DP WORLD HAWAWEKEZI BANDARI ZOTE, TUSIMMEZESHE MANENO CHONGOLO!!
Hansard ya Bunge ikinukuu neno kwa neno kikao cha tarehe 10 June 2023 kuhusu Azimio la Bunge kuhusu mkataba wa bandari zote za pwani na maziwa makuu
Mwanasheria Mohamed Salum anasema mkataba mama wa tarehe 10 Juni 2023 wa Azimio la Bunge
MKUTANO WA KUMI NA MOJA
Kikao cha Arobaini na Tano – Tarehe 10 Juni, 2023 VIDEO NA KUMBUKUMBU YAKE YA HANSARD
HANSARD YA BUNGE
10 JUNI, 2023
1
BUNGE LA TANZANIA
________
MAJADILIANO YA BUNGE
_________
MKUTANO WA KUMI NA MOJA
Kikao cha Arobaini na Tano – Tarehe 10 Juni, 2023
(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)
D U A
Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua
SPIKA: Waheshimiwa tukae.
Katibu.
NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE:
HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI
Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-
WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI:
Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania ilianzishwa kupitia Sheria Namba 17 ya mwaka 2004...
SPIKA: Mheshimiwa Waziri ni hati ya kuwasilisha mezani siyo
hoja. (Makofi)
WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI:
Maelezo ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi juu ya Azimio la
Bunge kuhusu pendekezo la kuridhiwa
Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa
10 JUNI, 2023
2
lengo la kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika
uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini la mwaka 2023.
Spika: Ahsante sana, Mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja
ambayo ilihusisha Kamati mbili; Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya
Umma na Kamati ya Miundomibu kwa niaba yao Mheshimiwa Augustino Holle Vuma ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa PAC.
MHE. VUMA A. HOLLE – Kn.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA
PAMOJA:
Maoni ya Kamati ya Pamoja kuhusu Azimio la Bunge kuhusu
pendekezo la kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la
kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.
SPIKA: Ahsante sana.
Katibu.
NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc –
KATIBU WA BUNGE:
HOJA ZA SERIKALI
AZIMIO LA BUNGE KUHUSU PENDEKEZO LA KURIDHIWA
MKATABA BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KWA LENGO LA KUANZISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIJAMII KATIKA UENDELEZAJI WA MAENEO YA BANDARI NCHINI
SPIKA: Sasa Waheshimiwa Wabunge nimuite Mheshimiwa
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi aje awasilishe hoja kuhusu Azimio la
Bunge kuhusu pendekezo la kuridhiwa Mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai.
Mheshimiwa Waziri Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.
10 JUNI, 2023
3
WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ilianzishwa kupitia Sheria Namba 17 ya mwaka 2004. Mamlaka hii iliridhia na kuchukua majukumu ya yaliyokuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Harbors Authority) iliyoanzishwa kupitia Sheria ya Mamlaka ya Bandari namba 12 ya mwaka 2012 ya mwaka 1977 baada ya kuvunjika ya iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupewa majukumu zaidi ya kumiliki, kuendesha na kuendeleza
bandari zilizopo Pwani ya Bahari ya Hindi na Maziwa Makuu.
Mheshimiwa Spika, Sheria hiyo ya Bandari Namba 17 mwaka
2014 inaipa TPA majukumu ya kumiliki, kusimamia, kuendesha na kuendeleza maeneo yote ya Bandari Tanzania Bara. Madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa TPA yameainishwa katika kifungu
namba tano cha sheria hiyo ambayo ni kuhakikisha Tanzania
inaendelea kunufaika na faida ya kijiografia ikiwemo kuchagiza
usimamizi bora na ufunganishaji wa tija wa bandari zilizoko Pwani
ya Bahari ya Hindi na Maziwa Makuu, kuhakikisha kunakuwa na
tija katika huduma zinazotolewa za upakiaji na ushushaji wa
mizigo pamoja na abiria, kuendeleza, kuboresha na kusimamia
miundombinu ya kibandari, kusimamia usalama wa bandari na
kuingia mikataba au makubaliano na mtu yeyote au taasisi
yoyote kwa ajili ya utoaji wa huduma za bandari.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuwekeza kwenye
bandari zake kwa vipindi tofauti tofauti kwa kutumia vyanzo
vyake na fedha za mikopo katika kutekeleza mikakati kwa lengo
la kuboresha sekta ya bandari nchini. Mikakati iliyochukuliwa hivi
karibuni ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa uboreshaji wa
Bandari ya Dar es Salaam (Dar es Salaam Maritime Gateway
Project) ambao umehusisha kwanza, uimarishaji na uongezaji wa
kina cha Gati Namba 01 mpaka Namba 07; ujenzi wa Gati jipya
la kuhudumia magari na uongezaji wa kina cha lango cha
kuingia Bandari ya Dar es Salaam. Uzoefu umeonesha kuwa
uwekezaji wa namna hii una faida kubwa kwa nchi iwapo
bandari itaendeshwa kwa tija na ufanisi mkubwa kwa kutumia
teknolojia ya kisasa.
