DP World pekee ndio watakaomnasua Rais Samia ili 'watanganyika' wasimtose!

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
655
Reaction score
1,069
“KUNA HATUA TATU WANAWEZA KUCHUKUA”

Hatua ya kwanza ni kampuni hiyo kukiri kwamba mkataba wao uliandaliwa vibaya, wakubali kuwa umekosewa na kwahiyo kuna vifungu vinatakiwa kurekebishwa. Wasijaribu kumshinikiza Samia wala kumdanganya kwamba anaweza kubadilisha sheria za nchi yetu, ili ziweze kuuruhusu na kuupokea mkataba wao kama ulivyo.

2. Hatua ya pili, DP World ijitenge na waislamu wa Tanzania wanaojifanya kuitetea! Kampuni hiyo iwakane hao waislamu wa kujitolea, iwaambie wazi kwamba DP World siyo kampuni ya dini ni kampuni ya biashara.

3. Waislamu waliojigeuza kuwa watetezi wa DP World, waeleweshwe kwamba hii ni kampuni ya kimataifa ya biashara siyo kampuni ya kiislamu!

Hao watetezi waliojiteua wenyewe wajulishwe kwamba DP World inafanya kazi zake kwa kutumia kanuni za biashara zinazotumiwa na walimwengu wote, kampuni hii haitumii aya za Korani kwenye operesheni zake.

Kwahiyo ikiwezekana Afisa uhusiano wa DP World aje Tanzania, afanye “press conference” ya kusafisha hali ya hewa ili mkataba wao usiendelee kuwafarakanisha Watanzania.

Mojawapo kati ya hayo yanayotakiwa kusafishwa kwa haraka ni hiyo dhana ya kuinasibisha kampuni ya DP World na dini.

DP World inabidi ijiweke mbali na hao waislamu wanaojifanya kuitetea, wengine wamethubutu kuutetea hata mkataba wasiousoma wala wasioujua!

Watu wa aina hii wanaotetea wasichokijua, kiuhalisi wanaichafua Kampuni, wengine wanaichafua zaidi kutokana na historia yao mbaya, waliwahi kuvunja Bucha za nguruwe enzi za utawala wa awamu ya pili ya Alhaji Ally Hassan Mwinyi, tena wakachoma makanisa kwenye utawala wa awamu ya nne wa Rais Kikwete.

DP World haiwezi kutetewa na watu wa aina hiyo wenye historia mbaya, inabidi kampuni hiyo iwaambie wazi hao waislamu, kwamba haiuhitaji kabisa utetezi wao! Kwasababu badala ya kufanya utetezi wanaugeuza kuwa uchafuzi.

DP World iwaeleze wazi hao waislamu kwamba kampuni inao wataalamu wake, wawezao kuitetea vizuri zaidi kuanzia kwenye nyanja ya sheria, biashara, hadi kwenye nyanja ya diplomasia, yaani uhusiano wa kampuni na watu wa mataifa mengine.

DP World ni kampuni iliyojitosheleza, haiwahitaji kabisa hao waislamu wanaojituma wenyewe kuitetea! ikiwa kuna waislamu wenye hamu ya kupambana na Wakristo, ama wapo waliodhamiria kushindana na Maaskofu, basi watafute jukwaa lingine nje ya suala la uwekezaji ambalo ni la kiserikali 100%. Tena wasiitimize hiyo nia yao kwa kutumia mgongo wa DP World ambayo ni asasi ya kiuchumi.

Ni vyema kwenye hiyo “press conference” akaweko pia mwakilishi wa serikali kupigilia msumari, kwamba hata utawala wa Samia hauwahitaji waislamu wawe ndio watetezi wake. Samia akiwa kama Rais wa nchi, anao wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja za kitaalamu, wawezao kutetea mazuri yote ya serikali ambayo imedhamiria kuwafanyia wananchi wake.

Samia akiwa kama Mwenyekiti wa CCM anao wataalamu wake ndani ya chama chake, wawezao kumtetea vyema kisiasa, wawezao kujenga hoja za kisera na hoja za kiutawala, zinazotofautiana kwa mbali kabisa na hisia za kidini.

Kwenye dini inajulikana wapo wenye vipaji vya kuhubiri, ambao kupitia mahubiri yao, wanaweza kuamsha hisia zilizolala za waumini wao. Lakini watu wa aina hiyo hawahitajiki kusimama upande serikali kama mawakili wa utetezi. Hao wakijitumbukiza kuwa upande wa serikali wanazidisha uchafuzi.

Uchaguzi mkuu unakaribia wala hakuna namna yoyote ya kuuepuka, ifikapo 2025 Watanzania watalazimika kumchagua Rais!

Mwelekeo ni kwamba ndani ya CCM hakuna mwenye ujasiri wa kumwambia wazi Samia, kwamba umechafuka mno, huchaguliki, wacha CCM iteuwe mgombea mwingine anayeuzika.

