Waarabu wa Dubai wanatisha.
Mama Samia hujakosea kabisa kuamuwa kuwaleta DP World Tanzania.
Tupo na wewe 100%.
Hivi mkuu, mijadala yote iliyofumuka kitaifa ihusuyo masharti mabovu ya mkataba wa muwekezaji, wewe haujasikia?
Na kama umesikia, kuna mtu yeyote kasema uwekezaji kutoka Uarabuni haufai au kinachopigiwa kelele na raia ni masharti ya hovyo yaliyomo kwenye mkataba?
Kuwa DpW wapo Uingereza na kwingine kwenye uwekezaji wa namna hiyo, si uhalali wa kututwisha sisi mikataba masalia ya kuumiza nchi.
Waziri mkuu mwenyewe keshasema, wapo raia wenye mashaka nao na hawastahili kubezwa.
Na mashaka hayo yanatokana na mikataba mingine ya kifisadi huko nyuma iliyoingiwa na kuridhiwa na nchi ambayo kila mtu mzima anafahamu.
Yawezekana Rais alikuwa na nia njema kufikiria jambo hilo, lakini ni namna gani utekekezaji wake ulivyoanzwa, ndiyo kitendawili na kizungumkuti kinachochanganya wananch!
Umeshamsikia Mbunge wa Nkansi aitwaye Kishoa kwa umakini na ukamuelewa?
Sasa, kati kati ya mijadala mizito namna hii ambayo haijapata muafaka wa kitaifa, halafu wewe unaanzisha mada ya kujiweka upande unaotiliwa shaka na kuitwa majina mabaya ya uchawa, wewe unaona fahari?
Nadhani haikustahili kwa mtu kama wewe unayeonekana humu Jf kama ni mwenye akili kubwa kuanzisha mada kama hii kwa sasa ambayo itakushushia tu heshima.
Ujue jambo hili hili tayari limeshatugawa waTz.
Na litakapofikia muafaka jambo hili, kuna baadhi ya watu wenye majina yenye kuheshemika, ambao hoja hii itawatweza na kudharaulika na jamii kutokana na kuunga kwao mkono hoja mbovu za kifisadi zisizofanyiwa na zinazoendelea kfanyiwa utafiti kabla ya kupata muafaka wa Umma.