DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

R.I.P Magufuli ulisema Tanzania ni tajiri na ukatuonyesha kwa vitendo baada ya kuanzisha miradi mikubwa barani Afrika, viongozi uliowaacha hawaamini kama Tanzania ni tajiri wanaamini katika kuombaomba.
Miradi gani? Zaidi ya kudumaza Uchumi? Miaka 6 yupo Madarakani uchumi haujakua hata asilimia 10%
 
Mbona huwa unatoa hoja za kiuoga oga wewe.
Tiririka mwanangu acha uoga wa kujipendekeza Kama Yule rafiki yako anayeitwa Lukas Mwashamba.
 
Kumbe Kweli Bunge halijaidhinisha Azimio la serikali?

Hii alama ya kuuliza ni ulinzi.
 
R.I.P Magufuli ulisema Tanzania ni tajiri na ukatuonyesha kwa vitendo baada ya kuanzisha miradi mikubwa barani Afrika, viongozi uliowaacha hawaamini kama Tanzania ni tajiri wanaamini katika kuombaomba.
Kwanza niko upande wa wanao pinga uuzaji bandari ila ulicho andika hapa sio sahihi.. kwani miradi mikubwa ela si tulikopa?
 
Uzi wako hapa ni swali kule umepeleka conclusion ?

Unataka tujadili swali lako au tukubaliane na conclusion yako ?

Sababu heading ya Gazeti nimeona kama umesema anastahili Pongezi....

Anyway binafsi huwa sina muda wa kupongezana kama mtu akifanya vyema ni kazi yake akikosea anastahili kuwa criticized after all hio kazi hakulazimishwa hata akiamua kuondoka sasa hivi kuna wengi wanaitaka....

Nadhani na wewe ungelisaidia taifa ukiwa more of a critic rather than a cheerleader... / Muunga mkono Hoja
 
Bado anafanya uteuzi vuta subira Paskali.
 
Ahsante sana kwa wasilisho zuri sana, big up. Asiyetaka kuelewa huwezi kumlazimisha. Ni kweli ingekuwa JPM wangesikia tu DP World inaendesha bandari na hakuna ambaye angenyanyua ulimi wake. Tumshukuru Mungu tuna mtu sahihi kwa wakati sahihi. Mi sikumbuki km mambo ya SGR, daraja la Kigongo-Busisi, Chato international Airport na mengine km hayo yalipelekwa bungeni. Rais Samia ametoa uhuru wa vyombo vya habari badala tuutumie vizuri tunautumia vibaya tena bila aibu kumtukana aliyetutunuku huyu ambao ulishaporwa kabla. Kwlei watanzania ni km punda tu, shukrani zetu ni mateke. Tunaye rais mzuri sana tumheshimu, tumsikilize, tutoe ushauri kwa staha. Rais ni rais anatumia katiba ile ile alokuwa anatumia JPM, Madaraka ya rais wetu ni makubwa sana tusimchokoze sana kupitiliza.
 
Samia ni msaliti katutoa sadaka kwa mwarabu.
Kwa bahati nzuri hizi propaganda zenu zitashindwa kama zilivyoshindwa zile za wakenya wa Loliondo, waliokuwa wanaitumia ardhi yetu kulishia mifugo yao, kulimia nk kwa kigezo cha kuuvaa umasai wa mchongo.

Wezi, wapiga madili, wauza spea za magari ya watu pale bandarini, wakwepa kodi na wapitisha madawa ya kulevya ambao walishindwa kujenga kupitia mfumo butu uliyokuwepo miaka yote pale bandarini ndo basi tena.

Hata wakijificha katika kimvuli cha kuwahusisha waarab haitosaidia kitu, maana raisi wetu anafahamu fika kwamba akicheka na nyani ataishia kuvuna mabua.

Hii vita ya kupambana na watu wanaonufaika na mfumo mbovu wa bandari yetu, ni sawa sawa na ile vita ya wauza madawa ya kulevya na mateja wao aliyopigana nayo hayati Magufuli, hadi kupelekea wanasiasa uchwara kuwa upande wa wauza madawa ili kupewa vijipesa vya kula na kujizolea kundi la mateja kadhaa katika vyama vyao.

Na bado hilo halikuweza kuwasaidia kitu walengwa.
 
Hii ni point muhimu. Hawataki kujibu point muhimu. Issue sio kukataa uwekezaji, kwamba ni waarabu, Rais ni Mzanzibari, Mwanamke, Muislamu. Hizo ni mbinu mbovu ya kuwagawanya Watanzania.

Issue ni vipengele, masharti ya mkataba.

Wamewekewa karatasi wakasaini baada ya kualikwa na kutembezwa Dubai, na vitu vingine. Hata wazungu, Wachina wangepingwa kwa mkataba mbovu kama huu. Mwanasheria na Mwanahabari nguli anautetea.

Wote tunahitaji wawekezaji kama nchi yoyote duniani. Lakini kwa win - win situation.

Uwazi, uwajibikaji, ukweli, uzalendo utatuweka huru na kusaidia.
 
HUU UPEPO UTAPITA TU ,NA MAISHA YATAENDELEA
KIKUBWA BANDARI IFANYE KAZI KIUFANISI ZAIDI,HAYO MAMBO MENGINE SISI HAYATUHUSU

Maana TPA na wengineo hapo wamekuwa wakifanya kazi kizembe,uwizi,kujuana tu

Ova
 

Mkataba wa hovyo kama huu. Ukipewa usaini kuuza nyumba yako utaona uko sahihi!

Anayenunua anakupa masharti, vipengele vyote wewe umekaa pale unacheka, unasaini!

kuuza nyumba, nchi yako ndio unaona uko sahihi sana?
 
Serikali imeshindwa vp kuwawajibisha hao wenye hiyo unayoita mirija?
Kwamaana hiyo unakiri kuwa Serikali yetu imeshindwa kutuongoza yenyewe ndio inahitaji kubinafsishwa?
 

Huyo ni mjinga mmoja fulani hivi.
 
Serikali imeshindwa vp kuwawajibisha hao wenye hiyo unayoita mirija?
Kwamaana hiyo unakiri kuwa Serikali yetu imeshindwa kutuongoza yenyewe ndio inahitaji kubinafsishwa?
Nyerere alishindwaje? Alijenga kila kitu kwa jasho na damu vilikufaje? Maana alipaswa kuwa mwenye hasira kali zaidi, UNAPIKUWA POSITIVE, NA MAZINGIRA YOTE YAKAWA NEGATIVE, WORK DONE HUWA ZERO HATA UWE NA JUHUDI GANI.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Hii nchi ukiwa mgeni ni rahisi kufikiri kwamba hao DP World watakuwa msaada sana hapo bandarini ila kimsingi kwa ambao tuna uzoefu na shuhuda za mambo yanayotokeaga ni kwamba hapo itakuwa ni mfumo wa kubadilisha walaji tu.
Yani kundi lililokuwa linanufaika linaporwa tonge wanaingia wengine kula keki kupitia mkataba na DP World. Nina hakika bila huo mkataba kuvuja hii ishu ingepigwa kimya kimya tu ni kwamba kuna mtu hakupewa mgao wake akachomesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…