DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

Paschal Mayala(Nzala)umeandika vizuri kwani umepongeza Sana. Tuanzie hapa.
1. Umesema IGA ni makubaliano kati ya nchi na nchi. Je Dubai ni nchi? Tuelimishe hapo.
2. Unajua kwamba kuna tofauti kati ya mkataba wa nchi na nchi na mkataba kati ya nchi na kampuni au taasisi? je ni mkataba upi unapaswa kupelekwa Bungeni? .
3. Tupo na awamu ya Samia, Magufuli ameingiaje hapo? Je mshindani mkuu wa Samia ni Magufuli?
4. Unadhani Watanzania wote Hawa wa ndani na Diaspora ni wajinga kupiga kelele zote hizi? Huoni kama kuna kitu hakiko Sawa?
5. Bandari ni zetu, kwanini wao watupe masharti magumu hivyo, je kati ya sisi na wao nani alipaswa kumpa masharti mwenzake???
6. Wamekuambia hata kama uhusiano wa kidiplomasia utakufa wao mkataba wao uko pale pale? Bro imekaaje hiyo ? Huoni kama ni mtego?
Ngoja niishie hapo bro. Bro sisi kutokuwa na mamlaka na umasikini wetu haimanishi kwamba na kichwani hazipo. Na si kweli kwamba kila tajiri na mwenye mamlaka ana akili kuliko wengine. Tunategemeana...
Pascal ni mfurukutwa na mwanachama wa CCM! Usitarajie aikosoe serikali effectively, Pascal hata akiikosoa serikali ni indirect!!
 
Na hapa kuna ukakasi wa haya MAKUBALIANO YA IGA in reference to Article 63 (3) (e) ya Katiba ya nchi.

Haya ni makubaliano kati ya Serikali mbili, lakini yamepelekwa bungeni KANA KWAMBA ni makubaliano ya NCHI MBILI while in fact DUBAI sio NCHI.

Katiba inasemaje?? Huko mbeleni inaweza kuja kubainika kwamba kilichofanywa na BUNGE ni NULL and VOID.

Hili limkataba limekaa kimagumashi sana, ndio maana nazidi kusisitiza kwamba WANASHERIA hawakuandaa hili limkataba.

Sidhani kama MANGULI WA SHERIA wanaweza kuandaa limkataba la aina hii LENYE NIA OVU.

Sheria inasemaje pale ambapo mkataba ni ILLEGAL?? Mkataba unakiuka katiba, unakiuka sheria za mikataba na unakiuka THE NATURAL WEALTH AND RESOURCES PERMANENT SOVEREIGNTY ACT 2017.
Pascal ni mfurukutwa na mwanachama wa CCM kindakindaki usitegemee akosoe serikali!! Na ukiona anakosoa basi ni indirect!!
 
Nichukue fursa hii kuendelea kumpongeza rais wetu Mama Samia, kwa kuendelea kuwa na ngozi ngumu!, maana kuna vitu vinasemwa, ikijiuliza kama angekuwa ni Magufuli, vingesemwa?. Hata huo mkataba wa IGA, tungeuona?, hata huko Bungeni ungepelekwa?. Mnyonge tumnyongeni jamani, haki yake mpeni!, kwenye hili la kupeleka mkataba huu wa IGA kuridhiwa na Bunge, ni jambo jema linalo stahili pongezi za dhati.

👆👆👆
Magufuli hasingefanya upuuzi huu wa kuuza bandari,hakuwa mwizi,wala hakuwa na mpango wa kuuza Tanganyika, lini Tanganyika imeanza kutajwa tajwa,basi mficha ugonjwa kifo umuumb

Pascal ni mfurukutwa na mwanachama wa CCM kindakindaki usitegemee akosoe serikali!! Na ukiona anakosoa basi ni indirect!!
kinachoniuma wanatumia kalamu zao kudanganya watanzania, yaani waandishi kwenye hili la bandari wameshindwa kuitetea tanzania acha nchi yenyewe ijipiganie,
 
Nichukue fursa hii kuendelea kumpongeza rais wetu Mama Samia, kwa kuendelea kuwa na ngozi ngumu!, maana kuna vitu vinasemwa, ikijiuliza kama angekuwa ni Magufuli, vingesemwa?. Hata huo mkataba wa IGA, tungeuona?, hata huko Bungeni ungepelekwa?. Mnyonge tumnyongeni jamani, haki yake mpeni!, kwenye hili la kupeleka mkataba huu wa IGA kuridhiwa na Bunge, ni jambo jema linalo stahili pongezi za dhati.

