Nimesoma kinaga ubaga kifungu/sehemu ya 1 hadi 4 na nimegundua haya.
1. Definition au tafsiri ya neno Tanzania ktk mkataba huu haieleweki, haiko wazi na imekaa kimtego.
2. DP WORLD ni wakala wa serikali na DP WORLD nae atakua na mawakala wake(washirika) ambao watakua ni kama wafadhili. Kumbe hapa DP WORLD anaweza kugawa mradi kwa wengine kwa kigezo cha ufadhili, nae akalipwa, na yy akailipa serikali. Kumbe bandari hii inakwenda kuliwa na wataojiita wafadhili wa DP WORLD, DP WORLD wenyewe na Serikali ya Dubei
3.Ukataba huu utakua ni miendelezo wa mikataba mingine maana mkataba unaruhusu kuingiwa kwa mikataba mingine. Hivyo huu unaweza kurekebishwa ila wazee wa kupokea mirungula na chawa akina kitenge wakitia juhudi kidogo basi mikataba ya hovyo inaweza kuingiwa.
4. Mkataba huu unakwenda kuzikabidhi bandari zooote na fursa za bandari zoote nchini kwa DUBAI na DP WORLD yake maana mkataba unasema fursa zote na zozote za bandari zikionekana basi Serikali ya Tanzania inatakiwa kuitaarifu kwanza Dubai ili ione Kama Kuna haja ya kuchangamkia fursa. Huku ndo kusema bandari zetu tanganyika zimeuzwa kwa Dubai kwa ujinga wa kuingia mikataba ya hovyo.
5. Mwisho, Ndug Samia ni lini alitutangazia kwamba anakwenda Dubai kusaini mikataba ktk mambo ya bandari? Na baada ya kusaini ni lini walitupa taarifa kua wamesaini? toka 2022 hadi leo ndo tunapata taarifa ghafla, je tukisema mkataba umevuja tutakua tumetenda dhambi? Mimi nimwambie mheshimiwa kua nchi hii sio yake na Tanganyika sio ya wazanzibari hivyo watanganyika tunahaki ya kushirikishwa na kutaarifiwa na kusikilizwa ktk kila hatua maana watoto wetu mambo ya kiharibika hapa hawana pa kukimbilia, wala hawatokimbilia Zanzibar maana hata Sasa wazanzibar hawatuhitaji watanganyika ktk ardhi yao. Hatma ya watanganyika ni ya watanganyika wenyewe hvyo tunawajibu wa kukataa ujinga Kama Zanzibar wanavyokataa kwa miaka nenda rudi wakidai bara tunawanyonya. Kivyovyote vile tunahitaji tuione sura ya Tanganyika kwaajili yetu watanganyika.
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app