DP World inatisha 2: Tazama bandari inazozihudumia Uingereza

DP World inatisha 2: Tazama bandari inazozihudumia Uingereza

Mimi naiangalia mikataba tokea awamu ya Mzee Benjamini. Wakina Mwanyika wanaingia mikataba ya hovyo na Acacia mimi nipo. Bilateral Investment Treaties (BIT) zinaangaliwa upya kipindi cha Raisi Magufuli mimi nipo nafuatilia vizuri tu. Mitafaruku inatokea na wawekezaji kama San Lodges Mikindani Estates Mtwara, ndege zinakamatwa kule Afrika Kusini mimi

Waache washangilie, asante kwa kuchambua vizuri sana na wewe ulisoma ukaelewa hawa washangiliaji wengi walienda shule kucheza na kutembea tu ndio maana akili za wehu kama akina musukuma nazo wanazotegemea
 
Kwanza hichi unachokisema ni kwa pande zote mbili, hata wao hawawezi kuvunja jwankuamua tu au kwa kuwa labda kwao wameopinduana

Mkataba nu wa pande mbili (it takes two to tango).

Au wewe ulitaka Waarabu wawekeze pesa zao halafu uwaambie hutaki nkataba? Na bandari ipo kwako?

Usiwe kioja. Unataka kuwatapeli? Usifikiri Waarabu wajinga?

Ukitaka kuvunja mkataba kuna vigezo vyake kwenye mkataba. simpo. Jisomee kipengele cha 20 moaka 23 vipo wazi kabisa.

Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Pande moja inapo kiuka wajibu wake ndio kigezo kikuu cha mkataba kuvunjika. Hata wewe hapo ulipo kama umeolewa, Je mme wako akianza kuleta malaya wenye uti hapo kwenu, yeye akikataa kupokea talaka yako utabaki kwenye ndoa na kushiriki tendo kisa yeye ni lazima akubali kwa hiari yake ndio uondoke ?

Kuwa muelewa, huo ni mkataba wa milele, Hakuna kifungu chochote ambacho kimeweka muda wa mkataba kukoma
 
Wewe ni mtumwa ktk Nchi Yako,

Kwann kupoteza muda kusifia mume wa Jirani kuwa ana pesa na uwezo kumzidi mumeo?

Ktk NDOA hiyo role Yako ni ipi?

Acha uongo na unafiki, Lete mawazo chanya ya kuongeza uwezo wa ndani wa Watanzania wenzetu kuendesha Bandari Kwa kiwango Bora Cha kidunia.
Naona hoja za bandari zimekushinda umeanza kuhororoja, kubwabwaja na kubweka bila mpango.


Kwa kutumia lugha yako, Uingereza siyo jirani yetu. Jirani zetu ni wanaotuzunguka. Ususahau hilo.


Tunaisikfia DP World kwa kuwa tumepeleka posa tuoane nao. Sasa Wajomba lazima tuwasifie sifie msiipingepinge ndoa ingawa wajomba wenyewe ndiyo mpo vile. Kina Deus Soka.

Waarabu wanasema "mjomba ni mzazi hata kama ni kiazi cha orojo".

Utajaza.mwenyewe mjomba.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Mkataba wa Uingereza ni wa kuendesha bandari baina ya DP World na "Associated British Ports" ya Uingereza ninwa kibiashara, mikataba ya kibiashara huwa ni siri za kibiashara baina ya pande mbili.


Mkataba unaouona unaongelewa Tanzania hivi sasa ni IGA baina ya serikali ya Dubai na Serikali ya Tanzania. Ni vitu viwili tofauti.

Tutapokuwa na nkataba wa kibiashara baina ya DP World na TPA pia utakuwa tofauti sana na huu tuuonao sasa.



Mama anaupiga mwingi Kimataifa.

