DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kampuni ya DP World ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeanza kushusha vifaa katika Bandari ya Dar es Salaam kuanza uwekezaji.

Aidha, TPA imebainisha kuwa makabidhiano ni tangu Aprili 7, mwaka huu bila kuathiri uendeshaji wa bandari hiyo. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alisema hayo Dodoma akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa katika Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Mrisho alisema DP World ambao wataendesha gati namba moja hadi saba, wameshusha meli nzima yenye vifaa vya kisasa ikiwamo mashine nane za RTG, mashine nyingine 19 za kushusha kontena, jenereta kubwa za kuendesha mashine hizo na mashine nyingine nne ziko njiani.

DP World_bandari.jpg
 
Ccm wamekubali kwamba DP World wana akili kuwazidi wao wote pamoja na mwenyekiti wao. Kama DP World wanaweza kuendesha bandari kwa ufanisi kwanini serikali ya ccm isiweze? Hawastahili kuwepo madarakani kabisa.
 
Hata kama wametoa ushuru stahiki, wakitaka kuzipiga wanaozifikia watazipiga tu
Meli nzima sio mchezo. Humo kuna mpaka marashi?😌...fanicha za nyumba n.k n.k?

Yani bado watakuwa wanapata tax Incentives hapo kama sikosei, manake ule Mkataba unawataka Serikali "Wafanye kila waliwezalo" kufanikisha gawio lao. Acha tu. Watazipiga watazipiga.
 
Yes kama kuna wa kulaumiwa ni serikali na si mwingine
 
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kampuni ya DP World ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeanza kushusha vifaa katika Bandari ya Dar es Salaam kuanza uwekezaji.

Aidha, TPA imebainisha kuwa makabidhiano ni tangu Aprili 7, mwaka huu bila kuathiri uendeshaji wa bandari hiyo. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alisema hayo Dodoma akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa katika Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Mrisho alisema DP World ambao wataendesha gati namba moja hadi saba, wameshusha meli nzima yenye vifaa vya kisasa ikiwamo mashine nane za RTG, mashine nyingine 19 za kushusha kontena, jenereta kubwa za kuendesha mashine hizo na mashine nyingine nne ziko njiani.

Wamwambie Msukuma aende akashangae tena sasa wamesogea
 
Chadema wamewanywesha kangara hata tafakari hamna tena!,
Sasa na wewe, hapo ndio umetafakari mpaka mwisho wa fuvu? Hivi hukuona CHADEMA walivyoshirikiana na Uongozi wa Juu kufanikisha ugawiaji huo? Nyuma ya pazia ya Maridhiano. Siwezi kusahahu walivyozima vuguvugu lile kwa kutowapa Ushirikiano "Sauti ya Tanganyika" Siwa samehi kwa hilo. Haijalishi, mimi sio CHADEMA ni CCM-very green.
kila jambo ni kulaumu kwa uchungu tu,
Sioni ajabu kwamba huna Uchungu na Nchi hii-Umedhihirisha hayo katika posti zako nyingi tu- kwangu mie sio uchungu, ni ukweli. Bandari imegawiwa. Tafuta posti zangu, nimekuwa nikisema hivyo hata kabla CHADEMA hawajatia neno.
bila akili.
::Tunataka kuona tija ya maboresho haya, kama taifa.

Maboresho yalishafanywa na Watanzania, kwa Matrilioni. DPW hakuna kitu wameweka pale, Usipotoshe
 
Back
Top Bottom