wake?
Usitake kuwajaza ujinga watu ambao ni werevu kukuzidi wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…