DPP amuondolea shtaka Abdallah Zombe

Felesi siyo Biswalo, angalia ndugu ingawa cheo cha DPP ni kile kile ila watumishi ni tofauti.
Kwa Jaji Dkt Feleshi pale JPM alichemsha, hakuna mtu anaweza muingilia Feleshi eti kwa rushwa, pia jamaa ni mchapakazi balaa, uliza mwanasheria yeyote wa serikali atakuambia bosi wao huyo wa zamani alivyo mwadilifu.
 
Sawa...acha wafarijiane tu hapa duniani kwa kusafishiana majina ila kama kweli alimwaga damu au alishiriki kudhulumu nafsi ya mtu,ataipata adhabu yake siku atakapofunga macho yake.
Mauaji ya wale wafanyanyabiashara yalikikuwa hivi: Kipindi kile walichouawa kulikuwa na wimbi kubwa la ujambazi. Amri ikawatolewa kutoka juu kwenda kwa wakuu wa polisi wa Mikoa yote kuwa ''majambazi washughulikiwe kwa nguvu zote tena ikibidi wauwawe wanapokamatwa bila kufikishwa mahakamani ili kutoa onyo kwa majambazi''. Sasa siku walipokamatwa wale wafanyabiashara kulikuwa kumetokea tukio la ujambazi. Baada ya polisi kuwahisi na kuwakuta na kiasi kikubwa cha fedha wakachukulia (kwa uzembe bila kufanya upelelezi wa kina) ni majambazi. Wale polisi waliowakamata wakawasilina na Zombe kuwa majambazi wamekamatwa. Zombe akatoa amri kuwa ''na wauwawe''. (Kumbuka Zombe alipotoshwa na askari wale waliowakamata wale majambazi na yeye akatoa amri ya kizembe bila kuhakikisha zaidi). Halafu kuna jambo jingine la muhimu ambalo ndilo lililochochea mauaji yao. ie. Polisi waliowakamata waliingiwa na tamaa ya kumega zile fedha walizowakuta nazo. Zile fedha ndizo hasa ziliwapofusha polisi macho ''kuulizia zaidi'' kwani waliona kuwa wakiwaua itakuwa rahisi kwao kumega zile fedha. Hivyo hii kesi si Zombe wala si wale polisi watakaofungwa. Hii ni kwasababu wale waliotoa amri (serikali) wanajua kabisa mauaji yalifanywa kutokana na amri yao japo uzembe ulitumika. Ndio maana siku zote watu wenye weledi wanasisitiza mhalifu yoyote ahukumiwe na mahakama na si vingine.
 
MIMI NILISHASEMA SERIKALI YA RAIS JPM UENDA ITAGONGA MWAMBA NA KUSHINDWA VIBAYA KWENYE VITA VYA UFISADI NA RUSHWA KAMA OFISI YA DPP NA MAHAKAMA WATU WATAKUA WALE WALE.MAFSDI,WAUAJI,MAJAMBAZI WAKISHIKWA NA KUSHTAKIWA OFISI YA DPP NA MAHAKAMA WATAKUA WANAWAACHIA NA KUENDELEA KUPGA HELA,AINGII AKILINI KILA KESI ZA VIGOGO NA ZA PESA NYINGI SERIKALI INASHINDWA WHY?LAKINI KESI YA RUSHWA YA MWENYEKITI WA MTAA KAOMBA RUSHWA YA ELFU KUMI ANAFUNGWA NA MAHAKAMA UTASIKIA INASEMA HILO NIFUNDISHO KWA WENGNE.HAPO HAMNA KITU TUNACHEZEA WAKILI TU.
 
una mshtaki mtu kwa kosa la mauaji, harafu unakuja na rufani ya kosa la kuficha wauaji? DPP anajua anachokifanya kweli?
Hivi ofisi ya DPP kuna wanasheria kweli wanaostahili kuitwa Wanasheria? Rufani ni juu ya kuachiliwa kwenye Kosa la Mauaji halafu unakuja badilisha shitaka hilo katika hatua hii kweli??!! Siyo kosa wala si dhambi kukubali kushindwa katika kesi maana yote ni matokeo. Mwachieni Zombe aendelee na shughuli zake amesumbuliwa vya kutosha sana.
 
