DP World wameachia Bandari? TPA yatangaza kutafuta Mzabuni kuhudumia Makasha katika Terminal II

Kumbe bandari haijauzwa!
 
Hivi umeusoma hata ule mkataba wa IGA, au unaimba tu hapa kama kasuku?!

Nenda kasome zile terms za hovyo kule usituimbie taarabu zako hapa.
Uelewa wako mdogo sana. Hizo terms zingekuwa na matatizo hao mabosi wa TPA wangepata wapi mamlaka ya kuandika hilo tangazo la kumhitaji muendeshaji mwingine?.

Tafuta mtu mwenye uelewa wa kitu wa kina ili upate shule kiasi kwamba unapokuja kuandika kitu uwe angalau kwa asilimia sitini unaelewa unaandika nini.
 
IGA unayosema wewe ni ya DPW, ina uhusiano gani na huyu mwekezaji mpya anayetafutwa?.

Tatizo lile lile la Tanzania kila mtu kujifanya anajua kila kitu, kumbe anaishia kuchekesha tu watu.
Ndio maana nimejua wewe ni kichwa maji usiyejielewa, hujui hata kama ile IGA ya DPW itaingilia sehemu ya majukumu ya huyo mwekezaji kama akiwa tofauti na hao waarabu, kasome ile IGA usipotezee watu muda hapa na kelele zako
 
Hivi umeusoma hata ule mkataba wa IGA, au unaimba tu hapa kama kasuku?!

Nenda kasome zile terms za hovyo kule usituimbie taarabu zako hapa.
Sasa kati ya wewe na yeye nani aliyesoma akaelewa? Nyie si mlisema Bandari kauziwa DP World, iweje TPA atangaze kukodisha mali ya mtu?
 
Waraka wa Kanisa unakataa kubinafsisha wao wanataka serikali iendelee
Kwa maelezo haya, nina uhakika haujausoma. Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya watu hawakuusoma waraka wa TEC, badala yake walisimuliwa misikitini na kwenye vijiwe vingine kuwa Maaskofu wa RC wanakataa uwekezaji
 
Hao wajinga ndio wamejazana humu na viswali vyao vya kitoto.
 
Ndio maana nimejua wewe ni kichwa maji usiyejielewa, hujui hata kama ile IGA ya DPW itaingilia sehemu ya majukumu ya huyo mwekezaji kama akiwa tofauti na hao waarabu, kasome ile IGA usipotezee watu muda hapa na kelele zako
Hujui unachoandika mkuu denooj. Kama IGA ingekuwa na nguvu hapo bandarini, hilo tangazo lisingeandikwa na boss wa TPA.

Na hilo sio tangazo la mwisho, kuna muendelezaji anatafutwa kwa ajili ya bandari ya Mbamba bay. Kuna mwingine atatafutwa kwa ajili ya uendeshaji wa bandari ya Bagamoyo, na kuna wengine watatafutwa kwa ajili ya Bandari ya Ziwa Tanganyika.
 
Narudia tena, kasome IGA yote ndio urudi hapa, kulazimisha kuwaamini TPA ambao walishajichanganya toka mwanzo kwa taarifa zao ni ujinga, nenda kasome ile IGA uje hapa uniambie TPA wana nguvu gani baada ya mwarabu kupewa bandari, Sawa?
 
Hivi unajua ile IGA ina kipengele kinachotaka mwarabu awe wa kwanza kujulishwa juu ya fursa mpya za kiuchumi zitakazojitokeza?

Kama unajua, niambie, hiyo bandari ya Bagamoyo, huko Mbamba Bay na nyingine sio fursa mpya za kiuchumi kwa mwarabu?

Halafu nikiwaita hamna akili mnaona nawaonea!.

Hebu kasomeni ule mkataba, wacheni kelele zenu.
 
Kwani lini na wapi DP World walipewa kuendesha bandari?

DP World hawana mkataba hata mmoja wa kuendesha bandari, msudhani Tanzania hii kila mtu ni mjinga mwenzenu.

Mnajitekenya wenyewe na kujichekesha wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…