10 JUNI, 2023
4
Mheshimiwa Spika, pamoja na kuchukua hatua mbalimbali
za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam bado ufanisi katika
utoaji huduma za bandari haujafikia viwango vinavyofikiwa
kimataifa. Hali ya sasa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam
imeendelea kuwa kiwango cha chini ukilinganishwa na bandari
shindani kikanda. Kwa mfano, wastani wa meli kusubiri nangani
kwa Bandari ya Dar es Salaam ni siku tano, ikilinganishwa na siku
1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.
Ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na
changamoto mbalimbali zikiwemo:-
(i) Kukosekana kwa mifumo ya kisasa ya TEHAMA;
(ii) Kutokuweko kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya
bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena pamoja ya
maegesho ya meli; na
(iii) Kukosekana kwa mktambo ya kutosha na ya kisasa
kuhudumia shehena ambayo teknolojia yake inabadilika
mara kwa mara na ina gharama kubwa ya uwekezaji na
uendeshaji.
Mheshimiwa Spika, athari za kutokuwa na ufanisi katika
Bandari ya Dar es Salaam ni pamoja na meli kusubiri muda mrefu
nangani ambako kunasababiisha kuongezeka kwa gharama ya
kutumia Bandari ya Dar es Salaam. Kwa mfano, gharama za meli
kusubiri nangani kwa siku moja ni takribani dola za Kimarekani
25,000 sawa na takribani shilingi za Kitanzania 58,000,000 kwa siku;
meli kutumia muda mrefu kupakia na kupakia shehena gatini kwa
wastani wa siku tano ikilinganishwa na siku moja inayokubalika
kimataifa; na meli kubwa kutokuja katika Bandari ya Dar es
Salaam kutokana na kuchukua muda mrefu kuhudumiwa. Hali hii
husababisha bandari yetu kuwa siyo bandari inayolisha shehena
na bandari zingine (feeded port) na hivyo kuongeza gharama ya
kutumia bandari hiyo na kuikosesha nchi mapato ambayo
yangeweza kutumika katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya
kimkakati nchini ambayo ingesaidia kukuza uchumi na kuboresha
huduma za wananchi wetu.
10 JUNI, 2023
5
Mheshimiwa Spika, pia kuongezea gharama katika mnyororo
mzima wa uzalishaji (total route costs) kutoka nje ya nchi, kupitia
bandari yetu kwenda nchi za Jirani zinazotumia bandari yetu ya
Dar es Salaam. Kwa mfano, gharama kusafirisjhia kasha moja
kutoka nje ya nchi (on transit) kwenda nchi ya Jamhuri ya
Demokrasia ya Kongo inafikia takkribani dola za Kimarekani 8,500
hadi 12,000. Hii ni gharama kubwa sana ikilinganishwa na bandari
za nchi jirani au nchi shindani.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kuwa Serikali pekee
haitoweza kutatua changamoto zilizopo kwenye Bandari ya Dar
es Salaam, kuanzia miaka ya 2000 Serikali ya Awamu ya Tatu
iliingia Mkataba wa Upangaji na Uendeshaji (Lease and
Concession Agreement) na kampuni ya kimataifa ya uendeshaji
wa Vitengo vya Makasha Hutchson ya Hong Kong huko nchini
China. Mkataba huo ulidumu kwa takribani miaka 22 kuanzia
mwaka 2000 hadi mwaka 2022 na uliipa haki ya kipekee kampuni
hiyo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kuhudumia makasha
katika Gati Namba 08 hadi Namba 11 za Bandari ya Dar es
Salaam. Wakati huo huo TPA ikiendesha na kuhudumia maeneo
mengine ya bandari hiyo.