Tuna vijana wanasheria wazuri tu wanamaliza vyuo vikuu kila mwaka ingekuwa ni vizuri wapate kazi katika hii ofisi ya DPP.
 
Haki iko mbinguni tu....... ,mnawatia uchungu wanafamilia waliopoteza ndugu zao katika mauaji yale ya kikatili kama kumuachia Zombe mlishamuachia basi muachieni tu atakutana na noma zake siku ya kiama.
 

Hivi kumbe hata wao kwa wao wanaweza kubadilishiana kesi???? Nilidhani ni kwa watu wanyonge tuuu!!!!!!!
 
Hakuna cha ajabu hapo...Huyu DPP ndo jukwaa la maigizo...Hii kesi ilishakwisha..zimebaki stori tu
 

Kwani Mzee wangu DPP amekwambia anataka kushinda kesi au anataka HAPA KAZI TU!!!!!!!!!!!!!Ili aonekane anafanya kazi basi hata kesi ya Paka kula panya ataipeleka mahakamani
 
Wangeacha kuhangaika tu maana wanapoteza muda na fedha. Ukweli unajulikana nini Zombe na wenzake walifanya lakini udhaifu wa upelelezi na uendeshaji wa mashitaka ndiyo uliofikidha hapo. Ndiyo maaan binafsi nafikiti kuanzidha mahakama maalumu kwa ajili ya makosa fulani ni kuacha uhalisia wa tatizo. Tuwape uwezo hawa, yaani wapelelezi na waendesha mashitaka, na tutashind maovu.
 
rufaa imetupiliwa karibu, unaweza kuiokota na kuirudisha tena kotini
 
Tuna vijana wanasheria wazuri tu wanamaliza vyuo vikuu kila mwaka ingekuwa ni vizuri wapate kazi katika hii ofisi ya DPP.
unaweza kuwalipa?! wanaenda katika makampuni ya sheria yanayolipa vyema.... wana changamoto nyingi za kimaisha, wanafata kwenye mkwanja wa kutosha.
 
Wafanyabiashara waliuawa sinza kwenye ukuta wa posta wakisemekana walikuwa wanatoroka na vile vile hao askari waliofanya mauaji walikubali kuwa walitumwa kufanya hvyo. Mpaka mwaka 2010 askari hao wapatao tisa walikuwa washafariki mmoja mmoja kwa nyakati tofauti wakiwa ktk harakati za kutoa ushahidi nakumbuka alibaki mmoja ambaye hali yake kiafya haikuwa nzuri hvyo kupelekea naye kufariki, na mchezo ukaishia hapo.
 
Ndo kilichokuwa kimelengwa muda mrefu. Sasa kesi ndo imekuwa lainiiiiiiiii!! . Zombe vs Republic , the accused is going to win smoothly
 
Hiv Zombe alisha staafu au?
 
Nasoma hapa na kujiuliza hivi ni kesi mpya ama ileee ya mabwepande?
Zombe Ana matukio!
 
Kwa taarifa yenu yale yalikuwa majambazi yaliyokubuhu na alichofanya huyu kamanda kilikuwa sahihi kabisa na kinafanyika duniani kote, kosa lake alijichanganya kidogo tuu! Na huu ndo ukweli mchungu, ukitaka meza, ukikataa tema!
Ukishajua mtu ni jambazi wewe kama askari (mtoa comment), unabeba bunduki yako na kuwaua. Ndivyo? [emoji15]
 
haishangazi sanaa labda kama angehukumiwa kifungo cha maisha ndo ningeshangaaa.wakubwa wengi wa wanao patikana na na makosa ya kifungo huwa niwale tu wanao amua kutolewa kama sadaka wa kafara.
 
Nchi hii inatia kinyaa,yani mtu aue watu alafu sasa wanaanza kufanya ujanja wa kumuachia aisee hili ni jipu mkuu magufuli aone hili amtumbue uyo dpp haraka sana haiwezekani mtu aue watu alafu leo wanataka kumuachia hii si haki hata kidogo huu ni mchezo mchafu magu aingilie kati hatuna wanasheria wa serikali kwenye hii nchi ni uozo mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…