DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Kumbe wasomi wote nchini wanaoupigia kelele mkataba ni hamnazo except mleta mada na watu wawili wengine toka Kiembembuzi
 
Unamtishia nani nyau?

hao uliowataja hapo mbona ni nyau ukilinganisha na madhara yatakayotokana na huyo DP World?

Cha kushangaza hapa hata huoni aibu kulaumu hivi vipanya, badala ya hiyo hiyo serikali kuvishughulikia.

Naona akili yako ya kupambanua mambo ni fupi sana, kama hao wanaotuingiza kwenye uhujumu huu huko serikalini, wasiojua njia sahihi za kushughulikia matatizo yetu, badala yake wanakimbilia mapapa ya dunia kuja kutumaliza kabisa.
 
Kwani umeona wapi siku hizi mizigo inasafirishwa nje ya makontena? Ukipewa kuhandle containers ndio sawa umepewa bandari yote.
Halafu mnadanganyika na kauli. Hati iliyotiwa sahihi na waziri hamuoni? Wataenda hatua moja and then fumba fumbua wanashika kila kitu.
Kama nia yao sio kutoa bandari yote kile waliyotia sahihi ni nini?
Tuliona ulaghai wa kwenye richmond/dowans. Tukaona epa, ticts, iptl, kwenye madini ndio usiseme. Ulaghai wa hawa madalali kwenye serikali ya ccm ni kibao.
 
Hatutaki hii ni nchi ya watanganyika wewe kibaraka ulitolewa ubongo uboho kawambie waliokutumia HATUTAKI
 
Wametoa miezi 12 tuweke inputs zetu kwenye hili azimio then baada ya hapo ndo Mikitaba inatiwa wino kazi inaanza
 
Tufanyeje sasa? Tuoa maoni yako
 
Mkuu, Magari na mafuta vinawekwa kwenye Contena? Sijakuelewa.

Unajua Meli ya Magari inatia nanga wapi na meli ya mafuta inatia nanga wapi?
Ushafika bandari ya Dar? Makontena ndo DP WORLD wanahusika tu basi
 
Hebu tupe sehemu ya mkataba wa makubaliano ya miaka mitano tuione.
Ndo maana nimependekeza Mkataba uwekwe kwa kiswahili ili watu kama wewe wasiendelee kupotoshwa
 
Wengi hawakatai DP kuwekeza ktk bandari zetu kama unavyosema, tatizo liko kwenye baadhi ya vifungu vya msingi wa mkataba uliopitishwa.
Ndo maana nasema kuna watu wamelishwa matango pori. Hadi sasa hakuna mkataba wowote uliopitishwa. Hata bunge limepitisha maazimio sio Mkataba. Jipeni muda kusoma mambo
 
Mim niliyajua haya. Kwanin wakenya ndio wapinge.sisi tulikua twasubir gar imekuja mara ipo sijui icd gan mara icd gan usumbufu mtindo mmoja.mwisho bond.waje dp kwanza middle east huko ndio kuna mapesa kwa sasa,
Hao waKenya gani wamepinga ebu wataje tuwanange.
Maana kila mtu anawalaumu bila kuwataja.
 
Ni zaidi ya Happ. Ndio maana imebidi nchi mbili ziingie makubaliano. Ingekuwa kuchukua nafasi wala wasingehitaji nchi mbili kukaa.
Nchi mbili zipi,au ni kati ya nchi na kampuni.
Maana nchi ni United Arab Emirates.sio Dubai,wala hiyo kampuni ya DP World.
 
Yule katumia lugha ya Kisheria, mimi nimetumia lugha nyepesi ili uweze kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…