DP World hawawekezi bandari zote, tusimmezeshe maneno Chongolo!

Ulishaacha UCHOKO??tuanze na hilo kwanza[emoji1787][emoji1787]
 
Akibanwa aonyeshe kifungu gani kwenye mkataba kinaongelea hayo aliyoyasema anakimbilia kuomba msaada kwa vijana wa Wambura
 
Achana nao hawa Suphian. Hawa wamechanganyikiwa kwa hiyo walichobaki nacho ni kuomoteza maneno na kutengeneza hekaya zao ili kufurahisha genge!
 
Mzunguko wote wa Nini? Kinacholalamikiwa bado hakijibiwi wanajizungusha tu. Yatolewe majibu kwa maswali yafuatayo: Ikiwa mkataba huu ni mzuri, kwa Nini bandari za Zanzibar hazimo kwenye mkataba? Mkataba huu una ukomo? I bara ya 4(2) inayosema iwapo Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini ndio basi, je, ni halali nchi huru, Tena kwa mali zake ikaombe ridhaa Dubai? Jibuni maswali yenye utata msizunguke.
 
KIFUNGU CHA 2
LENGO LA MKATABA

  1. Madhumuni ya Mkataba huu ni kuweka mfumo wakisheria wa maeneo ya ushirikiano kwa ajili ya maendeleo, uboreshaji, usimamizi na uendeshaji wa bandari za bahari na maziwa, kanda maalum za kiuchumi, hifadhi za usafirishaji, korido za kibiashara na miundombinu mingine ya kimkakati ya bandari nchini Tanzania. Maeneo ya ushirikiano pia yanajumuisha kujenga uwezo, uhamisho wa ujuzi, utaalam na teknolojia, kuimarisha taasisi za mafunzo na msaada wa utafutaji wa masoko.
 
Hebu kwanza! Ilani ilizungumzia kuboresha Bandari! Nani anapinga? Hakuna. Ila ilani haiongeleii kuhusu mkataba wa kiupuuzi kama wa DP world. Bagonza kaweka suala hili vizuri.

Ila serikali na wapiga porojo ndiyo wanapotosha ati watu hawataki uwekezaji! La hasha kila mtu anakubali ila siyo mkataba ulivyo. Liwe ni suala la TPA na DP World tu. Si la nchi na Bandari zote big no
 
Charity begins at home! Kama ungekuwa mzuri, wazanzibari wangeupeleka kwao kwanza
 
KIFUNGU CHA 5
HAKI ZA KUENDELEZA, KUSIMAMIA AU KUENDESHA






1. Nchi Wanachama zinakubali kwamba DPW itakuwa na haki ya kipekee ya kuendeleza, kusimamia na/au kuendesha Miradi kama ilivyoainishwa katika Kiambatisho cha 1 Awamu ya 1,
 
Hawa mapoyoyo na mapunguwani wa JF wasikuumize kichwa, wanaelewa sana kila kitu. Tuwachie sisi tuna deal hapa.
Poyoyo na punguani,[emoji56][emoji15][emoji125][emoji125][emoji125]
Your browser is not able to display this video.
 
Sawa uzushi lakini mkataba wa IGA umesema kuwa bandari zote za bahari na maziwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…