DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

Kichwa cha habari..
" TUPUUZE"
Inatupa ujumbe tosha kuwa hufai kuaminiwa na makala ni batili.

Ungetoa hoja ili watu wachague kupuuzia hizo kelele au waendelee.

Pascal Mayalla ...umasikini na ukweli havikai pamoja.

Msimamo na njaa ni maadui.

Umasikini na ukweli ni maadui.

Acha njaa za kijinga, simania haki acha upotoshaji.

Alichofanya Sa100 ni Loliondo part2 tena hii ni mbaya kuliko Loliondo ya Mwinyi.
 
Mkuu Paskali, kongole nyingi zikufikie kutokana na umahiri wako katika fani ya uandishi wa habari hapa nchini, sambamba na uelewa wako mzuri wa mambo ya sheria. Ila kwa upande wangu nafikiri ungalianza na uchambuzi wa kisheria kuhusu kile kilichoridhiwa na Bunge letu kuhusu makubaliano haya, sambamba na maeneo yote ambayo unayohisi yana ukakasi wa kisheria. Natambua Watanzania wengi wana hamu kubwa kusikia mapungufu yalitopo ndani yake kuliko sifa zilizosheheni katika mkataba husika. Wengi wana mashaka kuhusu usiri, vifungu vyenye mitego ama hila mbaya, na pia uharaka wa kufanya maamuzi makubwa bila ushiriki wa wadau wengi katika suala zima la uendeshaji wa bandari za Tanzania Bara.

Kukwepa kuzungumzia ukomo wa mkataba, kutokuweza kutenguliwa kwa mkataba uliofungwa kupitia sheria za kimataifa kwa sababu zozote zile, ama kutokuguswa kimkataba kwa bandari za upande wa Tanzania Visiwani ni mambo ambayo kwa vyovyote vile hayakwepi kuamsha hisia na mihemko yenye uelekeo hasi kwa upande wa serikali na hata Bunge letu kwa kadiri ambavyo wamekwisha lishughulikia jambo hili nyeti kitaifa, kikanda na kimataifa.

Mimi nafikiri ndivyo ambavyo ungalipaswa kujielekeza katika andiko lako la leo. Maudhui uliyoweka katika andiko lako la leo ni kama vile unataka kuuzunguka mbuyu ili kukwepa kukikosoa moja kwa moja chama chako na viongozi wote wanaonyoshewa vidole, kushutumiwa, na pia kulaumiwa kutokana na sakata hili.
 
Tunachotaka ni majibu ya hoja zetu, sio uzuri wa DPWORLD au nia njema ya mhe. Rais. Nakumpa mfano mdogo tu, gari la serikali likipata itilafu likawa halitengenezeki unadhani unaweza kuliuza ndani ya mwezi au wiki kama mali yako binafsi? Je ukiliuza ndani ya wiki au mwezi huoni kuwa ni faida kuliko kusubiri vibali vikamilike ambavyo vyaweza kukamilika baada ya miaka 5 nakukuta gari lenyewe lilishaoza, lkn watu wakiuliza kwanini gari umeliuza bila kufuata utaratibu uwape majibu, na kumbuka kuna watakaosema unauza mali za serikali hovyo hovyo.
 
Halafu hiyo IGA inasema wazi kwamba HGA zinapaswa kufuata masharti yaliyoko kwenye IGA.

HGA ni mkataba wa kuwezesha utekelezaji wa IGA na sio mkataba wa kufanya mabadiliko ya IGA.

HGA na IGA hazipaswi kwenda kinyume kwa kadiri ya masharti yaliyowekwa kwenye IGA. Kwahiyo hizi ahadi za kutuambia ati tusubiri mabadiliko kwenye HGA ni ahadi za urongo ambazo haziwezekani kisheria.

Hapa tuseme tu kwamba SAMIA KABORONGA.

Njia iliyopo ni KUFUTA IGA na MoUs zote waanze upya au waachane kabisa na huo mpango.

Na nikiuangalia huu mkataba wa IGA unaonesha kabisa haujaandaliwa na WANASHERIA, umeandaliwa chumbani na watu wenye NIA OVU.
 
Lengo la mama ni zuri lakufanya bandari yetu ifanye kazi kwa manufaa ya watanzania wote na sisi wanainchi wakawaida tunaomba wale wenye profetiona zao za sheria washirikishwe kwa kiwango kikubwa kuepusha sintofahamu iliyotanda.
 