👆👆👆
Magufuli hasingefanya upuuzi huu wa kuuza bandari,hakuwa mwizi,wala hakuwa na mpango wa kuuza Tanganyika, lini Tanganyika imeanza kutajwa tajwa,basi mficha ugonjwa kifo umuumbua.
Good thinking
 
Mimi nakubaliana na Wewe,na Asante kwa kutia Nia ya kutuelimisha Watanzania tusiolewa!
Lakini kinachofanya watu wapige kelele kwanza ni kutokana na historia ya nchi yetu kuingizwa kwenye Mikataba feki na wasomi wetu tena Wana sheria wetu ndicho kinachotufanya Watanzania tusimwamini hata Rais wetu hata kama ana Nia njema.
Lakini la pili ni usiri unaofanywa na serikali wakati wa kusaini Mikataba! Huu usiri unatufanya watanzania tuamini kuwa kuna harufu ya rushwa na ufisadi.
Tatu ni Wananchi kutoiamini serikali ya CCM kwa sababu CCM inaingia madarakani kwa rushwa na kupora kura Kwa mabavu! Wanasema hakuna jema ambalo mwizi anaweza kulifanya watu wakamwamini,hata lingekuwa jema kiasi gani.
Mwisho na Mimi niungane na Wewe kuwa huenda Mama ana Nia njema kabisa,ambayo kwa maslahi ya Taifa kila mpenda maendeleo atamuunga Mkono.
 
Nichukue fursa hii kuendelea kumpongeza rais wetu Mama Samia, kwa kuendelea kuwa na ngozi ngumu!, maana kuna vitu vinasemwa, ikijiuliza kama angekuwa ni Magufuli, vingesemwa?. Hata huo mkataba wa IGA, tungeuona?, hata huko Bungeni ungepelekwa?. Mnyonge tumnyongeni jamani, haki yake mpeni!, kwenye hili la kupeleka mkataba huu wa IGA kuridhiwa na Bunge, ni jambo jema linalo stahili pongezi za dhati.

👆👆👆
Magufuli hasingefanya upuuzi huu wa kuuza bandari,hakuwa mwizi,wala hakuwa na mpango wa kuuza Tanganyika, lini Tanganyika imeanza kutajwa tajwa,basi mficha ugonjwa kifo umuumbua.
Ni matakwa ya IGA kuridhiwa na Bunge. Bila hiyo hatua hakuna IGA. Mbona kila siku tunaambiwa tumeingia mikataba mingi tu lakini hamna inayopelekwa bungeni.

Amandla...
 
Kuna Uzi Jana nilisoma umekomenti Et Ile ni IGA yaan MoU , sio HGA

Nilikujibu, ila bahati mbaya wakati najibu wakawa wameufuta ule Uzi.

JMT imeengia kwenye makubaliano ya Mkataba na DP World ambao Hawa ni foreign investor na sio Serikali ya UAE .

Makubaliano ya kimikataba ya Nchi na Foreign investors (HGA) juu ya project inayokwenda kua implemented Huwa ni LAZIMA YAWE YALE YANAYOMLINDA MUWEKEZAJI KIUCHUMI NA KISIASA BILA KUJALISHA MABADILIKO YOYOTE YA KISHERIA YA NCHI HUSIKA.

ndio Sababu Hiki kilichojadiliwa na Bunge na Watanzania mwanzo mwisho ,kinaonyesha namna gan DP world wamepewa mamlaka Kubwaaaa sana kuliko hata Nchi husika ,na hii ndio HGA yenyewe , yaan hata kama Mahusiano ya kidplomasia yakivunjika, Bado DP world wataendelea kunufaika !!.

Sasa mnapojaribu kuwaambia watanzania kua óhooo hizo ni IGA óhooo Hazina shida , Kwakweli, Tafuteni watanzania wajinga wajinga ndio muwadanganye.

