DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Vipi kuhusu ushuru wa magari utashuka au ndio yale yale ya kodi 110% ya bei ya kuagiza?
Ndugu yangu, huu ushuru ni hatari. BMW X6 inauzwa na kuletwa yaani CIF $10,108 TRA wanaweka katika Calculator yao $18,741. Unawaonesha kuwa hili gari invoice ni halali, wao wanakomaa tu. Kwa hili hata aje PD - Kuzimu siamini anaweza kutusaidia kulilekebisha. Ujanja ni kupitisha magari Zanzibar
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Unaweza kumleta humu nasi tumtwange yetu? Je, ni mwarabu wa Dubai au ni mzawa??
 
Ndugu yangu, huu ushuru ni hatari. BMW X6 inauzwa na kuletwa yaani CIF $10,108 TRA wanaweka katika Calculator yao $18,741. Unawaonesha kuwa hili gari invoice ni halali, wao wanakomaa tu. Kwa hili hata aje PD - Kuzimu siamini anaweza kutusaidia kulilekebisha. Ujanja ni kupitisha magari Zanzibar
Sasa ukipitishia Zanzibar halafu ukalileta bongo sindio unalipa difference uliokwepa TPA? 🤣
 
Mkuu labda kama umefunga akili yako kusikia unachotaka kusikia. Hakuna kitu kinauzwa bali sehemu tu ya bandari ya Dar anapewa Muwekezaji. Nakazia sehemu ndani ya Bandari ya Dar. Wanaosema ni bandari zote watafuta Kiki za kisiasa ili kujenga chuki dhidi ya watendaji, Bunge na kumkosea adabu rais.
Ukiwa CCM unakuwa kama kipofu
 
"Nimefafanuliwa na mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga maswali" Kwahiyo kila alichokuwa anakwambia huyo mwanasheria wewe ulikuwa unameza tu na kusema tawile. Kwahiyo kama amekudanganya nawe unatudanganya sisi pia. Kikwete aliwahi kusema "za kuambiwa changanya na zako"
 
Wengi wanoikataa DP World ni wale waliozoea Upigaji na wanajua wakija hawana chao.

Waliozoea hela za ICD na minada ya Bandari na kubambikizia kodi ili wapate Rushwa, hawapendi kuona DPW inakuja bongo.

Watatumia kila njia kupinga hata kupotosha Raia.
Nibora apige mbongo pesa iingie kwenye mzunguko kuliko hao Mapharao
 
Nadhani Uungwana ulitakiwa ulete hoja yako au useme wapi nimedanganya ndo unitukane ili kufurahisha nafsi yako. Mengine unajishushia heshima Mkongwe kama wewe kushindwa kujadiliana kwa hoja.
Hoja kwenye hamna acha uchawa
 
Nibora apige mbongo pesa iingie kwenye mzunguko kuliko hao Mapharao

Hiyo sasa ni chuki dhidi ya waarabu, hivi unajiskiaje kumchukia mwenzio!! Unapata faida gani!!! Kabla ya wao kuja, umefaidika na nini katika bandari hiyo?

Acha chuki, anae umia na kuteseka ni wewe, na sio wao, yani wao wala hawana time na wewe, matrilionea wale, wakiamua kuinunua nchi nzima hawashindwi, ni sekunde tu washamaliza, hela wanazo mzee. Wewe unalalamikia kabandari tu wakati wenzio wamewekeza nchi mbali mbali maviwanda, mabandari n.k!!!

Narudia tena na tena, acha chuki

Nimemaliza, Bhujiku ng'waka nkoi
 
Hakuna bandari hata moja amepewa si Tanganyika wala Zanzibar. Na hata hiyo bandari atakapewa sehemu ya bandari ya Dar tu pale TICTS alipokuwa kama haya maazimio bunge limepitisha yatakubalika.

Hadi sasa tumepewa miezi 1w kujadili maazimio kabla ya kuyasiani ili Mkataba wa kuendesha bandari usainiwe. Huo Mkataba sasa ndo watasema tutakuwa tunarenew baada ya Muda gani? Miaka 2,10,20 au mongapi? Hivyo vinakaa kwenye Mkataba sio Maazimio ya Nchi na Nchi ya Ushirikiano kwenye Uendelezaji wa Uchukuzi majini.
Kilichojadiliwa na kupitishwa bungeni ni kitu gani? Tulijadili kuazimia kumpa bandari ngapi Tanganyika, bandari ngapi Zanzibar? Na kwa miaka mingapi?
 
Hiyo sasa ni chuki dhidi ya waarabu, hivi unajiskiaje kumchukia mwenzio!! Unapata faida gani!!! Kabla ya wao kuja, umefaidika na nini katika bandari hiyo?

Acha chuki, anae umia na kuteseka ni wewe, na sio wao, yani wao wala hawana time na wewe, matrilionea wale, wakiamua kuinunua nchi nzima hawashindwi, ni sekunde tu washamaliza, hela wanazo mzee. Wewe unalalamikia kabandari tu wakati wenzio wamewekeza nchi mbali mbali maviwanda, mabandari n.k!!!

Narudia tena na tena, acha chuki

Nimemaliza, Bhujiku ng'waka nkoi
sawa wewapetu
 
Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.
Kwa hiyo wewe ni mjuaji zaidi ya hao serikali katika maelezo yao?

Ingekuwa hivi kama unavyoeleza hapa, sida ingetoka wapi.
Usitake kufikiri kuwa wewe ni mjanja zaidi ya hao wengine wote.
Huo mkataba wa IGA ndivyo unavyoeleza, kama wewe unavyoeleza hapa?

Huko Bungeni haya uliyoeleza hapa ndiyo yaliyowasilishwa kwa wabunge na kulazimisha wayapitishe kwa udi na ubani?

Jambo rahisi kabisa, kama wewe ulivyoliweka hapa litawashinda vipi serikali nzima kulieleza kwa uwazi kwa wananchi wake?
Usitake kuwajaza ujinga watu ambao ni werevu kukuzidi wewe.
 
Back
Top Bottom