Hakuna bandari yoyote wliyiyoewa. Tuoneshe. Huo mkataba wako wa bandari waliyopewa.
Mkstaba uliopo ni wa ushirokianonwa msendeleo ya bandari siyibwa yendeshaji bandari.
Jinsi unavyochangia mada, sina uhakika kama unaielewa tofauti IGA na HGA. Pole sana.
Elimu elimu elimu - kwa sauti ya Lowasa.
Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Mimi naiangalia mikataba tokea awamu ya Mzee Benjamini. Wakina Mwanyika wanaingia mikataba ya hovyo na Acacia mimi nipo. Bilateral Investment Treaties (BIT) zinaangaliwa upya kipindi cha Raisi Magufuli mimi nipo nafuatilia vizuri tu. Mitafaruku inatokea na wawekezaji kama San Lodges Mikindani Estates Mtwara, ndege zinakamatwa kule Afrika Kusini mimi nipo nashuhudia. Tanganyika inapelekwa kwenye mahakama za Uingereza kisa makinikia mimi nipo nashuhudia kwa macho yangu.
Itoshe kusema nimefanya kazi kwenye hizi mahakama za kimataifa ambako sheria za kimataifa zinatumika. Kiufupi INTERNATIONAL ECONOMICS LAW ndiyo uwanja wangu wa nyumbani, na wahenga husema mcheza kwao hutuzwa. Nimesoma na nimefundishwa sheria na wasomi wakubwa hapa nchini na duniani. Wewe BUSH LAWYER utaniambia nini mimi nisichokifahamu ?
Eti mara IGA, mara HGA unadhani unaonekana mwerevu. Kiufupi ni wajinga tu ndiyo wanachekelea wasiyoyafahamu. Sasa hebu nikupashe habari kidogo jinsi ambavyo duniani kote mambo yanafanyika ili uachane na ujinga. Mikataba ya biashara duniani kote, msingi wake hujengwa kwenye kitu kiitwacho BILATERAL INVESTMENT TREATIES (BIT's) ambazo nchi moja husaini na nchi nyingine ili kuruhusu uwekezaji baina ya raia, mashirika na makampuni ya nchi hizo mbili. Hii mikataba huwa inaweza kusimamiwa na sheria za kimataifa kama zile za World Trade Organization Rules (WTO Rules) au Customary International Law. Wewe mjinga haya unayafahamu ?
Sasa Tanzania ina BITs kama 21 hivi ambazo zinaruhusu uwekezaji nchini. Bahati mbaya sana taifa kama United Araba Emirates (UAE) halijawahi kusaini BIT na Tanzania, hivyo sasa wanafanyaje ili kuweza kuruhusu uwekezaji kwenye nchi zao ? Inabidi wasaini INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT (IGA) ambayo itakuwa na nguvu sana BILATERAL INVESTMENT TREATY. Ndiyo maana ukisoma hiyo IGA baina ya Tanzania na Dubai utaona zile kanuni za kisheria za biashara ambazo ziko kwenye BITs nyingine zimo humohumo ndani ya IGA. Hili nadhani madrasa haujafundishwa, hivyo ngoja nikupashe.
Kanuni za sheria ya biashara ambazo zinatakiwa kuwa ndani ya IGA na BIT ni hizi hapa:
Mosi,
THE RULES AGAINST EXPROPRIATION.
Hapa nchi (Host Government) inakubali kwamba kwa namna yoyote ile haitajaribu kushika au kukamata mali za huyo mwekezaji hata itokee nini. Kwenye hiyo IGA yenu ni IBARA YA 14. Hii kanuni ndiyo ilitumika na ACACIA, SUN LODGES kuiburuza Tanzania kwenye mahakama za kimataifa kipindi cha Raisi Magufuli.
Pili, THE RULES AGAINST DISCRIMINATION.
Hapa nchi (Host Government) inakubali kwamba kwa namna yoyote ile haitabagua wawekezaji wa nchi inayowekeza endapo watakuja kuwekeza kwenye nchi. Kwenye hiyo IGA yenu ni IBARA YA 11. Hivyo basi Tanganyika haitatakiwa kuwabagua waarabu wa DP World ambao watakuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya bandari kupitia HGAs au PROJECT AGREEMENTS.
Tatu, THE MOST FAVOURED NATION
Hapa nchi (Host Government) inakubali kwamba kwasababu imesaini makubaliano na mwekezaji, basi wawekezaji watakapokuja watapewa huduma za haraka kuliko raia wa mataifa mengine ambayo hayajasaini nayo IGA au BIT. Kwenye ile IGA yenu IBARA ZA 11 na 5 zinasema hiki kitu. Kama unakumbuka vizuri, Al Hajj Aliko Dangote alipata shida sana kwenye viwanda vyake kwasababu hii kanuni ilivunja kutokana na ukweli kwamba Tanzania na Nigeria hatuna BIT wala IGA.
Naamani haya kwaleo yanakutosha, nikikupa mengine sidhani kama utakuwa na kichwa cha kubeba. Sasa tunarudi kwenye HGA, nini maana ya Host Government Agreement ???
HOST GOVERNMENT AGREEMENT, ni mkataba wa kulinda uwekezaji husika (Specific Project) ambao unasainiwa baina ya nchi mbili ambazo zimesaini INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT hapo awali. Katika maana nyingine ni kwamba HGA ndiyo mkataba ambao unaanzisha utekelezaji wa miradi ambayo imekusudiwa ndani ya IGA. Hivyo, ili HGA inaanzisha mradi na kuulinda kwa kufuata kanuni ambazo nimezitaja hapo juu.
Kwenye hiyo IGA yenu kama kweli umesoma na kuelewa, maneno mawili yametumika. HGA au PROJECT AGREEMENT, lakini wewe likakupita ukadhani haya ni maneno tofauti au yenye ufundi. Jibu ni hapana, HGA inaweza ikaitwa majina kama PROJECT AGREEMENT au A BUSINESS CONCESSION. Like Notorious BIG once said "If you don't know, now you know"
NB 1: IGA ni baba wa HGA/PROJECTA GREEMENT, hivyo kama hakuna IGA basi hakuna HGA.
NB 2: Mlizani kila mtanzania ni mjinga lakini kipindi hiki yanawatokea puani. Hivi unadhani kwanini watu wenye akili kama Dr Eliezer Mbuki Feleshi ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengine wamenyamaza kimya sana kipindi hiki. Mama yenu katengenezewa ajali ya kisiasa na akanasa mazima. Hichi alichokifanya ni UHAINI (High Treason) na tutaenda naye mpaka mwisho.
NB 3: Huu mkataba (IGA) una majina matatu ya Wazanzibar ambao Samia (Raisi), Mbarawa (Waziri) na Aisha (Katibu Mkuu). Majina mengine hapo kiutaratibu hayakutakiwa kuwepo kwasababu za kimamlaka. Mkataba mkubwa kama huu alitakiwa awepo Dr Mbuki Feleshi na Mkurugenzi wa Bandari.
BITs nyingine zina majina kama Nyerere (Raisi) au Mkapa (Raisi), Chenge (Mwanasheria Mkuu) au Mwanyika (Mwanasheria Mkuu), na kiongozi mwingine mwenye dhamana. Huoni kama kuna walakini hapo ??? Kilichomponza Lowassa, Karamagi na Msabaha kwenye RICHMOND ni kusaini mikataba ambayo hakuwa na mamlaka nayo hivyo wakaingia QIBRA wahuni wakashusha kisu.
Bwahahahaa, mama yenu kaingia QIBRA. Wewe usiyeelewa utaniambia nini mimi ????