Nadhani Kuna haja kubwa ya kutumia Kalamu na Umaarufu kusimamia katika Ile kweli !!.

Kwamba watanzania Mmoja Mmoja, Taasisi mbalimbali na vyama mbalimbali, Kulalamikia hii kitu, kwamba wote hao ni wajinga, Et Pasko Mayala ndio mwenye akili na genge lake ??.

HAPANA !!.
 
Mimi nakubaliana na Wewe,na Asante kwa kutia Nia ya kutuelimisha Watanzania tusiolewa!
Lakini kinachofanya watu wapige kelele kwanza ni kutokana na historia ya nchi yetu kuingizwa kwenye Mikataba feki na wasomi wetu tena Wana sheria wetu ndicho kinachotufanya Watanzania tusimwamini hata Rais wetu hata kama ana Nia njema.
Lakini la pili ni usiri unaofanywa na serikali wakati wa kusaini Mikataba! Huu usiri unatufanya watanzania tuamini kuwa kuna harufu ya rushwa na ufisadi.
Tatu ni Wananchi kutoiamini serikali ya CCM kwa sababu CCM inaingia madarakani kwa rushwa na kupora kura Kwa mababu! Wanasema hakuna jema ambalo mwizi anaweza kulifanya watu wakamwamini,hata lingekuwa jema kiasi gani.
Mwisho na Mimi niungane na Wewe kuwa huenda Mama ana Nia njema kabisa,ambayo kwa maslahi ya Taifa kila mpenda maendeleo atamuunga Mkono.
Wazungu wana usemi kuwa njia ya kwenda jehanum imewekwa lami ya nia njema.

Amandla...
 
Kuna Uzi Jana nilisoma umekomenti Et Ile ni IGA yaan MoU , sio HGA

Nilikujibu, ila bahati mbaya wakati najibu wakawa wameufuta ule Uzi.

JMT imeengia kwenye makubaliano ya Mkataba na DP World ambao Hawa ni foreign investor na sio Serikali ya UAE .

Makubaliano ya kimikataba ya Nchi na Foreign investors (HGA) juu ya project inayokwenda kua implemented Huwa ni LAZIMA YAWE YALE YANAYOMLINDA MUWEKEZAJI KIUCHUMI NA KISIASA BILA KUJALISHA MABADILIKO YOYOTE YA KISHERIA YA NCHI HUSIKA.

ndio Sababu Hiki kilichojadiliwa na Bunge na Watanzania mwanzo mwisho ,kinaonyesha namna gan DP world wamepewa mamlaka Kubwaaaa sana kuliko hata Nchi husika ,na hii ndio HGA yenyewe , yaan hata kama Mahusiano ya kidplomasia yakivunjika, Bado DP world wataendelea kunufaika !!.

Sasa mnapojaribu kuwaambia watanzania kua óhooo hizo ni IGA óhooo Hazina shida , Kwakweli, Tafuteni watanzania wajinga wajinga ndio muwadanganye.

Nadhani Kuna haja kubwa ya kutumia Kalamu na Umaarufu kusimamia katika Ile kweli !!.

Kwamba watanzania Mmoja Mmoja, Taasisi mbalimbali na vyama mbalimbali, Kulalamikia hii kitu, kwamba wote hao ni wajinga, Et Pasko Mayala ndio mwenye akili na genge lake ??.

HAPANA !!.
Serikali haijaingia HGA hata moja kabla ya IGA kupata baraka za Bunge. Kwa sababu wigo wa IGA ni mpana kuliko bandari, HGA zinaweza kuwa nyingi tu na si lazima ziwe wazi.

Amandla...
 
Halafu hiyo IGA inasema wazi kwamba HGA zinapaswa kufuata masharti yaliyoko kwenye IGA.

HGA ni mkataba wa kuwezesha utekelezaji wa IGA na sio mkataba wa kufanya mabadiliko ya IGA.

HGA na IGA hazipaswi kwenda kinyume kwa kadiri ya masharti yaliyowekwa kwenye IGA. Kwahiyo hizi ahadi za kutuambia ati tusubiri mabadiliko kwenye HGA ni ahadi za urongo ambazo haziwezekani kisheria.

Hapa tuseme tu kwamba SAMIA KABORONGA.