Dubai sio nchi, ilitakiwa iwe UAE, dubai ni state ndani ya UAE hivo serikali inaingia mkataba na state ajabu sana
 
Mimi naiangalia mikataba tokea awamu ya Mzee Benjamini. Wakina Mwanyika wanaingia mikataba ya hovyo na Acacia mimi nipo. Bilateral Investment Treaties (BIT) zinaangaliwa upya kipindi cha Raisi Magufuli mimi nipo nafuatilia vizuri tu. Mitafaruku inatokea na wawekezaji kama San Lodges Mikindani Estates Mtwara, ndege zinakamatwa kule Afrika Kusini mimi nipo nashuhudia. Tanganyika inapelekwa kwenye mahakama za Uingereza kisa makinikia mimi nipo nashuhudia kwa macho yangu.

Itoshe kusema nimefanya kazi kwenye hizi mahakama za kimataifa ambako sheria za kimataifa zinatumika. Kiufupi INTERNATIONAL ECONOMICS LAW ndiyo uwanja wangu wa nyumbani, na wahenga husema mcheza kwao hutuzwa. Nimesoma na nimefundishwa sheria na wasomi wakubwa hapa nchini na duniani. Wewe uliyesomea kidigrii chako cha sheria huko madrasa na utaniambia nini mimi nisichokifahamu ?

Eti mara IGA, mara HGA unadhani unaonekana mwerevu. Kiufupi ni wajinga tu ndiyo wanachekelea wasiyoyafahamu. Sasa hebu nikupashe habari kidogo jinsi ambavyo duniani kote mambo yanafanyika ili uachane na ujinga. Mikataba ya biashara duniani kote, msingi wake hujengwa kwenye kitu kiitwacho BILATERAL INVESTMENT TREATIES (BIT's) ambazo nchi moja husaini na nchi nyingine ili kuruhusu uwekezaji baina ya raia, mashirika na makampuni ya nchi hizo mbili. Hii mikataba huwa inaweza kusimamiwa na sheria za kimataifa kama zile za World Trade Organization Rules (WTO Rules) au Customary International Law. Haya wewe mjinga wa madrasa unayafahamu ?

Sasa Tanzania ina BITs kama 21 hivi ambazo zinaruhusu uwekezaji nchini. Bahati mbaya sana taifa kama United Araba Emirates (UAE) halijawahi kusaini BIT na Tanzania, hivyo sasa wanafanyaje ili kuweza kuruhusu uwekezaji kwenye nchi zao ? Inabidi wasaini INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT (IGA) ambayo itakuwa na nguvu sana BILATERAL INVESTMENT TREATY. Ndiyo maana ukisoma hiyo IGA baina ya Tanzania na Dubai utaona zile kanuni za kisheria za biashara ambazo ziko kwenye BITs nyingine zimo humohumo ndani ya IGA. Hili nadhani madrasa haujafundishwa, hivyo ngoja nikupashe.

Kanuni za sheria ya biashara ambazo zinatakiwa kuwa ndani ya IGA na BIT ni hizi hapa:

Mosi
, THE RULES AGAINST EXPROPRIATION.
Hapa nchi (Host Government) inakubali kwamba kwa namna yoyote ile haitajaribu kushika au kukamata mali za huyo mwekezaji hata itokee nini. Kwenye hiyo IGA yenu ni IBARA YA 14. Hii kanuni ndiyo ilitumika na ACACIA, SUN LODGES kuiburuza Tanzania kwenye mahakama za kimataifa kipindi cha Raisi Magufuli.

Pili, THE RULES AGAINST DISCRIMINATION.
Hapa nchi (Host Government) inakubali kwamba kwa namna yoyote ile haitabagua wawekezaji wa nchi inayowekeza endapo watakuja kuwekeza kwenye nchi. Kwenye hiyo IGA yenu ni IBARA YA 11. Hivyo basi Tanganyika haitatakiwa kuwabagua waarabu wa DP World ambao watakuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya bandari kupitia HGAs au PROJECT AGREEMENTS.

