DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Ccm wamekubali kwamba DP World wana akili kuwazidi wao wote pamoja na mwenyekiti wao. Kama DP World wanaweza kuendesha bandari kwa ufanisi kwanini serikali ya ccm isiweze? Hawastahili kuwepo madarakani kabisa.
Uingereza wamewatumia DP World wao nao hawana akili? Dunia imebadilika hata Mwalimu alishajua sera za Ujamaa zimefeli akaacha mabadiliko yaendelee.
 
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kampuni ya DP World ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeanza kushusha vifaa katika Bandari ya Dar es Salaam kuanza uwekezaji.

Aidha, TPA imebainisha kuwa makabidhiano ni tangu Aprili 7, mwaka huu bila kuathiri uendeshaji wa bandari hiyo. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alisema hayo Dodoma akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa katika Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Mrisho alisema DP World ambao wataendesha gati namba moja hadi saba, wameshusha meli nzima yenye vifaa vya kisasa ikiwamo mashine nane za RTG, mashine nyingine 19 za kushusha kontena, jenereta kubwa za kuendesha mashine hizo na mashine nyingine nne ziko njiani.

Watasema Rais Mzanzibari ameuza Mali za Tanganyika.

Kuishiwa ni kubaya sana
 
Wqmeleta mitambo iliyokwisha tumika!
Mitambo gani? Watanzania tumekopa, na tuanenda kuzilipa fedha zote, wenyewe, kwa mitambo na maboresho yote tuliyoanza kuyafanya since 2017. Wanachokifanya hawa DPW ni kukaa kwenye viyoyezi tu. Nothing more. Kwa lugha nyingine, ni waendeshaji tu.
 
Lissu angeweza kuendesha na kababu kake ka ubelgiji! ๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Hiyo haiondoi ukweli kwamba ccm yote hakuna mwenye akili na ushahidi ni huo wa mfano mmoja tu wa bandari, kwa miaka zaidi ya 60 inashindwa kuendesha bandari kwa faida wanazidiwa akili na kikampuni kilichoanzishwa mwaka 2005 kipindi ambacho Kikwete anaanza ngwe yake ya kwanza ya urais Ccm muache kuhadaa wananchi, hamna mnaloweza zaidi ya kuiba na kujilimbikizia mali kifisadi. Inakuaje kampuni inakuwa na ufanisi kuliko serikali ambayo hata kodi hailipi?
 
Gati namba 1 hadi 7?

Mbona walisema wanapewa Gati moja?

Huyu malikia wetu jamani
Kuna watu wanafanya matembezi miji mbalimbali hawajui wanataka nini wakati wananchi tumedanganywa kuhusu bandari wala hawana hii habari.
 
Hiyo haiondoi ukweli kwamba ccm yote hakuna mwenye akili na ushahidi ni huo wa mfano mmoja tu wa bandari, kwa miaka zaidi ya 60 inashindwa kuendesha bandari kwa faida wanazidiwa akili na kikampuni kilichoanzishwa mwaka 2005 kipindi ambacho Kikwete anaanza ngwe yake ya kwanza ya urais Ccm muache kuhadaa wananchi, hamna mnaloweza zaidi ya kuiba na kujilimbikizia mali kifisadi. Inakuaje kampuni inakuwa na ufanisi kuliko serikali ambayo hata kodi hailipi?
Kwani ccm inamiliki meli? We mpuuzi nini?
 
Juhudi zote hizi zilete ongezeko la mapato kwa taifa na si vinginevyo!
Tungefurahi kuona tunapatiwa update za ongezeko la mapato kila wakati bila kupikwa kisanii.
Bunge la mwakajana lililokaa kujadili mkataba wa DPW walisema

Mapato ya serikali kwasasa ni 7 trillion ila dpw akianza kazi yatafikua 26trillion acha tuone kama ni kweli au siasa.
 
Uingereza wamewatumia DP World wao nao hawana akili? Dunia imebadilika hata Mwalimu alishajua sera za Ujamaa zimefeli akaacha mabadiliko yaendelee.
Ishu sio DP World bali kushindwa kwa ccm. Kama walishindwa kudhibiti wizi bandarini watawezaje kumdhibiti Dp World?
 
Mimi, Lissu, Erythrocyte na CHADEMA yetu tumepigwa under belt tena au kwenye chembe ya moyo!๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜„
 
Back
Top Bottom