Njia iliyopo ni KUFUTA IGA na MoUs zote waanze upya au waachane kabisa na huo mpango.

Na nikiuangalia huu mkataba wa IGA unaonesha kabisa haujaandaliwa na WANASHERIA, umeandaliwa chumbani na watu wenye NIA OVU.
Ndicho kilichopo , DP World Kwa werevu mkubwa na uwezo na uzoefu mkubwa wa haya mambo, WAMETUNUNUA.

Hiyo Pasko anayoita IGA, kiuhalisia ni HGA !!.
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya leo.

View attachment 2661201View attachment 2661204
Kama kawaida yangu, kila nipotapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" zinazozungumzia jambo lolote lenye maslahi kwa taifa, liwe ni la kisiasa, kiuchumi au kijamii, na hufanywa kwa mtindo wa maswali fikirishi, kisha hukuwekea hoja zangu elimishi, na kukuachia fursa wewe, utoe majibu yako.

Leo naendelea na mada ya wiki iliyopita kuhusu makubaliano ya kiserikali, IGA ambapo Bunge letu limeridhia makubaliano ya IGA kati ya Serikali yetu na kampuni ya DPW ya Dubai, kutuendeshea Bandari ombalo ni jambo zuri, lakini bado kuna kelele nyingi za huku na kule, kelele nyingine ni kelele za kijinga tuu kwa watu kutokujua, IGA ni nini, na HGA ni nini, hivyo swali la leo ni "Hili la Mkataba na kampuni ya DPW kutuendeshea bandari zetu, hizi kelele, kulalamika, shutuma, na lawama ni za kweli?, are they justified?, au ni kelele tuu za ujinga tuu wa kutojua sheria na mikataba?. Mhusika mkuu wa kelele hizi, kulalamikiwa huku, shutuma hizi na kutwishwa lawama ni Rais Samia!, Je Rais Samia, anastahili kulaumiwa au kupongezwa?.

Kiukweli jambo hili la DPW na serikali yetu, limefika hapa lilipofika kwa udhaifu tuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini kushindwa kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kutokuwa proactive na badala yake kinakuwa reactive when the cat is already out of basket!, sina uhakika kama ni udhaifu wa uongozi, lack of vision, uwezo duni wa communicators wetu kwenye technical issues kama hii ya mikataba, au ni lack of resources kuendesha vipindi vya public information programs kuwaemisha Watanzania.

Sasa kwa vile na mimi mwandishi wako wa makala hizi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, na ninauwezo wa kuelimisha umma, baada ya kuona serikali yetu imeshindwa kwenye hili, uzalendo umenituma kujitokeza kujitolea kuelimisha umma kidogo kuhusu IGA na HGA, kwa kuwasisitiza Watanzania wenzangu, kwanza tupunguze kelele, kupotosha na kulaumu, kwa vitu ambavyo hatuvijui kwa undani.

Kwenye hili la DPW na Bandari, kiukweli kabisa, Rais Samia anastahili pongezi za dhati na sio lawama!, IGA na DPW ni Makubaliano Tuu Sio Mkataba, Mkataba ni HGA!. ila kabla ya kwenda huko tuanze na jambo kuu la kwanza la msingi kabisa ni utendaji wa Bandari zetu na uwezo wetu wa uendeshaji, ni mdogo, hivyo tunahitaji usaidizi.

Jambo la pili kubwa na la msingi sana ni nia njema ya dhati na dhamira safi ya Rais wetu Mama Samia, kulisaidia taifa letu kutoka hapa tulipo, tuweze kusonga mbele kimaendeleo, na kufika kule tulikopaswa kuwa. Maadam Mama Samia ana nia njema na dhamira safi, naomba tuendelee kumuunga mkono kwa dhati na kumsupport ili kutimiza nia hiyo.

Ila katika utekelezaji nia njema hiyo, ndipo kwenye matatizo, kuanzia matatizo makubwa ya msingi ya kisheria, hadi matatizo madogo madogo ya uelewa finyu na tafsiri potofu za hapa na pale, ambayo hayamuhusu kabisa Rais Samia, lakini kwa vile mkubwa ni jalala, kila kitu anatupiwa yeye!, wakati matatizo mengine wala hayamhusu kabisa yeye kama Samia, ila kwa vile yeye ndio kichwa cha nchi, ndio nembo yetu, hawezi kukwepa kuhusishwa na kutajwa tajwa mara ni Mzanzibari, mara anauza nchi, mara hivi mara vile, huu ni ujinga mtupu!.

