DP World Washusha Meli yenye Kontena 4,000 Dar Port. Meneja TPA asema ni matokeo ya uwekezaji, adai huo ni Mwanzo tu

DP World Washusha Meli yenye Kontena 4,000 Dar Port. Meneja TPA asema ni matokeo ya uwekezaji, adai huo ni Mwanzo tu

Hao ni waongo tu, kuna meli zimefika 13/6 na bado hazijashusha mizigo lkn hiyo iliyofika jana eti itakaa kwa muda wa siku 5 tu. Je kwa nini meli zilizofika tarehe 17 mbona hazijapangiwa siku ya kusha?
Watu wanamizigo ya tarehe 10/04 hawajapata pale Yoonek Cargo Hadi Sasa afu tunapigwa fix za kijinga
 
Mleta mada hacha kuleta sifa ili tusifie utuone chawa au wajinga

leta taarifa kamili hy meli inaitwaje? Inamilikiwa na nchi gani au kampuni gani?

imetoka wapi na inaenda wapi baada ya kutoka tz

tusije kufurahia kumbe imeleta silaha na vifaru kwaajiri ya M23 Alafu 2027 waje wavamie tz kwa kutumia hzo silaha
Isije kuwa inashusha makontena 1000 baadae yanasepa.
Au makotena yanashushwa hawalipo kodi wala ushuru.
 
Yah nimeitafuta hii Habari sijona mtandaoni ila nakumbuka hilo
 
Haya Sasa DP World wameanza kufanya Yao Dar Port Kwa kuleta meli kubwa zaidi ,urefu zaidi ya mita 300👇👇


Kampuni ya DP World iliyoingia ubia na Serikali kwa ajili ya uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam imeingiza meli ya kwanza yenye urefu wa mita 294.12 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji na maboresho yanayofanywa na kampuni hiyo katika kuendesha bandari hiyo.

Hayo yameelezwa na meneja mizigo mchanganyiko wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA, Abed Galusi.

My Take
Kasi ya kuondoa mzigo ili.kuepusha Msongamano itaendana? 👇👇
Meli kubwa ya MSC ADU V iliyobeba makasha 4,000 imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa meli yenye mzigo mkubwa wa makontena kuwasili Tanzania.

MSC ADU V iliyotengenezwa mwaka 2005 ina urefu wa mita 294.12 unaokaribiana na viwanja vitatu vya mpira wa miguu imetia nanga leo Jumamosi Juni 22, 2024.

Akizungumza na wanahabari Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abeid Gallus amesema ujio wa meli hiyo umetokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari hiyo na uwekezaji wa Kampuni ya DP- World.

Gallus amesema bandari ya Dar es Salaam imefanya maboresho katika kina cha maji na ununuzi wa vitendea kazi vya kisasa.

Amesema mwanzo kulikuwapo na kina cha mita nane hadi 12.7 sasa hivi kipo 14.5 chenye uwezo wa kuingiza meli yenye urefu wa mita 305 na kina 13.5.

"Hii ni historia kwetu hapo mwanzoni tulikuwa tunaingiza meli zenye urefu wa mita 267, tumeongeza uwezo wa bandari yetu ya Dar es Salaam katika uingizaji wa meli.

"Uwezo wa utendaji kazi wa bandari ya Dar es Salaam utazidi kuimarika zaidi kwa sababu hivi sasa tuna mwekezaji mpya DP World aliyeanza kazi na mabadiliko yameonekana mfano ni meli hii kubwa,"amesema Gallus.

Gallus amefafanua kuwa katika usafirishaji ukipokea meli kubwa unaongeza kiwango cha mizigo unaokuja katika bandari husika sambamba na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo.

Pia Soma
- Bandari ya Dar es salaam yazidi kupokea meli kubwa duniani
Mama anauza nchi tu!
Hakuna kitu hapo!
 
Back
Top Bottom