Mheshimiwa Spika, ili kutatua changamoto za bandari
zilizopo na kwa kuzingatia dhima ya Serikali ya kuboresha sekta ya
bandari nchini, ili kuongeza ufanisi na sekta ya bandari katika
mapato ya nchi, ajira na kuchagiza sekta nyingine za kiuchumi,
Serikali ilifanya maamuzi ya kutafuta wawekezaji wapya
wanaoendena na dhima ya Serikali. Hatua hizo zilihusisha
kupokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali wakiwemo
Makampuni ya Hutchson ya Hong Kong huko China, PSA
International kutoka Hong Kong, DP World ya kutoka huko Dubai,
Abu Dhabi Ports ya kutoka huko Abu Dhabi UAE, Adani Ports and
Logistics kutoka Mundra-India, Kampuni ya CMA - CGM kutoka
Ufaransa pamoja na kampuni ya EPMA Maersk kutoka huko
Denmark.
Mheshimiwa Spika, lengo kuu ni kufungua masoko ya
kimkakati katika eneo la bidhaa na biashara ya usafirishaji ndani
ya nchi na kanda zinazotuzunguka. Katika kupitia mawasilisho ya
10 JUNI, 2023
6
kampuni hizo pamoja na sifa zao za kimataifa, Serikali imeamua
kuanzisha majadiliano na Kampuni ya DP World kwa kuzingatia
uzoefu wake katika uendeshaji wa shughuli za bandari Barani
Afrika, Asia, Ulaya na Maerkani ya Kaskazini ya Kusini. Kampuni hii
ina uzoefu na utaalam wa kuchagiza myororo mzima wa
usafirishaji (end to end total logistics chain solution) kutoka
maeneo ambayo bidhaa zinatoka mpaka kufikia kwa walaji.
Mheshimiwa Spika,
uendeshaji wa maeneo maalum ya
kiuchumi (special economic zones) karibu na bandari, usafirishaji
wa baharini na nchi kavu kupitia njia ya reli; uwekezaji mkubwa
katika maeneo mbalimbali ambayo imewekeza na pamoja kuajiri
wazawa katika maeneo haya. Aidha, kwa upande wa mamlaka
au makampuni mengine ambayo TPA ilipokea mapendekezo yao
yalionesha nia ya kuwekeza bandarini peke yake na siyo
kuchagiza mnyororo mzima wa usafirishaji.
Mheshimiwa Spika, pia baadhi ya makampuni hayo hayana
uwezo wa kuendesha shughuli za bandarini Barani Afrika wakati
Kampuni ya DP World inaendesha bandari sita Barani Afrika na
bandari zaidi ya 30 duniani kote kwa ufanisi mkubwa sana.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia nia ya Serikali kuvutia
uwekezaji nchini wakati wa Maonesho ya Dubai Expo 2020 tarehe
28 Februari, 2022 hati ya makubaliano takribani 30 ilisainiwa baina
ya taasisi za Serikali za Tanzania na sekta binafsi za Tanzania na
taasisi za Serikali na sekta binafsi za huko Dubai kwa lengo la
kuvutia uwekezaji nchini ili kuchochea ukuaji wa uchumi na
maendeleo ya nchi.
Mheshimiwa Spika, moja kati ya makubaliano hayo ni baina
ya TPA na DP World iliyolenga kuanzisha ushirikiano wa uboreshaji,
uendeshaji na uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.
Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha utekelezaji wa hati ya
makubaliano hayo, Serikali iliteua timu ya wataalam ambayo
ilipewa jukumu la kufanya majadiliano na wataalam wa Serikali
ya Dubai na kufanikisha kuandaliwa na kusainiwa kwa
10 JUNI, 2023
7
makubaliano baina ya Serikali na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Dubai kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
Makubaliano hayo ni kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamiii
kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari
Tanzania.
Mheshimiwa Spika, lengo la makubaliano haya ni kuweka
msingi wa makubalino (framework agreement) baina ya nchi na
nchi ili kuwezesha kuanza kufanyika kwa majadiliano na kuingiwa
kwa mikataba mbalimbali kama vile mikataba ya nchi mwenyeji,
upangishaji na uendeshaji kwa ajili ya uwekezaji na uendeshaji wa
maeneo ya bandari nchini.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa masharti ya makubaliano
hayo unapaswa kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ili utekelezaji wake
uweze kuanza. Hivyo Serikali kupitia Wizara ya ujenzi na uchukuzi
imeanzisha mchakato wa kupata ridhaa ya Serikali ya kuwasilisha
makubaliano hayo hapa Bungeni kwa ajili ya kuridhiwa.