Nichukue fursa hii kuendelea kumpongeza rais wetu Mama Samia, kwa kuendelea kuwa na ngozi ngumu!, maana kuna vitu vinasemwa, ikijiuliza kama angekuwa ni Magufuli, vingesemwa?. Hata huo mkataba wa IGA, tungeuona?, hata huko Bungeni ungepelekwa?. Mnyonge tumnyongeni jamani, haki yake mpeni!, kwenye hili la kupeleka mkataba huu wa IGA kuridhiwa na Bunge, ni jambo jema linalo stahili pongezi za dhati.

Sasa tuje kwenye hili la IGA na HGA. Hapa Watanzania wanahitaji kuelimishwa hii IGA ni nini na HGA ni nini ? kazi ambayo ingefanywa kikamilifu na kitengo cha mawasiliano serikalini, tusingefika hapa tulipofika!.

IGA ni neno la Kiingereza linaloitwa Inter Governmental Agreement, IGA ni makubaliano kati ya nchi na nchi sio mkataba wa contract, ni mkataba wa makubaliano, ambao kwa kiingereza unaitwa MoU, (memorandum of understanding) kati ya serikali yetu na serikali ya Dubai kuingia mkataba wa kimataifa wa ushirikiano. Mkataba wenyewe wa ushirikiano ndio unaitwa HGA yaani Host Government Agreement, huu ndio mkataba. Kila mkataba ni makubaliano ila sio kila makubaliano ni mkataba.

Kitu kilichojadiliwa na kuridhiwa na Bunge letu ni IGA na sio HGA, hivyo hata ikithibitika pasipo shaka kuwa kuna mambo bado hayajakaa sawa kwenye makubaliano hayo ya IGA, mambo hayo yatarekebishwa kabla ya kuingia mkataba wa HGA na serikali yetu, hivyo Tanzania kufaidika kwa kuboreshewa Bandari zetu, na mwekezaji DPW kufaidika kwa kuvuna mapato halali kwa uwekezaji wake hivyo wote wawili kufaidika kwa kufikia hali inayoitwa a win win situation na Tanzania kama nchi nchi kufaidika.

Japo serikali yetu ina watendaji wazuri wa kusimamia maslahi ya taifa, lakini huku nje mitaani kuna kuwa watu wazuri tuu wenye uwezo mkubwa tuu wa kuisaidia nchi yetu na serikali yetu pengine kuliko hata hao waliopo serikalini, hoja za watu hawa zisikilizwe na kutathminiwa kama zina mashiko na manufaa zijumuishwe ili tupate mkataba mzuri wa HGA.

Hivyo naomba kutoa wito, kila Mtanzania mwenye uelewa na ushauri mzuri wa kusaidia, ajitokeze, atoe ushauri, wa namna bora ya kuiboresha HGA inayokuja na kuiomba serikali yetu iwe sikivu kupokea michango chanya, tutaisaidia sana serikali yetu, tutamsaidia sana Rais wetu Samia na kulisaidia taifa letu Tanzania.

Naendelea kusisitiza Rais wetu, Mama Samia, ana nia njema ya kweli na ya dhati kulisaidia taifa letu, tumuunge mkono tukiwemo sisi watu wa Mhimili wa Nne, the media, tuna wajibu wa kulisaidia taifa letu kwa kuhabarisha taarifa sahihi na kuelimisha maeneo yenye ukakasi kwenye hii IGA ili hivyo vipengele kakasi vya IGA viboreshwe kwenye HGA ili hii kazi nzuri ya Mama Samia iendelee!.

Kwa upande wangu mimi kama nilivyosema, licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, kwa kujitolea kutetea bure haki kwa wasio na uwezo, hivyo wiki ijayo nitawachambulia hii IGA kisheria kwa kuwaonyeshea maeneo yenye ukakasi wa kisheria.

Kwa vile Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu na kulisaidia taifa letu kama makala hizi zinachofanya na huu ndio uzalendo wa kweli wa mtu kwa taifa lake.