Kutokana na huo utamaduni wa woga na unafiki, walio karibu na Samia watamwambia MAMA gombea tu, utashinda, huku wakijua hatashinda, ila kwa minajili ya kulinda ulaji wao, wamejiaandaa kumtangaza kama Rais kwa kipindi cha pili.

CCM ikiingia kwenye uchaguzi mkuu huku mgombea wake Samia akiwa amechafuka sana, hapo ni wazi ushindi wa CCM utategemea mbinu mbadala.
18. Hizo njia mbadala kama “rigging” ama kumtangaza kibabe kuwa mshindi hata kama atakuwa ameshindwa, ndizo zitaipeleka nchi kwenye machafuko ambayo hayajawahi kutokea tangu Tanganyika ipate uhuru.

Ndio maana sisi sote tunaoitakia mema nchi yetu, tunasema ni vyema Samia akajisafisha, ili walau aingie kwenye uchaguzi akiwa amevikwa haya mawili “kupendwa na kuaminika.” Walio karibu naye wanaweza kumdanganya kwamba MAMA gombea na utashinda, lakini “candidate” anapogombea huku akiwa haaminiki kuna hatari mbili zisizozuilika.

Hatari ya kwanza ni hiyo ya kupoteza ama shindwa, kwamba Samia anaweza kutoswa kuanzia ndani ya chama chake CCM hadi serikalini, kwani hao wakiamua kufanya kweli wanao uwezo wa kumwangusha. Kwasababu wanazijua mbinu zote mbadala, ambazo CCM imezitumia siku zote kujipatia ushindi.

Sijui hao wanaoamua kuchafua hali ya hewa wanatarajia Samia atashinda kwa muujiza gani! Muujiza wa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano?

Hatari ya pili ni hiyo kwamba Samia anaweza kubebwa, kwa nguvu za dola akatangazwa mshindi, lakini nchi isitawalike!

Mungu Ibariki Tanzania
 
Umeandika maelezo marefu yenye mashiko, swali linabaki ni vipi dp wanaweza kuupata ujumbe huu?
 
“KUNA HATUA TATU WANAWEZA KUCHUKUA”

Hatua ya kwanza ni kampuni hiyo kukiri kwamba mkataba wao uliandaliwa vibaya, wakubali kuwa umekosewa na kwahiyo kuna vifungu vinatakiwa kurekebishwa. Wasijaribu kumshinikiza Samia wala kumdanganya kwamba anaweza kubadilisha
Ewe mgalatia usiye na akili ni nani aliye kuroga?
 
Hao watetezi waliojiteua wenyewe wajulishwe kwamba DP World inafanya kazi zake kwa kutumia kanuni za biashara zinazotumiwa na walimwengu wote, kampuni hii haitumii aya za Korani kwenye operesheni zake.
 
Hao watetezi waliojiteua wenyewe wajulishwe kwamba DP World inafanya kazi zake kwa kutumia kanuni za biashara zinazotumiwa na walimwengu wote, kampuni hii haitumii aya za Korani kwenye operesheni zake.
Pia hawatumii Hadithi za Mtume kufanya biashara zao.
Ni wanyonyaji kama wanyonyaji wengine.
Inawezekana walisaini Mkataba Msikitini labda.
 
“KUNA HATUA TATU WANAWEZA KUCHUKUA”

Hatua ya kwanza ni kampuni hiyo kukiri kwamba mkataba wao uliandaliwa vibaya, wakubali kuwa umekosewa na kwahiyo kuna vifungu vinatakiwa kurekebishwa. Wasijaribu kumshinikiza Samia wala kumdanganya kwamba anaweza kubadilisha sheria za nchi yetu, ili ziweze kuuruhusu na kuupokea mkataba wao kama ulivyo.

2. Hatua ya pili, DP World ijitenge na waislamu wa Tanzania wanaojifanya kuitetea! Kampuni hiyo iwakane hao waislamu wa kujitolea, iwaambie wazi kwamba DP World siyo kampuni ya dini ni kampuni ya biashara.

3. Waislamu waliojigeuza kuwa watetezi wa DP World, waeleweshwe kwamba hii ni kampuni ya kimataifa ya biashara siyo kampuni ya kiislamu!

Hao watetezi waliojiteua wenyewe wajulishwe kwamba DP World inafanya kazi zake kwa kutumia kanuni za biashara zinazotumiwa na walimwengu wote, kampuni hii haitumii aya za Korani kwenye operesheni zake.

Kwahiyo ikiwezekana Afisa uhusiano wa DP World aje Tanzania, afanye “press conference” ya kusafisha hali ya hewa ili mkataba wao usiendelee kuwafarakanisha Watanzania.

Mojawapo kati ya hayo yanayotakiwa kusafishwa kwa haraka ni hiyo dhana ya kuinasibisha kampuni ya DP World na dini.

DP World inabidi ijiweke mbali na hao waislamu wanaojifanya kuitetea, wengine wamethubutu kuutetea hata mkataba wasiousoma wala wasioujua!