Paschal Mayala(Nzala)umeandika vizuri kwani umepongeza Sana. Tuanzie hapa.
1. Umesema IGA ni makubaliano kati ya nchi na nchi. Je Dubai ni nchi? Tuelimishe hapo.
2. Unajua kwamba kuna tofauti kati ya mkataba wa nchi na nchi na mkataba kati ya nchi na kampuni au taasisi? je ni mkataba upi unapaswa kupelekwa Bungeni? .
3. Tupo na awamu ya Samia, Magufuli ameingiaje hapo? Je mshindani mkuu wa Samia ni Magufuli?
4. Unadhani Watanzania wote Hawa wa ndani na Diaspora ni wajinga kupiga kelele zote hizi? Huoni kama kuna kitu hakiko Sawa?
5. Bandari ni zetu, kwanini wao watupe masharti magumu hivyo, je kati ya sisi na wao nani alipaswa kumpa masharti mwenzake???
6. Wamekuambia hata kama uhusiano wa kidiplomasia utakufa wao mkataba wao uko pale pale? Bro imekaaje hiyo ? Huoni kama ni mtego?
7. Wanakupa mkataba usio na kikomo(lifetime) huoni kama ni matapeli Hawa.
8. Wanataka ardhi kila watakapohitaji kwa shughuli zao,.huoni kama Watanzania watafurushwa Sana na Jamaa watajaa kwa wingi huku. Hapa wametutega kuna ajenda nyuma yake. Ni kichaa tu anaweza kukubali masharti haya
Ngoja niishie hapo bro. Bro sisi kutokuwa na mamlaka na umasikini wetu haimanishi kwamba na kichwani hazipo. Na si kweli kwamba kila tajiri na mwenye mamlaka ana akili kuliko wengine. Tunategemeana...
 
nimesoma mkala yako, kwa uweledi mkubwa kama mtanzania,

nimegundua na kuona yafuatayo;
1. kweli najua wewe ni msheria, ila andiko lako lina ombwe kubwa sana la sheria za investment,
2. paragraph yako ya pili, unatushutumu kuwa hatujui IGA, na HGA na ulichokieleza kwenye andiko lako nadhani wewe ndio huna ufahamu wa hizo terms, na namna zinavyotumika kwenye sheria za uwekezaji.

2. udadavuaji wako wa IGA na HGA unaonyesha hujajipa kazi kuelewa implication za IGA in case of breach in HGA?, hivyo naweza kuhitimisha pia tafiti yako kwenye sheria za uwekezaji hujaitendea haki
3. aidha kwa makusudi au kutokujua, ukisoma paragraph 8 umeeleza IGA imeenda Bungeni kwa hisani ya Samia hivyo tumpongeze kwa ujasiri, nilidhani kama wakili na mwandishi ingeeleza wajibu wa international agreement to be tendered to the parliament, confer (angalia) article (ibara) ya63 (3) (e) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
4. ukiendelea kusema IGA sio mkataba, unawakosea sana Watanzania, aidha kwa makusubi au kwa kutokujua, the implication ya makubaliano ya mataifa mawili (bilateral agreement) kwa level ya international agreemeent.
5. ebu waeleze watanzania kwa nini tanzania imeingia IGA kwenye investment ya bandari?, usisimply kuwa kuwa sio mkataba, na level yake ni nini ulipopelekwa bungeni? tukivunja makabuliano ya IGA kinafuata nini, waeleze haya kwa mtazamo wa investment laws, na consequences zake in case of breach of HGA, na inatumikaje hiyo IGA

6. mwisho napenda kuwashauri, ukisoma kuanzai paragraph yako ya kwanza hadi nane tayari umechagua upande, hivyo no neutrality ya kazi yako kama mwandishi,


please tumia sheria tueleze implication za IGA, and HGA kwenye investment laws.
 
Na hapa kuna ukakasi wa haya MAKUBALIANO YA IGA in reference to Article 63 (3) (e) ya Katiba ya nchi.

Haya ni makubaliano kati ya Serikali mbili, lakini yamepelekwa bungeni KANA KWAMBA ni makubaliano ya NCHI MBILI while in fact DUBAI sio NCHI.

Katiba inasemaje?? Huko mbeleni inaweza kuja kubainika kwamba kilichofanywa na BUNGE ni NULL and VOID.