Wasalaam

Paskali.
Ila mkuu,yule boss wa TPA alisema tulichoingia na Dubai(ambayo sio nchi),ni IGA,ambayo kwa maneno yake ni "regal binding"tukivunja tunashitakiwa,na hatukuingia MOU,kama unavyodai,
Mpaka Sasa tupo ndani ya mkataba,ambao tukivunja,tunashitakiwa!!na IGA sio MOU,MOU ni makubaliano ya kiungwana,sio regal binding,unaweza ukaachana nayo ukijisikia,ni sawa na kupiga chini mchepuko,usio toa huduma Bora,
 
La bandari walalamikaje wengi ni wale waliokuwa wanatumia bandari yetu kupitisha magendo yao ikiwemo madawa ya kulevya, waliokwepa kulipa kodi, waliokuwa wanapiga madili kwa kuiba vifaa vya magari yaliopo bandarini na vitu vingine vilivyopo hapo.

Unakuta mtu anaagiza mzigo China afu ukifika hapo unatolewa kupitia gate la uwani na baadae mtoaji anapozwa huko mtaani na mwenye mzigo afu serikali inakosa mapato.

Hii naifananisha na mfanyakazi anaekuibia dukani kwako afu ukileta mtu mungine asimamie pesa za mauzo, mfanye kazi huyo aingie mtaani na kuanza kulalamika na kukuchafua kisa umezuia wizi wake aliokuwa anautumia kujineemesha kupitia duka lako.

Wengine ni wale nyumbu na misukule ya wanasiasa fulan wanaotumiwa kwa sababu mbali mbali zikiwemo za kisiasa, huku wanasiasa hao wakiwa wameshahongwa na wale wanaonufaika na mfumo mbovu wa bandari uliyopo nk.

Nashauri raisi asilegeze kamba, maana itakuwa ni sawa na kumpa ushindi adui anaepanga kukuangamiza kupitia gharama zako mwenyewe.

Vita vya panzi furaha kwa kunguru. Hii vita inampa furaha Mkenya ambae anatamani Tanzania iendelee kuwa na mfumo huu huu mbovu ili bandari yao ya Mombasa iendelee kuonekana bora katika ukanda mzima wa Africa Mashariki.
Samia ni msaliti katutoa sadaka kwa mwarabu.
 
Haha Asante, nimekunywa. Ongea na Kaka yako Pascal amelewa kuwa katikati ya wenye nchi.

Kazi yake ni ku- spin stuffs vionekane more palatable to the public.

Hatuwezi jua labda kuna bahasha kaki kasogezewa maana anatumia gharama kubwa sana kuandika nakala zake didhani kama anatoa hela yake mfukoni
 
Kichwa cha habari..
" TUPUUZE"
Inatupa ujumbe tosha kuwa hufai kuaminiwa na makala ni batili.

Ungetoa hoja ili watu wachague kupuuzia hizo kelele au waendelee.

Pascal Mayalla ...umasikini na ukweli havikai pamoja.

Msimamo na njaa ni maadui.

Umasikini na ukweli ni maadui.

Acha njaa za kijinga, simania haki acha upotoshaji.

Alichofanya Sa100 ni Loliondo part2 tena hii ni mbaya kuliko Loliondo ya Mwinyi.
Hakika.
 
Hatuwezi jua labda kuna bahasha kaki kasogezewa maana anatumia gharama kubwa sana kuandika nakala zake didhani kama anatoa hela yake mfukoni

Ni kazi yake, ndio inamuweka mjini. Kuitetea CCM hata ikifanya uovu gani.

Vyovyote Pascal avyoviita IGA, HGA, MoU, dili, haya ni makubaliano / mkabata semantics stuffs. Kwa namna yoyote Ile ukiyaaangalia ni upuuzi.

USA,UK, China nchi yoyote inayojitambua haingekubali au kupewa dili la hovyo kama hili.

Wangemuhoji Rais vipengele vyote muhimu. Akizingua anaondolewa labda na kushtakiwa. Asingeruhusiwa kupuuza, kujificha.

Ila waandishi wetu nguli kama Pascal wanatetea upuuzi. Badala ya kuhoji, kufanya opposite. Inasikitisha.
 
Back
Top Bottom