Tatu, THE MOST FAVOURED NATION
Hapa nchi (Host Government) inakubali kwamba kwasababu imesaini makubaliano na mwekezaji, basi wawekezaji watakapokuja watapewa huduma za haraka kuliko raia wa mataifa mengine ambayo hayajasaini nayo IGA au BIT. Kwenye ile IGA yenu IBARA ZA 11 na 5 zinasema hiki kitu. Kama unakumbuka vizuri, Al Hajj Aliko Dangote alipata shida sana kwenye viwanda vyake kwasababu hii kanuni ilivunja kutokana na ukweli kwamba Tanzania na Nigeria hatuna BIT wala IGA.

Naamani haya kwaleo yanakutosha, nikikupa mengine sidhani kama utakuwa na kichwa cha kubeba. Sasa tunarudi kwenye HGA, nini maana ya Host Government Agreement ???

HOST GOVERNMENT AGREEMENT, ni mkataba wa kulinda uwekezaji husika (Specific Project) ambao unasainiwa baina ya nchi mbili ambazo zimesaini INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT hapo awali. Katika maana nyingine ni kwamba HGA ndiyo mkataba ambao unaanzisha utekelezaji wa miradi ambayo imekusudiwa ndani ya IGA. Hivyo, ili HGA inaanzisha mradi na kuulinda kwa kufuata kanuni ambazo nimezitaja hapo juu.

Kwenye hiyo IGA yenu kama kweli umesoma na kuelewa, maneno mawili yametumika. HGA au PROJECT AGREEMENT, lakini wewe likakupita ukadhani haya ni maneno tofauti au yenye ufundi. Jibu ni hapana, HGA inaweza ikaitwa majina kama PROJECT AGREEMENT au A BUSINESS CONCESSION. Like Notorious BIG once said "If you don't know, now you know"

NB 1: IGA ni baba wa HGA/PROJECTA GREEMENT, hivyo kama hakuna IGA basi hakuna HGA.

NB 2: Mlizani kila mtanzania ni mjinga lakini kipindi hiki yanawatokea puani. Hivi unadhani kwanini watu wenye akili kama Dr Eliezer Mbuki Feleshi ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengine wamenyamaza kimya sana kipindi hiki. Mama yenu katengenezewa ajali ya kisiasa na akanasa mazima. Hichi alichokifanya ni UHAINI (High Treason) na tutaenda naye mpaka mwisho.

NB 3: Huu mkataba (IGA) una majina matatu ya Wazanzibar ambao Samia (Raisi), Mbarawa (Waziri) na Aisha (Katibu Mkuu). Majina mengine hapo kiutaratibu hayakutakiwa kuwepo kwasababu za kimamlaka. Mkataba mkubwa kama huu alitakiwa awepo Dr Mbuki Feleshi na Mkurugenzi wa Bandari.

BITs nyingine zina majina kama Nyerere (Raisi) au Mkapa (Raisi), Chenge (Mwanasheria Mkuu) au Mwanyika (Mwanasheria Mkuu), na kiongozi mwingine mwenye dhamana. Huoni kama kuna walakini hapo ??? Kilichomponza Lowassa, Karamagi na Msabaha kwenye RICHMOND ni kusaini mikataba ambayo hakuwa na mamlaka nayo hivyo wakaingia QIBRA wahuni wakashusha kisu.

Bwahahahaa, mama yenu kaingia QIBRA. Wewe ambaye usiyeelewa utaniambia nini mimi ????
Hakuna tatizo bado hatujasaini HGA.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Hakuna tatizo bado hatujasaini HGA.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.

Tatizo lipo kubwa maana waliojipeleka kujiuza kwenye state ya Dubai wanasema dubai ni nchi shame on them yanaongea tu wakati yameingizwa chaka
 
Fanya kazi tafuta pesa lea familia yako vizuri somesha watoto na uwatengenezee mazingira ya kujiajiri na kujitegemea ayo mambo mengne yanaumiza kichwa tuuu CCM na viongozi wake wameshaamua na ata tukipiga kelele dude litaenda tuu
Cha msingi tafta pesa ata nchi ikiuzwa utahamia msumbiji, rwanda,comoro,ata visiwa vya Caribbean island uko
 
Waarabu wa Dubai wanatisha.