Mheshimiwa Spika, ufafanuzi kuhusu mkataba wa
makubaliano hayo; kwa mujibu wa ibara ya pili ya makubaliano,
lengo ni kuweka msingi wa ushirikiano baina ya Serikali mbili kwa
maeneo mahususi yaliyoainishwa ndani ya makubaliano husika,
rejea appendix namba moja ya makubaliano hayo ambayo
utekelezaji wake utafanywa kupitia mikataba mahususi baina ya
taasisi zilizoidhinishwa katika makubaliano kama taasisi tekelezi
ambazo ni TPA na DP World. Hivyo makubaliano haya hayana
masharti yanayoifunga Serikali kuhusu maeneo ya ushirikiano
yaliyoainishwa pasipokuwa na mikataba mahususi ya utekelezaji
wa miradi inayojadiliwa na kukubaliwa na pande zote mbili.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, mawanda ya utekelezaji chini ya
makubaliano haya yatahusisha uendelezaji na uendeshaji wa
baadhi ya maeneo ya bandari na siyo bandari yote kwa ujumla ..... makofi
10 JUNI, 2023
8
Aidha, uendelezaji na uendeshaji huo utafanyika kupitia
mikataba mahususi ya miradi (project agreements) ambayo
itajadiliwa na kuingiwa kwa kila eneo la ushirikiano na itahusisha
matumizi ya ardhi pekee na siyo umiliki wa ardhi ikiwa ni pamoja
na Serikali kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu za nchi
zinalinda umiliki wa ardhi ya Watanzania zinazingatiwa na
kusimamiwa ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, makubaliano haya yameainishwa
awamu mbili za maeneo ya ushirikiano; awamu ya kwanza
itajumuisha kusimamia, kuendesha na kuendeleza baadhi ya
magati katika Bandari ya Dar es Salaam, maboresho ya gati la
majahazi na gati la abiria katika Bandari ya Dar es Salaam ili
kuvutia vyombo vikubwa Zaidi na meli za kitalii kutia nanga katika
Bandari ya Dar es Salaam, kuwekeza katika maeneo
yaliyotengwa katika bandari kavu, kufanya uwekezaji katika
mifumo ya kisasa ya TEHEMA ya kuendesha shughuli za kibandari
ili kuongeza ufanisi wa bandari kuwa shindani na kuwajengea
uwezo watumishi wa TPA kutekeleza shughuli za bandari kwa
ufanisi katika maeneo mengine ya bandari nchini. Msisitizo wa
Serikali ni kuhakikisha maeneo yote ya nchi yanabaki chini ya
umiliki wa Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika awamu ya pili ya miradi yaani
phase two majadiliano haya yatafanyika kwenye maeneo
mbalimbali ikiwemo kuongeza thamani ya bidhaa, maeneo ya
viwanda na miundombinu mingine itakayoongeza ufanisi katika
usafirishaji wa bidhaa kwenda na kutoka nchi zinazotuzunguka,
kuwekeza katika bandari zingine za bahari na maziwa kama
itavyopendekezwa na Serikali kupitia TPA kwa kuzingatia ulinzi na
maslahi mapana ya Taifa, na kuwekeza katika vyombo vya
usafirishaji wa shehena yaani matishari katika maziwa makuu ili
kuunganisha bandari za maziwa makuu na bandari za nchi za
jirani kama itavyopendekezwa na TPA na kukubaliana na
mwekezaji.
