DP World inatisha 2: Tazama bandari inazozihudumia Uingereza

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
DP World wameunda biashara iliyounganishwa kwa ubora wa hali juu - bandari mbili za kina kirefu zenye vituo vya reli ya mizigo huko London Gateway na Southampton, kituo cha vifaa (logistics park) inayopanuka kwa kasi na biashara ya juu ya programu za software zinazotoa viunganisho vya mtandaoni kwa wateja na udhibiti wa usalama.

DP World wamewekeza kwenye miundombinu sahihi ya biashara na masuluhisho mahiri ya vifaa kwa wateja wao wsnaotumia bandari hizo. Kila mwaka, DP World kupitia bandari hizo wanasafirisha takriban kontena milioni 3.6 - bidhaa zenye thamani ya £43 bilioni katika kontena hizi husafirishwa kwenda na kutoka nchi zilizo nje ya EU.

DP World wanaamini katika soko la Uingereza wana matarajio na rasilimali za kutosha kuhimili na kuboresha ukuwaji, kusaidia biashara, kuunda nafasi za kazi na kuboresha viwango vya maisha. Utaalam wao wa biashara unaoongoza katika sekta ya bandari, unatambuliwa kwa kutoa ushauri wa kiufundi na wa kimkakati mara kwa mara kwa Serikali ya Uingereza.



Chanzo: DP World in the UK
 
Huu ujinga wa waislam mkiona mwarabu mna m treat kama ndugu yenu sijui utaisha lini
mnamtetea mpaka basi
ungetuwekea mkataba wa huko nchi zenye akili tulinganishe na huu wa kwetu
 
Ninyi mnachekesha sana! Hivi nani amekataa uwekezaji? Kinachopigwa ni mikataba mibovu. Pimbi wakubwa nyie!
Mkataba huu hapa👇🏾 tuoneshe ubovu wake 👇🏾

 
Uzuri nchi inaendeshwa na mfumo kristu.Huu mkataba ukipush through bila marekebisho mniite nyau
 
Ahsante FaizaFoxy kwanza leo umeandika vizuri bila ya kukosea kosea hongera kwa hilo na pia udini umeweka kando. Nakushukuru kwa your support kwa ujio wa DP World na maendeleo ya Tanzania.
 
Waarabu wa Dubai wanatisha.


Mama Samia hujakosea kabisa kuamuwa kuwaleta DP World Tanzania.

Tupo na wewe 100%.
Asaini MKATABA wa milele kabisa Ndoa ya milele na Mwarabu
 
Naomba mtuwekee mkataba wa DP world na uingereza tulimganishe na huu wa Tanganyika
 
Huu ujinga wa waislam mkiona mwarabu mna m treat kama ndugu yenu sijui utaisha lini
mnamtetea mpaka basi
ungetuwekea mkataba wa huko nchi zenye akili tulinganishe na huu wa kwetu
Acha ujinga wewe,ni wapi umetajwa uislamu hapo? kwahiyo na wale wote wanaoipinga DPW nao wanapinga coz DP ni ya waislamu? au umeamua tu kuziweka akili zako kwenye mfuko wa shati? kama unazo hizo akili pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…