Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe wasomi wote nchini wanaoupigia kelele mkataba ni hamnazo except mleta mada na watu wawili wengine toka KiembembuziWatu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.
Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.
Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.
Unamtishia nani nyau?Wengi wanoikataa DP World ni wale waliozoea Upigaji na wanajua wakija hawana chao.
Waliozoea hela za ICD na minada ya Bandari na kubambikizia kodi ili wapate Rushwa, hawapendi kuona DPW inakuja bongo.
Watatumia kila njia kupinga hata kupotosha Raia.
Kwani umeona wapi siku hizi mizigo inasafirishwa nje ya makontena? Ukipewa kuhandle containers ndio sawa umepewa bandari yote.Salaam Wakuu,
Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.
Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.
Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.
Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.
Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.
Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.
Nimewapenda bure DP World.
Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?
Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.
Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.
Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.
Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.
Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.
Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania
Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.
Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.
Watanzania tujitafakari na tujielewe.
Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?
Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.
Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.
Hatutaki hii ni nchi ya watanganyika wewe kibaraka ulitolewa ubongo uboho kawambie waliokutumia HATUTAKIWengi wanoikataa DP World ni wale waliozoea Upigaji na wanajua wakija hawana chao.
Waliozoea hela za ICD na minada ya Bandari na kubambikizia kodi ili wapate Rushwa, hawapendi kuona DPW inakuja bongo.
Watatumia kila njia kupinga hata kupotosha Raia.
Wametoa miezi 12 tuweke inputs zetu kwenye hili azimio then baada ya hapo ndo Mikitaba inatiwa wino kazi inaanzaMkataba uwe tu fine polished kwa kuzingatia maoni Muhimu lakini Kazi iendelee!
Hiki ni Kitu Kizuri sana na Siku si Nyingi Watu watajua tunaye Rais wa Faida!
Achilia mbali mambo ya SIASA-Nampongeza sana Mh Rais Samia na asife Moyo kwa Sababu maamuzi haya ni ya Kishujaa.
Siku Tra itatangaza kwamba tumefikia Makusanyo ya T 3 mpk 4 kwa Mwezi ndo watu watamuelewa Mama!
Tena kama inafaa Mwarabu angetupa Mkopo wa 20T(au upfront payment au interest free loan)deductable kwenye operations ingetupa millage kweli!
Na pesa iyo nusu inaenda kwenye Miundombinu ya Barabara na nusu kwenye Kilimo na Ufugaji kupitia Mabank Maalumu kwa Agriculture,Livestock and Aquaculture ili tuweze kuwa na Mizigo ya ku export kupitia Bandari kwa kuwa sasa kutakuwa na professional Handling and logistics!
By the way
Kondoo wetu,Mbuzi wetu na Ng'ombe wetu si wataenda kuuzwa hapo Middle East kwa Sababu hawa Mabingwa wakiona fursa kidogo tu wanaunganisha Biashara na Dunia Nzima.
Mimi nadhani Serikali ituandae sisi wafanyabiashara ili tuweze kuchukuana na Fursa zitakazotokana na Ufanis wa Bandari Mpya!
Swali
Ni lini hii kitu itakuwa imekamiliks na Kuanza Kazi??
Tunachelewa Bhana!!!
Tufanyeje sasa? Tuoa maoni yakoKitu mnachosau ni kuwa England iko vizuri hata kabla ya DP World. Siyo sawa na sisi wenye ka rail line kamoja kutoka bandarini. Kama ingekuwa rahisi kihivyo mbona bandari ya Beira haina hizo technology na standards ingawa wapo pale kwa miaka kadhaa. Au kwa mawazo yetu ni kwamba sisi tuko so special sana kwa Warabu kwa hiyo wayatufanyia tofauti na wengine siyo.....!!?
Mkuu, Magari na mafuta vinawekwa kwenye Contena? Sijakuelewa.Kwani umeona wapi siku hizi mizigo inasafirishwa nje ya makontena? Ukipewa kuhandle containers ndio sawa umepewa bandari yote.
Halafu mnadanganyika na kauli. Hati iliyotiwa sahihi na waziri hamuoni? Wataenda hatua moja and then fumba fumbua wanashika kila kitu.
Kama nia yao sio kutoa bandari yote kile waliyotia sahihi ni nini?
Tuliona ulaghai wa kwenye richmond/dowans. Tukaona epa, ticts, iptl, kwenye madini ndio usiseme. Ulaghai wa hawa madalali kwenye serikali ya ccm ni kibao.
Ndo maana nasema kuna watu wamelishwa matango pori. Hadi sasa hakuna mkataba wowote uliopitishwa. Hata bunge limepitisha maazimio sio Mkataba. Jipeni muda kusoma mamboWengi hawakatai DP kuwekeza ktk bandari zetu kama unavyosema, tatizo liko kwenye baadhi ya vifungu vya msingi wa mkataba uliopitishwa.
Hao waKenya gani wamepinga ebu wataje tuwanange.Mim niliyajua haya. Kwanin wakenya ndio wapinge.sisi tulikua twasubir gar imekuja mara ipo sijui icd gan mara icd gan usumbufu mtindo mmoja.mwisho bond.waje dp kwanza middle east huko ndio kuna mapesa kwa sasa,
Nchi mbili zipi,au ni kati ya nchi na kampuni.Ni zaidi ya Happ. Ndio maana imebidi nchi mbili ziingie makubaliano. Ingekuwa kuchukua nafasi wala wasingehitaji nchi mbili kukaa.
Yule katumia lugha ya Kisheria, mimi nimetumia lugha nyepesi ili uweze kuelewa.Kwa hiyo waziri wa Ujenzi na Uchukuzi alikuwa hajui hicho unachotuambia sasa? Mpaka akashindwa kukielezea kama unavyokielezea wewe??? Tumemsikiliza vizuri sana pale Bungeni, hakusema hicho unachokisema wewe. Kama angesema hicho, angeeleweka kirahisi sana. Usitutoe kwenye reli Mkuu..