Mheshimiwa Spika, ili kutoa fursa kwa wawekezaji wengine
kuwekeza katika maeneo mengine ya bandari nchini kwa lengo
la kuleta ushindani, tija na ufanisi, uwekezaji tarajiwa chini ya
10 JUNI, 2023
9
mkataba huu hautahusisha maeneo ya Gati Namba 8 hadi 11,
yaani Kitengo cha Pili cha Makasha, Gati la Mafuta Kurasini
Namba 1 (KOJ 1), Gati la Mafuta Kurasini Namba 2 (KOJ 2), Boya
la Kupokelea Mafuta (SDM) na Gati la Kuhudumia Magari katika
Bandari ya Dar es Salaam pamoja na maeneo yote ya awamu ya
kwanza na ya pili ambayo hayatafikia muafaka katika
majadiliano yatakayofanyika baada ya kuridhiwa kwa
makubaliano haya. Uwekezaji huo pia hautahusisha Bandari ya
Tanga na Bandari ya Mtwara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, makubaliano hayo yatatoa haki ya
upekee ya kufanya majadiliano kwa awamu ya miradi
iliyoainishwa kwenye makubaliano hayo kwa kipindi kisichozidi
miezi 12. Msingi wa kutoa haki hii ya kipekee ni kuwezesha pande
mbili kufanya majadiliano na kumpa uhakika mwekezaji
kujadiliana katika maeneo pasipokuwepo na majadiliano na
mwekezaji mwingine katika maeneo hayo hayo. Hivyo, iwapo
kipindi hicho kitakwisha bila kufikia makubaliano TPA ina uwezo
wa kuanzisha majadiliano na wawekezaji wengine katika maeneo
hayo pasipo kuwepo kwa mgogoro wowote chini ya
makubaliano haya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu muda; makubaliano haya
yatakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa
au kwisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na
mikataba ya miradi. Msingi wa makubaliano hayo kuendana na
mikataba ya miradi ni kutokana na kwamba unaweka msingi
unaowezesha kuingia na kutekelezwa kwa mikataba hiyo nchini.
Iwapo makubaliano hayo yatakuwa na ukomo kabla ya kuisha
mikataba ya miradi iliyo chini ya makubaliano haya utekelezaji
wa mikataba ya miradi baada ya kuisha kwa makubaliano hayo
itakuwa batili.
Mheshimiwa Spika, vilevile uhai wa makubaliano haya
utawezesha kuingiwa kwa mikataba mbalimbali yenye masharti
na muda wa ukomo tofauti na ambayo yote inategemea msingi
wa uhai wa makubaliano haya. Hivyo, endapo upande mmoja
wa makubaliano haya utajitoa athari yake ni kufa au kuvunjika
10 JUNI, 2023
10
kwa utekelezaji wa mikataba yote ya miradi iliyoanzishwa chini ya
makubaliano haya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jukumu la ulinzi na usalama katika
Bandari ya Dar es Salaam litaendelea kusimamiwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyombo vyake vya
ulinzi na usalama ambavyo vipo katika maeneo yote ya bandari
kwa kuzingatia sheria za nchi na mikataba ya kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, suala hili limezingatiwa pia katika
makubaliano haya na kuwekwa bayana kwamba masuala ya
ulinzi na usalama hayatakiukwa kwa namna yoyote wakati wa
utekelezaji wa shughuli za uwekezaji. Vilevile taasisi zote za Serikali
ambazo zinahusika katika shughuli za bandari zitaendelea
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ndani ya eneo
la bandari. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, uwepo wa sekta binafsi kutoa huduma
katika maeneo ya bandari umeendelea kuwepo na kusimamiwa
na Serikali kwa miongo tofauti tofauti. Aidha, katika kipindi chote
ambacho sekta binafsi imejihusisha katika uendeshaji wa bandari
hakujawahi kujitokeza tukio la kuhatarisha usalama wa nchi yetu.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba kuwataarifu kwamba, uwepo
wa ajira za Watanzania hususan watumishi wa Bandari ya Dar es
Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika azimio hili,
bali kila aina ya uwekezaji ambayo nchi itaufanya. Ibara ya 13 ya
makubaliano inaitaka DP World kuendeleza ajira za watumishi
wote waliopo, kuajiri Watanzania pamoja na kuwaendeleza
kitaaluma. (Makofi)
Vilevile makubaliano haya yameweka wazi bayana masharti
ya Kampuni ya DP World kutumia wakandarasi wa ndani katika
manunuzi ya huduma na bidhaa pamoja na kusaidia vyuo vya
mafunzo vya nchini katika masuala ya elimu ya usafirishaji maji
Soma zaidi toka : 10 June 2023 Bunge kuhusu pendekezo la kuridhiwa mkataba baina ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai
Kwa hisani kubwa ya Bunge
:
Parliament of Tanzania
Bunge la Tanzania / Parliament of Tanzania