DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

Pascal ni mfurukutwa na mwanachama wa CCM! Usitarajie aikosoe serikali effectively, Pascal hata akiikosoa serikali ni indirect!!
 
Pascal ni mfurukutwa na mwanachama wa CCM kindakindaki usitegemee akosoe serikali!! Na ukiona anakosoa basi ni indirect!!
 

Pascal ni mfurukutwa na mwanachama wa CCM kindakindaki usitegemee akosoe serikali!! Na ukiona anakosoa basi ni indirect!!
kinachoniuma wanatumia kalamu zao kudanganya watanzania, yaani waandishi kwenye hili la bandari wameshindwa kuitetea tanzania acha nchi yenyewe ijipiganie,
 
Good thinking
 
Mimi nakubaliana na Wewe,na Asante kwa kutia Nia ya kutuelimisha Watanzania tusiolewa!
Lakini kinachofanya watu wapige kelele kwanza ni kutokana na historia ya nchi yetu kuingizwa kwenye Mikataba feki na wasomi wetu tena Wana sheria wetu ndicho kinachotufanya Watanzania tusimwamini hata Rais wetu hata kama ana Nia njema.
Lakini la pili ni usiri unaofanywa na serikali wakati wa kusaini Mikataba! Huu usiri unatufanya watanzania tuamini kuwa kuna harufu ya rushwa na ufisadi.
Tatu ni Wananchi kutoiamini serikali ya CCM kwa sababu CCM inaingia madarakani kwa rushwa na kupora kura Kwa mabavu! Wanasema hakuna jema ambalo mwizi anaweza kulifanya watu wakamwamini,hata lingekuwa jema kiasi gani.
Mwisho na Mimi niungane na Wewe kuwa huenda Mama ana Nia njema kabisa,ambayo kwa maslahi ya Taifa kila mpenda maendeleo atamuunga Mkono.
 
Ni matakwa ya IGA kuridhiwa na Bunge. Bila hiyo hatua hakuna IGA. Mbona kila siku tunaambiwa tumeingia mikataba mingi tu lakini hamna inayopelekwa bungeni.

Amandla...
 
Kuna Uzi Jana nilisoma umekomenti Et Ile ni IGA yaan MoU , sio HGA

Nilikujibu, ila bahati mbaya wakati najibu wakawa wameufuta ule Uzi.


JMT imeengia kwenye makubaliano ya Mkataba na DP World ambao Hawa ni foreign investor na sio Serikali ya UAE .


Makubaliano ya kimikataba ya Nchi na Foreign investors (HGA) juu ya project inayokwenda kua implemented Huwa ni LAZIMA YAWE YALE YANAYOMLINDA MUWEKEZAJI KIUCHUMI NA KISIASA BILA KUJALISHA MABADILIKO YOYOTE YA KISHERIA YA NCHI HUSIKA.

ndio Sababu Hiki kilichojadiliwa na Bunge na Watanzania mwanzo mwisho ,kinaonyesha namna gan DP world wamepewa mamlaka Kubwaaaa sana kuliko hata Nchi husika ,na hii ndio HGA yenyewe , yaan hata kama Mahusiano ya kidplomasia yakivunjika, Bado DP world wataendelea kunufaika !!.



Sasa mnapojaribu kuwaambia watanzania kua óhooo hizo ni IGA óhooo Hazina shida , Kwakweli, Tafuteni watanzania wajinga wajinga ndio muwadanganye.


Nadhani Kuna haja kubwa ya kutumia Kalamu na Umaarufu kusimamia katika Ile kweli !!.



Kwamba watanzania Mmoja Mmoja, Taasisi mbalimbali na vyama mbalimbali, Kulalamikia hii kitu, kwamba wote hao ni wajinga, Et Pasko Mayala ndio mwenye akili na genge lake ??.


HAPANA !!.
 
Wazungu wana usemi kuwa njia ya kwenda jehanum imewekwa lami ya nia njema.

Amandla...
 
Serikali haijaingia HGA hata moja kabla ya IGA kupata baraka za Bunge. Kwa sababu wigo wa IGA ni mpana kuliko bandari, HGA zinaweza kuwa nyingi tu na si lazima ziwe wazi.

Amandla...
 
Ndicho kilichopo , DP World Kwa werevu mkubwa na uwezo na uzoefu mkubwa wa haya mambo, WAMETUNUNUA.


Hiyo Pasko anayoita IGA, kiuhalisia ni HGA !!.
 
Ila mkuu,yule boss wa TPA alisema tulichoingia na Dubai(ambayo sio nchi),ni IGA,ambayo kwa maneno yake ni "regal binding"tukivunja tunashitakiwa,na hatukuingia MOU,kama unavyodai,
Mpaka Sasa tupo ndani ya mkataba,ambao tukivunja,tunashitakiwa!!na IGA sio MOU,MOU ni makubaliano ya kiungwana,sio regal binding,unaweza ukaachana nayo ukijisikia,ni sawa na kupiga chini mchepuko,usio toa huduma Bora,
 
Samia ni msaliti katutoa sadaka kwa mwarabu.
 
Haha Asante, nimekunywa. Ongea na Kaka yako Pascal amelewa kuwa katikati ya wenye nchi.

Kazi yake ni ku- spin stuffs vionekane more palatable to the public.

Hatuwezi jua labda kuna bahasha kaki kasogezewa maana anatumia gharama kubwa sana kuandika nakala zake didhani kama anatoa hela yake mfukoni
 
Hakika.
 
Hatuwezi jua labda kuna bahasha kaki kasogezewa maana anatumia gharama kubwa sana kuandika nakala zake didhani kama anatoa hela yake mfukoni

Ni kazi yake, ndio inamuweka mjini. Kuitetea CCM hata ikifanya uovu gani.

Vyovyote Pascal avyoviita IGA, HGA, MoU, dili, haya ni makubaliano / mkabata semantics stuffs. Kwa namna yoyote Ile ukiyaaangalia ni upuuzi.

USA,UK, China nchi yoyote inayojitambua haingekubali au kupewa dili la hovyo kama hili.

Wangemuhoji Rais vipengele vyote muhimu. Akizingua anaondolewa labda na kushtakiwa. Asingeruhusiwa kupuuza, kujificha.

Ila waandishi wetu nguli kama Pascal wanatetea upuuzi. Badala ya kuhoji, kufanya opposite. Inasikitisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…