Mama Samia hujakosea kabisa kuamuwa kuwaleta DP World Tanzania.

Tupo na wewe 100%.
Sasa naanza kuamini wewe ni mama samia

Unakuja na thread za kusifu na kuabudu na mapambio mengi kwa mama
 
Hakuna tatizo bado hatujasaini HGA.


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Don't you know that IGA creates obligations among party members ???
Which cave have you crawled from with this bismal understanding ???

Wewe shuleni ulikuwa unafauluje kwa aina hiii ya uelewa ? Vitu vidogo kama hivi vinapitaje juu ya kichwa chako bila kuvielewa! Moja ya kanuni muhimu za INTERNATIONAL COMMERCIAL AGREEMENTS ni BREACH OF LEGITIMATE EXPECTATION. Ikimaanisha kwamba nchi itashitakiwa na wawekezaji, hata kwa hasara ambazo zinategemewa kutokea kwenye uwekezaji (LIKELIHOOD)...

Nakupa mfano hai, ACACIA GOLD MINE walienda kufungua kesi kule London Uingereza, dhidi ya serikali ya Tanzania hata kabla haijakamata makinikia. Wao walienda kufungua kesi kuizua serikali ya Tanzania isiendelee na mikakati yake ambayo ingewaletea hasara. Kule London walisema kile kitendo kimewachafua na kufanya hisa zao zishuke kule LONDON STOCK EXCHANGE. Hivyo kama mwaka huu wa fedha 2023/2024 mwekezaji alitegemea kupata faidi bilioni 100, ila serikali ikaingilia utendaji wake, sheria inaruhusu mwekezaji kufanya makadirio ya faida ambayo angeyapata kutokana na mwelekeo wa masoko ya dunia mwaka huo.

IGA inasema kwamba Tanzania ikishasaini huu mkataba na kupitishwa na bunge la Tanzania (Ratified by the Parliament), Tanzania haitakuwa na nguvu ya kuzuia tena vibali vya utekelezaji wa miradi mbali-mbali kupitia HGA au PROJECT AGREEMENT. Hili limewekwa wazi kwenye Ibara ya 1 (2), Ibara ya 6 na Ibara ya 7. Sasa ukizingatia kwamba tayari huu mkataba umeshakuwa ni sehemu ya sheria za Tanzania, serikali haiwezi kabisa kujitoa. Lakini baya zaidi tukikataa kusaini HGA basi wataenda kutuburuza kwenye mahakama za kimataifa......

Hivi wewe mambo marahisi kama haya unashindwaje kuyaelewa ????

Karl Marx once said "Religion is an opium of the masses"
 
Dubai sio nchi, ilitakiwa iwe UAE, dubai ni state ndani ya UAE hivo serikali inaingia mkataba na state ajabu sana
UAE tunayo mikataba mpaka ya Kidiplomasia. Tuna balozi yetu Abu Dhabi na wanabalozi yao Dar.


Dubai ni nchi iliyopo kwenye muungano wa UAE, (nchi saba) mfano wake ni kama Zanzibar na Tanganyika (nchi mbili) Kuna mambo ya Muungano na kuna mambo hayapo kwenye muubgano. Ushahidi 👇🏾

1687351701609.png
 
UAE tunayo mikataba mpaka ya Kidiplomasia. Tuna balozi yetu Abu Dhabi na wanabalozi yao Dar.


Dubai ni nchi iliyopo kwenye muungano wa UAE, (nchi saba) mfano wake ni kama Zanzibar na Tanganyika (nchi mbili) Kuna mambo ya Muungano na kuna mambo hayapo kwenye muubgano. Ushahidi [emoji1484]

View attachment 2664355

Pale kwenye saini uliona saini wa kiongozi yeyote wa nchi ya Dubai na cheo chake?
 
Sasa naanza kuamini wewe ni mama samia

Unakuja na thread za kusifu na kuabudu na mapambio mengi kwa mama
Koma. Waislaam hatuabudu binadam wala sanamu.


1. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. 1
2. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. 2
3. Hakuzaa wala hakuzaliwa 3
4. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. 4



Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
UAE tunayo mikataba mpaka ya Kidiplomasia. Tuna balozi yetu Abu Dhabi na wanabalozi yao Dar.


Dubai ni nchi iliyopo kwenye muungano wa UAE, (nchi saba) mfano wake ni kama Zanzibar na Tanganyika (nchi mbili) Kuna mambo ya Muungano na kuna mambo hayapo kwenye muubgano. Ushahidi [emoji1484]

View attachment 2664355

Dhamana ya Dubai ni UAE , sasa dhamana ya Tanganyika ni URT, sasa umeona mandate ya UAE kwenye mkataba huo? Jibu hakuna yaani nchi inaingia mkataba na kampuni binafsi, ndio maana kwa kuwafichia aibu tunaona tuwashauri kua iundwe kampuni iwe na share 50/50 na DP world na kampuni hiyo iwe inamikiwa na serikali direct au taasis za serikali ili baadae sasa uwezo ukiongezeka tutamaliza share zote 50 ziwe zetu maana tunakua na uzoefu na hapo tumewashauri hivo baada ya kuona mmechemka sasa kuwafichia aibu kiutu uzima mfanye hivo, sisi sio wajinga, tumesoma na duniani tumekaa na kuzunguka na exposure tunayo ya kutosha haswaa,
 
IBARA YA 23
MUDA NA KUKOMESHA

Kusitishwa kwa Mkataba huu kutakuwa chini ya idhini ya awali ya Nchi Wanachama, idhini hiyo haipaswi kuzuiliwa bila sababu.



Ni kwamba huo mkataba unavunjika tu endapo Serikali ya Tanzania na UAE kwa pamoja wakiridhia, Serikali ya Tanzania pekee haiwezi kuuvunja, Utawahonga kipi waarabu wakubali kwa hiari kuacha kusimamia bandari ?
Kwani serikali ya UAE peke yao wanaweza kuuvunja?
 
Pale kwenye saini uliona saini wa kiongozi yeyote wa nchi ya Dubai na cheo chake?

Tazama na viambatanishi utaona hao waluisaini walipewa idhini na nani.

Hivi unawafanya wanasherua wetu qajinga sana? Wewe ndiye mwenye kuijuwa sheria? Una kipi jwenye elimu ya sheria cha kuwashinda wanasheria wetu?


Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
DP World wameunda biashara iliyounganishwa kwa ubora wa hali juu - bandari mbili za kina kirefu zenye vituo vya reli ya mizigo huko London Gateway na Southampton, kituo cha vifaa (logistics park) inayopanuka kwa kasi na biashara ya juu ya programu za software zinazotoa viunganisho vya mtandaoni kwa wateja na udhibiti wa usalama.

DP World wamewekeza kwenye miundombinu sahihi ya biashara na masuluhisho mahiri ya vifaa kwa wateja wao wsnaotumia bandari hizo. Kila mwaka, DP World kupitia bandari hizo wanasafirisha takriban kontena milioni 3.6 - bidhaa zenye thamani ya £43 bilioni katika kontena hizi husafirishwa kwenda na kutoka nchi zilizo nje ya EU.

DP World wanaamini katika soko la Uingereza wana matarajio na rasilimali za kutosha kuhimili na kuboresha ukuwaji, kusaidia biashara, kuunda nafasi za kazi na kuboresha viwango vya maisha. Utaalam wao wa biashara unaoongoza katika sekta ya bandari, unatambuliwa kwa kutoa ushauri wa kiufundi na wa kimkakati mara kwa mara kwa Serikali ya Uingereza.



Chanzo: DP World in the UK

Wapelekwe Zanziba Sisi Watanganyika hatutakii

Hata kama wanahudumia Dunia nzima.

Sisi watangayika tuachwe hivyo na Bandari yetuuu
 
Back
Top Bottom