DPP anaposhindwa kuendesha kesi kwa MIAKA MINNE si ashitakiwe?

Asante Mama kwa kusikia kilio cha wapenda haki!!
DPP Biswalo OUT!
 
Asante Mama kwa kusikia kilio cha wapenda haki!!
DPP Biswalo OUT!
Kwa kweli KUDOS kwa Mama.
Mambo mengine ya uonezi kiserikali , au kwa matakwa ya mtu mwenye madaraka yanaumiza watu sana.
Mama Samia ubarkiwe sana kwa kusikia kero hizi.
 
Haya mambo ya kuwekana ndani indefinate sasa yatapunguwa kama c kuondoka kabisa kwa sababu yule aliyekuwa anatowa amri mungu keshamchukuwa na yule mtekelezaji leo hi ameshaondolewa na Rais.
 
kwani dpp ndio mpelelezi wa kesi mzee? yeye ndiye aliwakamata?
 
kwani dpp ndio mpelelezi wa kesi mzee? yeye ndiye aliwakamata?
DPP ana mamlaka ya kumwomba Jaji au Hakimu kufta kesi kama mkamataji hana lolote analofanya, ndani ya kipindi fulani.
Kesi haiwezi pelelezwa indefinately.
 
DPP ana mamlaka ya kumwomba Jaji au Hakimu kufta kesi kama mkamataji hana lolote analofanya, ndani ya kipindi fulani.
Kesi haiwezi pelelezwa indefinately.
kwani majaji hawawezi kufanya hilo suo motu kwa kuitisha jalada na kulifanyia mapitio? kwanini alaumiwe dpp peke yake? au sisi mawakili tufungue kesi za kikatiba? tumefanya hilo ili mahakama ichore mstari kama kesi za armed robbery?
 
Tayari leo Mh. Rais kapita nae. Imechangiwa pia na lile agizo la kufuta kesi zisizo kuwa na ushahidi jamaa kakaa kimya kama hakuna agizo toka kwa Mkuu wa nchi.
 
kwani majaji hawawezi kufanya hilo suo motu kwa kuitisha jalada na kulifanyia mapitio? kwanini alaumiwe dpp peke yake? au sisi mawakili tufungue kesi za kikatiba? tumefanya hilo ili mahakama ichore mstari kama kesi za armed robbery?
Tatizo kubwa hapa , Muhimili wa Sheria na Mahakama kuliingiliwa na wanasiasa.
Wanasiasa wanaamrishaPolisi kukamata, wanawaamrisha Majaji kufunga watu, hata kuamrisha Polisi kumweka mtu ndani kwa kubambika kesi.
 
Kuna mahakama huru?
 
Kama ni kweli, kama unavyosema, DDP ameamrishwa, hivyo ni kesi za kubambika, sasa washitakiwe kwa nini ili hali umeeleza wamepewa amri?!. Manyanyaso, maonevu, dhulma, kumbambikia watu kesi, kusotesha watu mahabusu, kutotenda haki etc, issues hizi huwa zinashughulikiwa na karma. Mama Samia hataki mambo haya, na keshaelekeza yaangaliwe na yamalizwe.

P
 
Mkuu aliyeagiza kubambikwa mtu kesi ndiye anashughulikia na karma.
Haya tumeyaona maishani.

Aliyetekeleza maagizo kinyume na kiapo chake cha kazi , kushitakiwa ni sawa na iko kwenye mstari, maana sheria itamhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…