DPP anaposhindwa kuendesha kesi kwa MIAKA MINNE si ashitakiwe?

Hakuna cha mama wala nini, inahitajika mabadiliko ya sherea from the scratch system ni ile ile watu ni wale wale

Tubadili sheria zetu ziwe zenye kwenda na uhalisia wasasa, mambo yamebadilika jamani sasa ni karne ya 21
 
Mkuu karma unafanya kazi kivyako na tumeona ukienda bila upendeleo.
You reap what you down.
Lakini hatuwezi kuachia karma wakati sheria zinapindwa na ndio maana Mama Samia kasema sheria hizo hizo zitumike kuweka mambo sawa.

Kwa kesi ya Rugemalila, huyu bwana ni lazima stadia haki yake ya kimsingi.
 
Rais alikuwa ni JK pekee hawa wengine ni waigizaji tupu, JK nakumbuka watu walipiga kelele kuhusu mama wa pesa ya mboga na Ezekieli Maige akawatoa haraka sn, ikaja akina Hamis Kagasheki naye akamtoka, Emmanuel Nchimbi jambo sikuwa nimepevuka sn lakini hayo matukio nayakumbuka sn, huwezi kuwa na DPP takataka kama Mganga kwenye ofisi za umma pamoja Ole Sabaya ni mpuuzi mkubwa sn na dharau kwa wananchi.
 
Hakuna cha mama wala nini, inahitajika mabadiliko ya sherea from the scratch system ni ile ile watu ni wale wale

Tubadili sheria zetu ziwe zenye kwenda na uhalisia wasasa, mambo yamebadilika jamani sasa ni karne ya 21
Upo sahihi kabisa mkuu, tunaishi kwa hisani ya watawala, sheria za hovyo kabisa tena wamejitungia kinga za kutoshitakiwa.
 
Hiyo taasisi ya DPP ni sehemu ya vitengo katili sana, na imekuwa ikitumika kukomoa na kuumiza wote wanatofautiana na viongozi wa serikali.
Mchawi ni katiba wazee tutafute mbadala wa katiba haraka
 
Tukimpata DPP asiye na maadili (ethics), hizi "Plea bargain" na "Nolle prosequi" zinaweza kumfanya kuwa billionaire. Nadha hata huyu Biswalo kazitumia sana hizi.
 
Tukimpata DPP asiye na maadili (ethics), hizi "Plea bargain" na "Nolle prosequi" zinaweza kumfanya kuwa billionaire. Nadha hata huyu Biswalo kazitumia sana hizi.
Sheria yake afungwe mahabusu kwa miaka minne, wakati huo tukitafuta uchunguzi wa makosa.
 
Tayari leo Mh. Rais kapita nae. Imechangiwa pia na lile agizo la kufuta kesi zisizo kuwa na ushahidi jamaa kakaa kimya kama hakuna agizo toka kwa Mkuu wa nchi.
Una ABC zaidi kuhusu hili la kukaa kimya kwa muda baada ya agizo la president kuhusu kesi ambazo hazina msingi?
 
Kama walikula mzigo unaobebwa kwa sandarusi unawaonea hiruma ya nini?
Mungu akuepushe usije kuingia kwenye mazingira ya "kubambikiwa" kesi au ndugu yako wa karibu asiingie kwenye mazingira hayo. Hadi Rais akaamuru hilo, anajua mazingira ya ubambikiaji wa kesi yapo.
 
Kinachonipa faraja juu ya hili ni ile ahadi yake bwana wa Mbingu na ardhi na volovyomo ndani yake ya kuwa, "Kwenye kutoa msamaha wa anaedhulumu ni jukumu la mdhulumiwa pekee"
 
Mungu akuepushe usije kuingia kwenye mazingira ya "kubambikiwa" kesi au ndugu yako wa karibu asiingie kwenye mazingira hayo. Hadi Rais akaamuru hilo, anajua mazingira ya ubambikiaji wa kesi yapo.
Mkuu wamedhulumiwa watu wengi sana kwa kesi za uhujumu uchumi, kumbe lengo ni kupora mali zao au kudhulumu.
Mifano ikomingi sana.
 
DPP haombi kwa mahakama kufuta kesi, anatoa taarifa kuwa anafuta kesi. rekebisha sentensi.
Sawa mkuu, tena hapo ndio inamuweka DPP katika picha mbaya zaidi, kwa kushindwa kufuta kesi zinazoenda miaka na miaka , kutokana na kutokuwepo upelelezi unaoweza kusimama makhakamani.

Hisia ni kwamba wanafanya hivyo kwa maslahi yasiyojulikana.
Ndio maana lazima washitakiwe.
 
mojawapo ya sababu za kufuta kesi inatakiwa kuwa ni maslahi ya umma. tuwe wakweli, kwa wale mashehe kwa mfano waliokuwa wanahatarisha usalama zanzibar kipindi kile wamesababisha watu kumwagiwa tindikali, makanisa kuchomwa na mambo machafu kibao, kati ya wao kutoka au kukaa ndani unafikiri maslahi ya umma yatakuwa ni yepi? DPP anayo mamlaka kufuta kesi lakini mamlaka hayo anatakiwa kuyafanya kwa kuzingatia vigezo fulani (public interest, kutenda haki n.k). hivyo ndivyo ninavyojua.
 
Kwani huyu Sigh si tuliambiwa kuwa aliandika barua kukiri makosa na kuomba msamaha? Sasa vipi mbona bado yumo ndani na watu wameshindwa kufata amri ya Magu ambae ndie aliekuja na nadhani hii ya kutaka wahalifu wakiri na kuomba msamaha na ndio waachiwe?
 
Mkuu ile ilikuwa coercion into admission.
Staili wanayofanya wale rouge police kuminya watu sehemu za siri ili wakubali makosa.
Ambayo vile vile ni illegal.
DPP ashtkiwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…