Watu wa aina hii wanaotetea wasichokijua, kiuhalisi wanaichafua Kampuni, wengine wanaichafua zaidi kutokana na historia yao mbaya, waliwahi kuvunja Bucha za nguruwe enzi za utawala wa awamu ya pili ya Alhaji Ally Hassan Mwinyi, tena wakachoma makanisa kwenye utawala wa awamu ya nne wa Rais Kikwete.

DP World haiwezi kutetewa na watu wa aina hiyo wenye historia mbaya, inabidi kampuni hiyo iwaambie wazi hao waislamu, kwamba haiuhitaji kabisa utetezi wao! Kwasababu badala ya kufanya utetezi wanaugeuza kuwa uchafuzi.

DP World iwaeleze wazi hao waislamu kwamba kampuni inao wataalamu wake, wawezao kuitetea vizuri zaidi kuanzia kwenye nyanja ya sheria, biashara, hadi kwenye nyanja ya diplomasia, yaani uhusiano wa kampuni na watu wa mataifa mengine.

DP World ni kampuni iliyojitosheleza, haiwahitaji kabisa hao waislamu wanaojituma wenyewe kuitetea! ikiwa kuna waislamu wenye hamu ya kupambana na Wakristo, ama wapo waliodhamiria kushindana na Maaskofu, basi watafute jukwaa lingine nje ya suala la uwekezaji ambalo ni la kiserikali 100%. Tena wasiitimize hiyo nia yao kwa kutumia mgongo wa DP World ambayo ni asasi ya kiuchumi.

Ni vyema kwenye hiyo “press conference” akaweko pia mwakilishi wa serikali kupigilia msumari, kwamba hata utawala wa Samia hauwahitaji waislamu wawe ndio watetezi wake. Samia akiwa kama Rais wa nchi, anao wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja za kitaalamu, wawezao kutetea mazuri yote ya serikali ambayo imedhamiria kuwafanyia wananchi wake.

Samia akiwa kama Mwenyekiti wa CCM anao wataalamu wake ndani ya chama chake, wawezao kumtetea vyema kisiasa, wawezao kujenga hoja za kisera na hoja za kiutawala, zinazotofautiana kwa mbali kabisa na hisia za kidini.

Kwenye dini inajulikana wapo wenye vipaji vya kuhubiri, ambao kupitia mahubiri yao, wanaweza kuamsha hisia zilizolala za waumini wao. Lakini watu wa aina hiyo hawahitajiki kusimama upande serikali kama mawakili wa utetezi. Hao wakijitumbukiza kuwa upande wa serikali wanazidisha uchafuzi.

Uchaguzi mkuu unakaribia wala hakuna namna yoyote ya kuuepuka, ifikapo 2025 Watanzania watalazimika kumchagua Rais!

Mwelekeo ni kwamba ndani ya CCM hakuna mwenye ujasiri wa kumwambia wazi Samia, kwamba umechafuka mno, huchaguliki, wacha CCM iteuwe mgombea mwingine anayeuzika.

Kutokana na huo utamaduni wa woga na unafiki, walio karibu na Samia watamwambia MAMA gombea tu, utashinda, huku wakijua hatashinda, ila kwa minajili ya kulinda ulaji wao, wamejiaandaa kumtangaza kama Rais kwa kipindi cha pili.

CCM ikiingia kwenye uchaguzi mkuu huku mgombea wake Samia akiwa amechafuka sana, hapo ni wazi ushindi wa CCM utategemea mbinu mbadala.
18. Hizo njia mbadala kama “rigging” ama kumtangaza kibabe kuwa mshindi hata kama atakuwa ameshindwa, ndizo zitaipeleka nchi kwenye machafuko ambayo hayajawahi kutokea tangu Tanganyika ipate uhuru.

Ndio maana sisi sote tunaoitakia mema nchi yetu, tunasema ni vyema Samia akajisafisha, ili walau aingie kwenye uchaguzi akiwa amevikwa haya mawili “kupendwa na kuaminika.” Walio karibu naye wanaweza kumdanganya kwamba MAMA gombea na utashinda, lakini “candidate” anapogombea huku akiwa haaminiki kuna hatari mbili zisizozuilika.

Hatari ya kwanza ni hiyo ya kupoteza ama shindwa, kwamba Samia anaweza kutoswa kuanzia ndani ya chama chake CCM hadi serikalini, kwani hao wakiamua kufanya kweli wanao uwezo wa kumwangusha. Kwasababu wanazijua mbinu zote mbadala, ambazo CCM imezitumia siku zote kujipatia ushindi.

Sijui hao wanaoamua kuchafua hali ya hewa wanatarajia Samia atashinda kwa muujiza gani! Muujiza wa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano?

Hatari ya pili ni hiyo kwamba Samia anaweza kubebwa, kwa nguvu za dola akatangazwa mshindi, lakini nchi isitawalike!

Mungu Ibariki Tanzania
Na hakuna dola inayoweza kumbeba ikiwa anampa mwarabu ardhi aimiliki kama yake hata manowari ya kivita anaweza kuipaki bandarini.
 
Back
Top Bottom