DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

HABARI KUBWA NA YA KUHUZUNISHA ni kuwa watachukua port zote zenye manufaa kwao (watachagua wao) maana lengo ni kukamata mpaka nchi za jirani kibiashara
Hapa ndio maana watakaobaki waliambiwa kuna Ridandasi
 
Mimi binafsi napenda uwekezaji, ila uwe na tija kwa taifa, pia serikali ilituambia kua baada ya ile IGA kutafuata uwekezaji kamili. Ambapo kila hatua itakua na mikataba yake, mfano dp world wanataka kujenda bandari ya nchi kavu vigwaza, utaratibu na sheria zote za kiuwekezaji itatakiwa zifuatwe kusudi taifa linufaike na uwekezaji huo.

Hivyo kama kweli serikali ina nia njema kwa uwekezaji wowote mkubwa kwenye nchi yetu, ijaribu kua na uwazi kwenye kila mikataba inayoingia na wawekezaji, hii itapelekea sisi wananchi kuiamini serikali yetu kua kila inachofanya ni kwaajiri ya maslahi ya taifa kiujumla.

Hivyo tatizo sio dp world! tatizo hapa ni uwazi tu ili watanzania tuwe tunajua tunachonufaika na uwekezaji.
 
Back
Top Bottom