DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Wafanyakazi walihoji baada ya hiyo miaka 30 tutaenda wap ?

Muarabu:msiwe na hofu mm nipo na nitaendelea kuwepo kwa zaidi ya hiyo miaka 30
Hii itakuwa propaganda akili ya kuambiwa changanya na yako kiuhalisia asilimia kubwa ya wafanyakazi Kama sio wote wamebakiza chini ya Miaka 30 kustaafu .

Rasmi imetamkwa wamechukua gati 4 Mpaka namba 7 .

Katiba ya nchi inasema ardhi ni Mali ya taifa , watumiaji wowote huwa wanakodi kwa
Miaka kadhaa.

Uvivu , uzembe na wizi bye bye .
 
msiwatishe waache wajiunge na mwarabu waachane na upuuzi wa kikokotoo, kama mwarabu anaboresha maslahi kwa asilimia 60 juu ya wanachopata Mungu awape nini tena? wakimbilie kwa mwarabu nchi imeshauzwa hiyo wanaojifanya kukomaa peleka nyasa huko na mwanza.
Hiyo 60% ni kwenye mshahara tu lkn kwa ujumla maslahi yanaongezeka Mara 3 zaidi
 
Mbona ujataja Berth Zero - Kwa ajili ya magari. Hii pia imeenda 😀
Halafu unavyosema vifaa vya kisasa...umeona tafauti yake na vifaa vilivyopo?
Vifaa vilivyoshuka mpaka sasa na vinavyokuja ni cha kisasa mno baada miezi 3-7 nadhani hii bandari itakuwa na uharaka saana wa kupokea na kushusha mizigo MASHINE ZINAZOSHUKA SI HABA
 
Sio mbaya, waliopo wapige tu hizo hela za mwarabu mana hakuna namna, tumeshauzwa.
 
mbona dawa ni ndogo tu kama ameichukua jumla, kuitafuta Tanganyika hadi ipatikane, halafu mwarabu ataitafuta Tanzania aliyoingia nayo mkataba, atembee kwa mguu hadi dubai juu ya maji (kidding), though kama anaongeza maslahi na kama ataongeza kweli ufanisi, ngoja tumwangalie anachofanya, aifanye bora kama zile za dubai hapo labda tutamsamehe.
DP kapania saana kuifanya hii port kuwa ya kisasa
 
Ni muda tu utasema Mzee nakuhakikishia kuna watu wamekaa kimya ngoja washike madaraka utakuja kuniambia
Wafanyakazi wanaotaka kwenda DP walihoji hichi kitu kuwa endapo siasa zitabadirika na kuingia kiongozi mwingine akavunja huo mkataba je wao maslahi yao yatakuwaje

Muarabu akajibu kuwa kwa mkataba waliongia sio rahisi kichaa yoyote kuthubutu kuuvunja (muarabu kajihakikishia usalama) kwa kuzingatia siasa zetu
 
Bro hii nchi huijui mkuu. Watu waliohongwa hapo wakikamatwa watataja kila kitu. Na wakikubali kutoa ushahid mahakaman jins DP World walivyotoa rushwa kupata hiyo tenders unavunja mkataba. Kuna magufuli mwingine atakuja tu we subiri.
 
Kwa manufaa ya vizazi vyetu vijavyo naunga mkono sekta nyingi tu zibinafisishwe ili kizazi kijacho kiadopt utendaji kazi wa wenzetu sio huu ujinga wa kiafrica uliopo sasa
Tungeanza na ikulu, ingependeza sana tukibinafsisha ikulu, ili viongozi wajao wajifunze.

Kifupi tunahitaji kutawaliwa upya, tumeshindwa kujiongoza kuelekea maendeleo.
 
Hiyo 60% ni kwenye mshahara tu lkn kwa ujumla maslahi yanaongezeka Mara 3 zaidi
sasa kama ni hivyo wanashangaa shangaa nini kukimbia fasta , yaani mtumishi wa serikali wa kibongo anajikuta sana hata kama anapokea aftatu kwa mwezi hajielewi kabisa sijui wanawaroga ndiomaana alipokuja jiwe alihangaika nao sana mara kawafukuza mara sijui hawana vyeti lakini wamo tu wala hawashituki, maslahi madogo bado wanalambalamba makalio ya siisiiemu.
 
DP kapania saana kuifanya hii port kuwa ya kisasa
aifanye ili atuprove wrong, ama la asifikiri ameuziwa mazima na milele, kuna siku Tanganyika itazaliwa, watu wakiona wanaletewa ujinga watazalisha Tanganyika na yeye atabidi atafute Tanzania ipo wapi aliyoingia nayo mkataba. na watu wajue, kwanini wabara hawajawahi hata siku moja kushupalia issue ya Tanganyika hadi Mzanzibari alipoingia na kugawa bandari na mbunga? why now? ni kwasababu wameona kama maslahi ya watanganyika yanadhulumiwa na wazanzibari wanadekezwa kuanzia kina fei toto kwenye yanga wanatetewa hadi mtu mkubwa wa mwisho kwasababu tu rais katoka kwao. tuambiwe na umeme waliodaiwa kipindi cha magufuli walilipaje na kama walisamehewa kwanini sisi wengine wasitulipie.
 
Vifaa vilivyoshuka mpaka sasa na vinavyokuja ni cha kisasa mno baada miezi 3-7 nadhani hii bandari itakuwa na uharaka saana wa kupokea na kushusha mizigo MASHINE ZINAZOSHUKA SI HABA
Tatizo.....ujanipa jibu sahihi.....mpaka sasa wameleta vifaa gani?
 
Back
Top Bottom