Hili limkataba limekaa kimagumashi sana, ndio maana nazidi kusisitiza kwamba WANASHERIA hawakuandaa hili limkataba.

Sidhani kama MANGULI WA SHERIA wanaweza kuandaa limkataba la aina hii LENYE NIA OVU.

Sheria inasemaje pale ambapo mkataba ni ILLEGAL?? Mkataba unakiuka katiba, unakiuka sheria za mikataba na unakiuka THE NATURAL WEALTH AND RESOURCES PERMANENT SOVEREIGNTY ACT 2017.
 
Anapongezwa kwa mkataba usio na kikomo??? Tena kwa Bandari zetu zote (Bara)??

Nyinyi ndo walee, wandishi mliosafiri kwenda Dubai, na hamuwezi acha ujinga mliotoka nao huko

Mnajua mnachokifanya!

Lakini mjue, Mtadaiwa tu
 
Pascal umeanza nsha zako badala ya kusoma gap kwanza!! Anyway Bi Faizafoxy anakuja na ufafanuzi juu ya hili!!
 
Hapa kama kuna kaukweli furani mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Mi naona bora angejiweka pembeni kwenye hili swala ili heshmabyake iendelee kuwepo ila kwa kutetea kitu ambacho waliomzidi umri na akili na maarifa wao wameona sio sahihi yeye anaona ni sawa naona kama anajidhalilisha sana kwa heshma aliojijengea hapo jf
 

Asipokuelewa tena hapa ni mkaidi
 
Uzuri hakuna anayeweza zuia isitekelezwe
tunaeleza ujinga ulijikita kama taifa kwenye kuingia mikataba ya kipuuzi, ndio maana tunasema bandari imeuzwa, hatumuzuii kutumia mamlaka yake kufanya atakavyo kama alivyo saini hiyo mikataba, ila kama watanzania tuna haki kutoa mchango wetu wa kimawazo na kitafiti kueleza hayo
 
Let me also declare interest, am an entrepreneur specialist and writing a hand-on text in entrepreneurship and I have my intellectual properties which characterizes why business fail and possible solutions and also, entrepreneurial ecosystem for reflective practice. Swali fikirikirishi kwanini wabunge wa CCM, walilipigia chapuo jambo hili na kelele kwa mwelekeo chanya,wakati liko kwenye utaratibu wa IGA (in a positive way) na kuzuia watu wengine wasilijadili eti wao ndiyo mwisho wa kufikiri kwa wa Tnzania. je wengine hawana haki ya kutoa mawazo?. Kwa taarifa yako biashara nyingi zinakufa siyo kwasababu watu hawana elimu ya ujasriamali hata wenye elimu hiyo biashara zimekufa, na zimekufa kwasababu ya (uncertainty and uncertainty inherent) kushindwa kukabiliana na usiyoyatarajia kwenye biashara mfano corona, (covid-19), lakini sehemu kubwa kwasisi nchi zinazoendelea maamuzi ya kisiasa ndiyo yanaua biashara kwasababu mengi hatuyatarajii, sera ambazo wabunge hao hao wanazipisha bila kuju madhara yatakayotokea baade, (the aftermath of policies to be implented), pia teknologia inavyobadirika wale amabao hawawezi kwenda na kasi hiyo inasababisha biashara zipate msukosuko mfano wewe unapokuwa unasubiria mteja aje kwenye biashara yako mwingine hela ishaingia kwenye account, (networking).
 
Nichukue fursa hii kuendelea kumpongeza rais wetu Mama Samia, kwa kuendelea kuwa na ngozi ngumu!, maana kuna vitu vinasemwa, ikijiuliza kama angekuwa ni Magufuli, vingesemwa?. Hata huo mkataba wa IGA, tungeuona?, hata huko Bungeni ungepelekwa?. Mnyonge tumnyongeni jamani, haki yake mpeni!, kwenye hili la kupeleka mkataba huu wa IGA kuridhiwa na Bunge, ni jambo jema linalo stahili pongezi za dhati.

πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†
Magufuli hasingefanya upuuzi huu wa kuuza bandari,hakuwa mwizi,wala hakuwa na mpango wa kuuza Tanganyika, lini Tanganyika imeanza kutajwa tajwa,basi mficha ugonjwa kifo umuumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…